Facebook

Wednesday 14 May 2014

Je unaijua faini aliyotozwa yule mmiliki wa ile gari iliyohusika na mlipuko wa Al shabaab.


TZA MUHAMED DUGAL ALI 

Mmiliki wa gari lililo lipuliwa na watuhumiwa wa kundi la Al Shabaab ameachiwa huru baada kutozwa faini ya shilingi milioni 8 za Kenya.
Ahmed Dugal Ali ameshtakiwa kwa kosa la kuchangia kutekelezwa kwa ugaidi huo kwa kutoa gari lake lililo lipuka na kuwaua maafisa wawili wa polisi katika kituo cha pangani Nairobi Aprili 23.
Mbali na kosa hilo pia amekutwa na kosa lingine la kumpa hifadhi mmoja wa washukiwa Mohamed Abass Hassan aliyefariki wakati wa mlipuko.

Upande wa mashtaka umedai kwamba bwana Dugal Ali alimpatia hifadhi mtu aliye faham vizuri kwamba alikua Gaidi katika eneo la Nyayo Estate jijini Nairobi kati ya mwezi machi na Aprili 23.
Mtuhumiwa huyo pia alikua anahitajika kulipa shilingi milioni 10 kabla ya kuachiliwa akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake Julai 1,wanaume wengine wawili waliokamatwa ni pamoja na Abdiaziz Bulle Ali na Mohammed Abdukkahi Falir.
Kwa pamoja na Dugal wamaeachiliwa huru baada ya kitengo cha polisi cha ATPU kusema hawana ushahidi wowote dhidi yao na wanaweza kufika mbele koti kutoa ushahidi.

Upande wa mashtaka ulisema kwamba koti inauhuru wa kuamua kuhusiana na  swala la kumuachia mtuhumiwa kwa bondi.
Wakili wa mtuhumiwa  Mbugua Mureithi aliiambia mahakama kwamba bwana Dugal alijisalimisha kwa polisi baada ya kugundua kwamba gari lake lilikua limehusika kutekeleza mashambulizi.
Wiki mbili zilizo pita polisi waliomba nafasi ya kufanya uchunguzi zaidi,mmoja wa maafisa wanaoendesha uchunguzi alikula akiapo na kuwasilisha ushahidi unao mhusisha Dugal na kundi la Alshabaab akisema kua mmoja wawalio kufa wakati wa mlipuko anauhusiano wa karibu naye.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua  matukio mbalimbali yanayotokea duniani

0 comments:

Post a Comment