Limekuwa jambo la kawaida sana siku hizi kurekodi video na kuisambaza kwa njia ya mtandao hususan kwa kutumia mobile application kama "Whatsapp" kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia "TEKNOHAMA".Ambapo imefikia hatua kila mtu ana miliki simu zenye uwezo mkubwa "Smartphone"
Siku za hivi karibuni mwanafunzi wa kike anayesoma Chuo kikuu Cha Dar Es Salaam (UDSM),kitivo cha Sayansi Jamii (College ya Social Science -COSS), ambaye ni mwaka wa kwanza anayeitwa Ramona Swai ambaye anakaa maeneo ya Chuo (Hostel-Campus Hall 7).Na alisoma shule ya Wasichana Dakawa kabla ya kujiunga na Chuo hicho
Alijirekodi video ambayo umeiangalia {unaweza kuiangalia} hapo juu kuwa ameshindwa kusoma kwa sababu masomo ni magumu sana kitu kilichompelekea kujirekodi na kutoa rai kwa mtu yeyote mwenye uwezo mzuri wa kifedha anaweza kwenda kumuoa kwa sababu yuko tayari kuacha masomo na kwenda kuolewa kutokana na ugumu wa masomo hayo.
Kufuatia kurekodi video hiyo tuliamua kufuatilia background ya Ramona Swai na kugundua kuwa ni Mwanafunzi asiyependa kujituma katika masomo na ni msichana anayependa sana kujirusha na starehe.Anayependa kuishi maisha mazuri.
Na kilichopelekea yeye kurekodi video hiyo ni kutokana na assignments walizopewa na Mwalimu (Lecturer) anayemfundisha anayeitwa Prof. Issa kaboka Musoke ambaye aliwapa assignment ya swali lililouliza:-
{Debate on how agency and structure dichotomy theory has influenced classical sociological theory 10 pages }
Ambayo ilitolewa na assignment nyingine ambazo walipewa wiki 10 waweze kukusanya (submit) assignment 4
Lakini wanafunzi wenzake anaosoma nao nilipata bahati ya kuongea nao na mmoja wao ambaye jina lake hakupendwa litajwe nilipomuuliza kuhusiana na hizi assignment alinijibu kwamba.
"kaka yani ukiangalia upande mwingine ma-test yanaandamana tena ni
mengi na isitoshe ma-asignment mengine ndo usiseme, mpaka mtu unaugua na
wengne mpaka tuliumwa baadhi mpaka walilazwa kwa sababu mikazi inavyotutesaa wenzenu tunakesha tukifanya assignment"
Lakini baada ya kutoa video hiyo ambapo tetesi zilienea kwamba amefukuzwa Chuo ndipo aliamua kuweka "Status"hiyo juu kwenye 'Profile' yake ya 'Whatsapp'
Lakini hatukuishia hapoo sisi kama katemimethsela.blogspot.com tulifuatilia wanafunzi wenzake katika Chuo hicho wanalizungumizaje tukio hilo kwa sababu kuna wengine wanosoma vitizo vya sayansi masomo ni magumu kwelikweli siyo kama yeye anavyodai na ndipo nilipopata hii 'screenshot' kutoka katika group moja la whatsapp la wanafunzi wanaosoma chuo hicho
CHUO IMECHUKULIAJE TUKIO HILI
Baada ya video hiyo aliyoisambaza hajaonekana Chuo kwa muda kidogo lakini ameagizwa akaonane na mkuu wa kitivo (College Of Social Science=COSS) Siku jumatatu asubuhi ili kujadiliwa kutokana na kitendo hiki alichokifanya kwani amekitia doa chuo hicho ambacho ni Chuo Cha Nne kwa katika viwango vya Ubora Afrika nzima
Hili sio tukio zuri kabisa katika jamii na chuo kwa ujumla kwani anawakatisha tamaa wengine na yeye mwenyewe kutotambua umuhimu wa Elimu na kuona kuolewa kama ni jibu sahihi juu ya Ugumu wa elimu ya Chuo kitu amabacho sio sahihi
Like page yetu facebook upate habari kama hizi kwa wakati..Bofya hapa uweze ku-like katemimethsela.blogspot.com/facebook
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua hatma ya Ramona Swai katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na vilevile kupitia hii blog utapata kujua maovu,skendo.kashfa na matukio mbalimbali yanayotokea vyuo mbalimbali hapa nchini kwa muda muafaka live bila chenga na zengwe lolote.Jukumu letu sisi ni kukuhabarisha hatuwezi kuficha,kuona aibu na kuendekeza matendo maovu yanayofanyika vyuoni
0 comments:
Post a Comment