Facebook

Tuesday, 10 June 2014

‘Umri wa kuishi wa Watanzania umepanda’

Rais Dkt. Jakaya akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu Dkt. Albina Chuwa katika uzinduzi wa chapisho la tatu la  Sensa ya idadi ya watu na  Makazi.
Rais Dkt. Jakaya akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu Dkt. Albina Chuwa katika uzinduzi wa chapisho la tatu la Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi.
Imeelezwa kuwa umri wa kuishi kwa Mtanzania umepanda kutoka miaka 50 mwaka 1988 hadi kufikia miaka 61 kwa mujibu wa sensa ya maendeleo ya watu na makazi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu Dkt. Albina Chuwa katika uzinduzi wa chapisho la tatu la sensa ya maendeleo ya watu na makazi, ongezeko hilo linakwenda sambamba na kuimarika kwa huduma za afya hapa nchini.
Dkt. Chuwa alisema kuwa kila kaya ilipata fursa ya kwenda katika vituo vya afya kupatiwa huduma na kupunguza magonjwa ambayo yalikuwa tishio kwa watanzania na kusababisha umri wa kuishi kuwa chini  kwa miaka michache.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa chapisho la tatu la Sensa ya Maendeleo ya Watu na Makazi.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa chapisho la tatu la Sensa ya Maendeleo ya Watu na Makazi.
Kwa upande wake Rais Dkt Jakaya Kikwete alisema kuwa, taarifa hiyo ni muhimu sana kwa watendaji mbalimbali katika taasisi za umma na serikali pamoja na sekta binafsi kuifanyiakazi, ili kuweza kuleta maendeleo kwa watanzania ambao kwa sasa idadi ya ongezeko la watu linazidi siku hadi siku na kwa sasa kuna watanzania milioni 48.
Idadi hii ni kubwa sana ukilinganisha na ukuaji na upanuaji wa huduma za jamii kama maji, umeme, barabara pamoja na huduma za afya, tusipotumia takwimu hizi kwa umakini hali ya watanzania itakuwa inazidi kuwa ngumu siku hadi siku, kwa sababu ya ongezeko la watu haliendani na uhalisia wa huduma za kijamii.
Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt. Jakaya Kikwete.
Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt. Jakaya Kikwete.

Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment