Timu Arsenal
imeonesha kuimarika msimu huu lakini imeshindwa tena kubeba kombe la
ligi kuu ya Uingereza na kubaki na changamoto zilezile za siku zote.
Arsenal imemaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 75 kwa michezo 38 huku
ikishinda michezo 22 na kutoka sare mechi 9 na kufungwa michezo 7 pekee
pamoja na kujikusanyia magoli ya kufunga 71 na ya kufungwa 36.
Timu hiyo ya Arsenal inatarajia kucheza mchezo wa fainali ya kombe la FA na Aston Villa mchezo ambao wanatakiwa kushinda kujifariji na kikosi chao bora msimu huu.
Mafanikio ya timu hiyo huyawezi kuyaweka mbali na uwepo wa mchezaji
nyota kikosini Alexis Sanchez aliyenunuliwa kwa Euro milion30 ambapo
ameonesha thamani yake baada ya kuifungia klabu hiyo magoli 24.
Kwa
upande wa kocha Arsene Wenger msimu huu umekuwa bora kwake kushika
nafasi ya tatu na kutegemea kucheza fainali ya kombe la FA.
Mategemeo ya msimu ujao kwao ni kuendelea kukitengeneza kikosi cha kupambana katika kampeni ya ubingwa wa England.
Kocha Arsene Wenger anasema wanajiandaa vya kutosha, pia wapo katika
mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na winga wakeTheo Walcott.
0 comments:
Post a Comment