Ommy amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa yeye na msichana huyo
waliweza kukaa kwa muda wa mwaka mmoja wakichati bila kuonana.
“Social network zilisaidia kutuunganisha lakini matokeo yake mpaka
tukaja kuonana. Mpaka nikaja kwenye tour tukaonana, si unajua kuna zile
mzee unashangaa ma Instagram mtoto ka like picha kama tisini hivi,
halafu ukichekecha unaona mbona kama umechorwaee ,bahati nzuri
ilipoanzishwa instamessage kwa hiyo kama unajiiba hivi. Ni Mtanzania,
mpaka kuonana ilichukua kama mwaka, tumechat tumechat mpaka ikafikia
time, sina haraka kwanini niwe na haraka, kufahamiana kunakuja
automatically,” alisema.
“Unajua mambo ya mapenzi Mungu mwenyewe ndio anajua, pengine wengine
anaweza wewe ukawa muuza mkaa demu akaja kununua mkaa. Lakini lile kopo
unavyolishika kimachejo wakati wa kupima yeye anapenda ule upimaji wako,
kwahiyo kuna kitu kama hivyo haijalisha mnakutana wapi, ikiwa tu
mmewekea mipaka yenu, masharti hivi na hivi maisha yenu yanaenda.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata skendo na tetsi mbalimbali zinazowahusu wasanii.
0 comments:
Post a Comment