Maneno ya mganga wa kienyeji wa Ghana, Nana Kwaku Bonsam, yameanza
kudhihirika baada ya uongozi wa timu ya taifa ya Ureno kuthibitisha
taarifa za mshambuliaji Cristiano Ronaldo, kutokuwa sehemu ya kikosi cha
timu ya taifa ya Ureno ambacho juzi kilicheza mchezo wa kimataifa wa
kirafiki dhidi ya Mexico.
Nana Kwaku Bonsam, amesema yeye ndiye anayemroga nahodha huyo wa timu ya
taifa ya Ureno, ili asicheze mchezo wa kundi la saba katika fainali za
kombe la dunia ambapo timu ya taifa ya Ureno itapambana na timu ya taifa
ya Ghana, Black Stars.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paul Bento alisema pamoja na
kutarajia kumkosa Ronaldo katika mchezo wa juzi wa kirafiki, bado
hajafahamu ni lini mshambuliaji huyo atakuwa fit kwa ajili ya kujiunga
na wenzake.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Real Madrid anasumbuliwa na maumivu ya
mishipa fulani laini katika mguu wake, ambapo kwa mara ya mwisho
alionekana uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya
mabingwa barani Ulaya walipocheza dhidi ya Atletico Madrid.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
SUAREZ ADAIWA KUMNG'ATA MCHEZAJI TENA
Picha za video zimeonesha mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez
akimng'ata beki wa Italy Giorgio Chiellini. Mwamuzi hakuona kitendo
hicho lakini huenda hatua zitachukuliwa baadaye.
…Read More
Suarez apewa adhabu kali na FIFA
STRAIKA
wa Uruguay Luis Suarez amefungiwa Miezi Minne kutoshiriki chochote
kwenye Soka baada ya kupatikana hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy
Giorgio Chiellini.
Straika huyo wa Liverpool pia amefungiwa Mechi 9 za Kimata…Read More
Uholanzi kumenyana na Mexico
Uholanzi kuvaana na Mexico mkondo wa pili
Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Mabao ya Uholanzi yaliyofungwa na Leroy Fern na…Read More
Van Gaal: ''FIFA imetuonea''
Van Gaal akashifu FIFA kwa ratiba mbaya za mkondo wa pili
Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal
amelishutumu shirikisho la soka duniani FIFA kwa "kufanya hila" kwa
jinsi linavyopanga ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia…Read More
0 comments:
Post a Comment