
Staa wa muziki wa Kenya anaetajwa kuingia kwenye TOP 5 ya Wasanii matajiri wa muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki huku orodha hiyo ikiwa na watu wengine kama Jose Chameleone.
Imefahamika kwamba Jaguar alikataa kuja kwenye tuzo za Kili 2014 alizokua nominated baada ya waandaaji kushindwa kufikia masharti aliyowapa na badala yake akaamua kwenda kuhudhuria harusi ya producer wa DNA aitwae Refigah.
Jaguar alitaka atumiwe ticket ya ndege ya business class, alitaka achukuliwe chumba kwenye hoteli ya nyota tano, apewe ulinzi popote atakapokwenda na vilevile apewe gari zuri la kifahari la kutembelea.
Kwenye sharti jingine Jaguar alitoa option kwa waandaaji na kuwaambia kama wangeshindwa kumpa ticket ya ndege basi walipaswa kuweka mafuta ili aje na ndege yake ndogo anayomiliki.

Chameleone, Wyre, Amani, Ay, Mtangazaji William Tuva, shabiki Daudi wa Kota na Dj wa Chameleone juzi Dar es salaam.
Tuzo za KILI 2014 zilihudhuriwa na mastaa wawili wa Kenya ambao ni Wyre na Amani huku Uganda ikiwakilishwa na Jose Chameleone ambae ndio alitangazwa mshindi kwenye kipengele cha Afrika Mashariki.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kwa muda muafaka.....
0 comments:
Post a Comment