Facebook

Friday, 20 June 2014

Polisi walazimishwa kuishi pamoja Kenya



Kitengo cha utendakazi cha askari polisi Nchini Kenya kimekumbwa na shida ya ukosefu wa makazi.
Hali imekuwa mbaya sana katika ski za hivu punde kiasi ya kuwa maafisa wa kike na wenzao wa kiume, wamelazimika kutumia kwa pamoja vyumba vyao vichache.

Hili limetokea baada ya zaidi ya maafisa wapya 7,000, kuingizwa katika kitengo hicho miezi miwili iliyopita na kuiongeza idadi ya maafisa wa polisi nchini Kenya kwa asilimia 10.
Hali inaweza zidi kudorora mwaka ujao ikiwa vyumba vipya havitapatikana kwa haraka kwani maafisa wengine 10,000 wataapishwa kujiunga na Idara ya polisi kuhuidumia wananchi na kulinda usalama .
Mpango huo wa kupanua kitengo hicho, ulizinduliwa bungeni na katibu wa fedha Henry Rotich alipoisoma bajeti ya mwaka 2014/2015, juma lililopita.
Kuishi kwenye vibanda

Polisi nchini Kenya walizimishwa kuishi pamoja katika vyumba vyao
Katika taarifa ya makamanda wa majimbo iliyoonyeshwa wanahabari, maafisa waliamrishwa kuwakaribisha wenzao wapya katika vyumba vyao wanamoishi pamoja na familia zao.
Hii inamaanisha kuwa kurutu anakaribishwa kwa chumba anakoishi Askari na mkewe na familia yake .
“maafisa wengine wanawazuia maafisa hawa wageni kuingia katika nyumba zao na kusababisha hali ngumu kwao.
Maafisa wa polisi watakaokiuka amri hiyo watachukuliwa hatua za kinidhamu . Taarifa hiyo ilisema.
Maafisa waliozungumza na wanahabari, kwa masharti ya kutotajwa walisema kuwa amri hiyo itawanyima faragha na wake zao mbali na kuibua uhasama na ugomvi katika familia zao.
Mgogoro huo uliwalazimisha maafisa hao wapya kutafuta makao katika vibanda viliyo katika vituo vya polisi kwa hofu ya kuvunja nyumba za wenzao .
Maafisa hawa wapya walitawazwa kuwa makonstebo mwezi Aprili na kuchukuliwa katika vitengo vya Polisi ,Kitengo cha Jinai na kikosi cha kupambana na ghasia. 


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

  • Msichana mwingine ajinyonga India Wanawake wa India wapinga ubakaji ambao umekithiri mno India Msichana mmoja mwenye umri mdogo amepatikana akining'inia mtini Kaskazini mwa India. Familia … Read More
  • Obama:Iraq inahitaji msaada. Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali yake inatazama "njia mbalimbali" ikiwemo nguvu za kijeshi kuisaidia Iraq kupambana na wanamgambo. Obama amesema Marekani ina nia ya kuhakikisha wapiganaji hawachukui tena… Read More
  • AL Shabab watangaza sheria ya mavazi !   Kundi la al-Shabab limewakamata wanawake takriban 100 na kuwataka kuvaa nguo kwa mujibu wa dini ya Kiislam, vinginevyo watapigwa mikwaju. Wanawake hao walikamatwa katika mji wa Buale, karibu kilomita 300 kusini… Read More
  • Rais wa zamani wa Ivory Coast,Gbagbo kushtakiwa na ICC     Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imetangaza mipango ya kutaka kumshtaki rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo. Gbagbo anatuhumiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi alioshindwa mwaka 20… Read More
  • Mwanakikundi wa Mafia "Mafioso" ataka kuungama kwa Papa. Kigogo mmoja wa zamani wa kundi la mafia amemuandikia barua Baba Mtakatifu, akiomba kwenda kuungama na kukiri "siri tatu muhimu sana" ikiwemo moja maarufu nchini Italia ya kupotea kwa mtoto. Katika barua hiyo yenye … Read More

0 comments:

Post a Comment