Facebook

Thursday, 5 June 2014

Ujerumani kuchunguza madai ya udaku uliofanywa na raia mmoja wa Marekani

Obama amesema amesikitishwa na kudorora kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili
Ujerumani inachunguza madai yaliyotolewa na mtoro mmarekani, Edward Snowden kuwa Marekani ilifanyia uchunguzi simu ya Chansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Mwendesha mkuu wa mashitaka wa Ujerumani,Harald Range, alifahamisha kamati ya kisheria ya bunge la ujerumani kuwa uchunguzi utafanywa dhidi ya watu ambao hawakutajwa.
Bi Merkel ametaka ufafanuzi kuhusu madai hayo ambayo yanahusisha shirika la ujasusi la Marekani (NSA).
Jopo litakaloendesha uchunguzi huo, ilitangazwa wakati wa ziara ya Rais Obama barani Ulaya.
Wakati huohuo, Bwana Range amesema kuwa aliamua kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya shirika la NSA kupeleleza wananchi wa Ujerumani.
'Machungu'
Viongozi wa Ujeruami na Marekani, wanatarajiwa kukutana mjini Brussels katika mkutano wa G7.
Rais Obama alimwambia Merkel mwezi jana kuwa alihisi uchungu mwingi kwamba ufichuzi wa Snowden umeathiri pakubwa uhusiano kati ya mataifa hayo.
Rais Obama amesema kuwa amewaamuru maafisa wake wa ujasusi kuchunguza uzito wa udukuzi dhidi ya raia wa Marekani na kuzingiatia swala la usiri wa maisha yao.
Merkel amependekeza kuanzisha mtandao wa mawasiliano wa Ulaya kuzuia ujumbe wa faragha wa maafisa ulaya kufikiwa na Marekani.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

Related Posts:

  • Obama aomba pesa awasaidie waasi Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi w… Read More
  • Mkereketwa apigwa risasi na kuuawa Libya Mzee akisaidiwa kupiga kura nchini Libya katika uchaguzi uliodhaniwa ungeimarisha usalama. Wakili mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu nchini Libya ameuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulika… Read More
  • Magaidi wajifaidisha na uwindaji haramu moja wa Ndovu waliouawa na wawindaji haramu nchini Kenya Makundi ya kigaidi na wanamgambo wamekuwa wakifaidi kutokana na uwindaji haramu wenye thamani ya dola bilioni 213 kila mwaka, na kutishia usalama wa kimataifa… Read More
  • Kenyatta aongoza kwa umaarufu utumiaji wa Twitter Afrika Rais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika. Kenyatta amempiku Rais wa Rwan… Read More
  • Gavana akabiliwa na kesi ya mauaji Kenya Timamy alikamatwa Jumatano na kufikishwa mahakamani Alhamisi Gavana wa kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mauaji ya zaidi ya watu sitini katika eneo la mpeketoni. Issa Timamy hata… Read More

0 comments:

Post a Comment