
Masaa machache yamebaki kabla mashabiki wa soka duniani kushuhudia mechi nyingine kali katika fainali za kombe la dunia, kati ya wababe wa Ulaya Uingereza na Italia.

Nahodha wa timu ya Uingereza, Steven Gerrard amesema hakutakuwa na kisingizio chochote cha kushindwa mechi hiyo na pia kuchukua kombe la dunia mwaka huu kwa kuwa wameshajiandaa vya kutosha.
Amesema muda unavyozidi kusogea ndivyo ambavyo hamu ya kucheza mechi hiyo inavyoongezeka.
“Tuko hapa sasa. Umbali wote tuliomaliza, joto la maandalizi tumeshafanya yote hayo. Hakuna kisingizio sasa.”
Uingereza imesafiri na mashabiki wa timu 2,5000 na wengine 7,000 wanatarajiwa kuingia kwenye mechi hiyo kuishabikia timu yao ya taifa.
Hivi sasa tunahamia katika site yetu mpya inayoitwa www.bantutz.com ni katika kuboresha huduma zetu za kutoa habari za uhakika na burudani
0 comments:
Post a Comment