
Don Jazzy alifika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Mohammed, Lagos Nigeria wakati akielekea kwenye tuzo za MTV Afrika Kusini ambapo aliruhusiwa na mfanyakazi huyo kuendesha kigari hicho tena akiwa na mfanyakazi huyo pembeni.
Wakati anafanya tukio hilo alirekodi kipande cha video kisha akasafiri akiwa mwenye furaha huku akimshukuru mfanyakazi huyo kwa kuliwezesha zoezi lake.
Baada ya kumalizana na mambo ya tuzo, Don Jazzy alishitushwa na taarifa za kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo ambaye jina lake halikutajwa huku sababu ikiwa tukio linalomhusisha yeye.
Baada ya muda aliamua kumpa ajira kwenye label yake ya muziki inayomiliki wasanii wakubwa kama Dr Sid na Tiwa Savage na akaiambia dunia kupitia Instagram.
Hivi sasa tunahamia katika site yetu mpya inayoitwa www.bantutz.com ni katika kuboresha huduma zetu za kutoa habari za uhakika na burudani
0 comments:
Post a Comment