Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari ya mtu mmoja aliyekutwa
amefia kaburini kwamba alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la
kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo
ya kishirikina.
Kwa mujibu wa Saturday Tribune la Nigeria, tukio hilo limetokea katika
mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku
nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na
marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya
kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao
wakiwa salama.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na
kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hili
waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka
kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.
Saturday Tribune iliongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la
Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa
kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilikuwa chanzo cha kifo
chake. Na kwamba polisi hawajathibisha kuwa tukio hilo linatokana na
masuala ya kishirikina
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua matukio mbalimbali yanayotokea duniani
Monday, 19 May 2014
Afia Kaburini Baada ya Kunaswa na Kitu Akijaribu Kufukua ili Aibe Fuvu
Related Posts:
BantuTz MAGAZETINI. Ni utaratibu ambao BantuTz imeuanzisha wa kukuwezesha kupitia kurasa za nyuma na mbele za magazeti mbalimbali nchini. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . … Read More
Hilo ndilo daraja kubwa kutoka Zanzibar hadi Dar Es Salaam.Unaweza ukadhani ni ndoto lakini hii ni habari ya kweli baada ya Hifadhi ya jamii NSSF kutangaza uwezekano wa kujengwa daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es salaam na Zanzibar. Uwepo wa daraja hilo unaweza k… Read More
Basi la Happy Nation lapata ajali mbaya Igurursi-Mbeya Taarifa zilizotufikia Muda huu zinasema kwamba kuna ajali mbaya imetokea katika eneo la Igurusi ,Kikosi kazi cha Mbeya yetu kinaelekea eneo la Tukio muda huu. Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kujua kila… Read More
Ndege ya rais wa China yahusishwa na wizi Pembe za ndovu Tanzania. Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping,wakati alipozuru bara Afri… Read More
Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba Katika mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa. Mdahalo huo uliokuwa ukita… Read More
0 comments:
Post a Comment