Facebook

Thursday, 12 June 2014

Riyama Ali:"Nikifa Sitaki Kusifiwa"

RIYAMA Ali mwigizaji wa kike asiye na kashifa katika tasnia ya filamu Bongo, amefunguka kwa kusema kuwa kama kuna msanii mwenzake au mtu mwenye mapenzi naye angependa kama ana sifa kuhusu yeye katika umahiri wa kuigiza na mengineyo basi atumie nafasi hiyo akiwa hai, haitaji kusifiwa akifariki kwani anaamini kuwa sifa hizo hatasikia.



 “Nasema mapema kabisa sitaki kusifiwa nikifa, sifa mtu uipate ukiwa hai kama ni faida au kufurahia mwenyewe ujionee lakini nimeshafumba macho kuna faida gani, sisikii sioni haya ya nini kwangu miye?,”anasema Riyama.



Msanii huyo amesema kuwa imekuwa tabia kwa baadhi ya wasanii kuleta maigizo katika misiba ya wasanii inapotokea mara nyingi waonapo televisheni ujipanga kwa ajili ya kuhojiwa na waandishi basi hata kama marehemu alikuwa na ugomvi naye basi atajifanya jana kabla ya umauti walikuwa wote na kumwachia usia kama rafiki.
 
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....
 
 

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment