WAZALISHAJI UMEME WAZALENDO
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM, Jumatatu, 18-1-2016: WIZARA ya Nishati na Madini imeandaa mkutano wa wazalishaji umeme wazalendo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar.
"Wizara itatoa ratiba kwa makampuni ya wazalendo kuja kutoa mapendekezo ya miradi yao tarehe 15-17 February 2016", alisema Prof Muhongo.
Prof Muhongo alisema mkutano huo utahusu miradi yote ya uzalishaji umeme kutoka vyanzo mbalimbali nchini.
Taarifa ya Waziri ilisema vikao na wadau hao vitafanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini.
"Iwapo kuna WABIA kutoka nje ya nchi tungalipenda na hao WABIA wawepo kwenye vikao", alisema Waziri.
Tanzania itazalisha umeme wake kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Gesi Asilia (natural gas), Maji - Maporomoko (Hydro), Makaa ya Mawe (coal) na Nishati Jadidifu (Renewable Energies).
Vyanzo vingine ni Jua (solar), Upepo (wind) , Jotoardhi (geothermal) na Mawimbi (tides&waves).
Alikitaja chanzo kingine ambacho mi maarufu kwa wananchi wengi wa kawaida kuwa ni Bio-Energies ambayo ni biogas (gesi ya kinyesi) na biomass (kuni).
Bantuz.Com
0 comments:
Post a Comment