Mwanamuziki mashuhuri duniani Jennifer Lopez, amejiondoa katika shamra
shamra za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia ambazo zitafanyika mjini
Sao Paulo siku ya Al-khamisi, kabla ya mchezo wa kwanza fainali hizo
ambao utashuhudia wenyeji Brazil wakicheza dhidi ya timu ya taifa ya
Mexico.
Taarifa za mwanamuziki huyo kutoka nchini Marekani zimethibitishwa na
shirikisho la soka duniani FIFA, ambapo hata hivyo sababu za kujiondoa
kwa Jennifer Lopez hazijaelezwa kwa kina Lopez, alitarajiwa kushiriki
katika shamra shamra hizo akiwa sambamba na mwanamuziki wa miondoko ya
rap, Pitbull pamoja na Claudia Leitte kutoka nchini Brazil, kwa ajili ya
kuimba wimbo maalum wa fainali za kombe la dunia za mwaka huu ambao
unaitwa "We Are One,”
"Kufuatia sababu zilizo nje ya uwezo wetu, hatutokuwa na Jennifer Lopez,
ambae ni mmoja wa wana muziki ambao wamerikodi wimbo maalum wa fainali
za mwaka huu, ambao unatarajiwa kuwa sehemu ya ufunguzi.” Imeeleza
taarifa ya FIFA.
Wasanii 600 wa fani mbali mbali za burudani, wanatarajiwa kushiriki
katika shamra shamra za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka
huu.
Watu zaidi wa elfu sitini (60,000) wanatarajia kushudia shamra shamra za
ufunguzi wa fainali za kombe la dunia wakiwa katika uwanja wa Sao
Paulo, na wengine zaidi wataziona shughuli hiyo kupitia luninga katika
viwanja vya wazi nchini Brazil.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
Instagram yamuweka Balotelli matatani.
Shirikisho la soka FA linachunguza ujumbe
wa Instagram wa mshambuliaji wa
Liverpool Mario Balotelli unaodaiwa kuwa ni
wa kibaguzi.
Ballotel mwenye umri wa miaka 24 akijibu
shutma dhidi yake kutokana na ujumbe wake
mtan…Read More
0 comments:
Post a Comment