Maafisa wa polisi wa Kenya wamemtia nguvuni mshukiwa anayetuhumiwa
kuendesha akaunti ya Twitter ambayo ina uhusiano na kundi la kigaidi la
Al shabaab na uliotoa habari kwamba Al shabaab walihusika kutekeleza
mauaji eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu.
Kwa mujibu wa Ripota Julius Kepkoech toka Kenya, Katibu wa wizara ya
Mambo ya ndani na usalama wa taifa, Mutea Iringo amethibitisha kwamba
Ismail Omondi ametiwa nguvuni Tarehe 18 June mwaka huu ambapo hata hivyo
Iringo amekanusha kwamba mshukiwa huyo hana uhusiano wowote na Al
Shabaab.
Iringo amesema, “Unaweza kuona kwamba yule anayekiri kuhusika na Alshabaab si mmoja wa kiongozi wa kundi hilo,”.
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo awali alisema kupitia ukurasa
wake wa Twitter kwamba: “Aliye kizuizini kwa sasa ni mshukiwa
anayeendesha mtandao wa kijamii unaodhaniwa kutumiwa na Al shabaab
kukiri kuhusika na uvamizi”
Hata hivyo Kimaiyo hakutoa taarifa zaidi kuhusiana na washukiwa.
Ismail Omondi ni mshukiwa wa tatu kutiwa nguvuni kuhusiana na mauaji
yaliyotokea Mpeketoni siku ya Jumapili na Jumatatu ambapo zaidi ya watu
60 wamepoteza maisha.
Mapema siku ya Jumatano, mshukiwa mwingine Ahmed Abdallah anayetuhumiwa
kumiliki gari lililowabeba wavamizi hao alikamatwa huku Salim Dyana
naye akikamatwa na polisi kwa tuhuma za kuliendesha gari lililowabeba
wavamizi kuelekea Mpeketoni Lamu.
Mlinzi mkuu wa Obama ajiuzulu
Mkuu
wa Idara ya Usalama nchini Marekani, aliyekuwa na jukumu la kumlinda
Rais Barack Obama, amejiuzulu kufuatia matukio yenye…Read More
0 comments:
Post a Comment