Facebook

Friday, 20 June 2014

Wanaharakati 8 washtakiwa Mombasa, Kenya

Mombasa ni moja ya miji ambayo imeshuhudia utovu mkubwa wa usalama
Wanaharakati wanane wamefunguliwa mashitaka mjini Mombasa Pwani ya Kenya wakituhumiwa kwa kuhusika na maandamano haramu.
Awali wanaharakati hao walikamatwa wakati wa maandamano yao kupinga kile walichosema ni serikali kukosa na kushindwa kudhibiti usamala nchini Kenya.
Gari la mmoja wa wanaharakati hao pia lilikamatwa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na maafisa wa shirika la kitaifa la kutetea haki za binadamu tawi la Mombasa.
Wanaharakati hao walifikishwa mahakamani na kusihitakiwa ingawa baadaye waliachiliwa kwa dhamana.
Baadhi yao walivamia kituo cha polisi wakiwataka wenzao kuachiliwa
Wanaharakati hao wamekosoa polisi kwa kuzuia maandamano yao ambayo wanasema ni haki yao ya kikatiba.
Wanawalumu kwa kuyaingilia ili kuwatawanya wakitumia gesi ya kutoa machozi.
Kenya imekuwa ikikumbwa na hali mbaya ya usalama pakishuhudiwa mashambulizio ya kigaidi kama yaliyotokea Jumapili usiku ambapo watu zaidi ya sitini waliuawa.

Related Posts:

  • Kutana na kisa hiki cha kahaba wazee wa Korea Kusini Wazee katika baadhi ya nchi huheshimika na kuwa akiba ya busara kwa kizazi cha vijana na zaidi ya yote huangaliwa na kusaidiwa kimaisha. Huko nchini Korea Kusini maisha kwa wazee ambao walichangia katika uchumi wa t… Read More
  • Wadau wakutana kupinga ubakaji vitani Angelina Jolie ni mmoja wa wanaharakati maarufu wanaopinga dhuluma za kingono ikiwemo ubakaji Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kwa wiki nzi… Read More
  • Kiongozi ataka vijana wajihami Nigeria Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mingi Kiongozi mmoja wa kijamii katika mji wa Chibok Nchini Nigeria ameiomba serikali ya taifa hilo kuwaruhusu kubuni makundi ya vijana waliojiham… Read More
  • Mashoga wapinga Urais wa Kutesa UN Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa. Uwezekano wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa, kushinda cheo cha Urais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kumeanzisha mjadala mkali nchini Uganda,… Read More
  • Majeshi ya DRC na Rwanda yakabiliana Majeshi ya DRC yakabili wanajeshi wa Rwanda mashariki mwa Congo Maafisa wakuu katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo wanasema kuwa makabiliano makali ya… Read More

0 comments:

Post a Comment