MBUNGE wa Ileje, Aliko Kibona (CCM) ameomba Serikali ieleze juu ya ndege
kutoka Malawi, ambayo imekuwa ikitia hofu wananchi wa Ileje, kwa
kuzunguka angani kila mara.
Mbunge huyo alisimama kutoa hoja hiyo baada ya kipindi cha maswali na
majibu na kuomba mwongozo wa Spika, Anne Makinda kuhusu suala hilo.
Kibona alisema:
“Nazungumzia jambo mahsusi linalotokea katika mpaka wa Tanzania na
Malawi katika Jimbo la Ileje. Kwa sasa kuna ndege kutoka nchi ya Malawi
inazunguka katika vijiji jirani na tayari imeleta hofu kwa wananchi; na
watoto hawawezi kusoma. Ninaomba mwongozo wako kama nipo sahihi. Naitaka
Serikali kwanza ieleze ile ndege inatoka wapi na inafanya nini; na Pili
naitaka Serikali imfahamishe Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhusu ndege hiyo
ili naye awafahamishe wananchi ili wasiwe na hofu”.
Mbunge huyo alisema aliamua kuleta hoja hiyo bungeni, kwa kuzingatia
uhusiano uliopo hivi sasa baina ya Tanzania na Malawi. Baada ya maelezo
hayo ya Kibona, Spika alisema:
“Suala la Mheshimiwa Kibona linahitaji kufanyiwa kazi sana”. Serikali
inaendelea na vikao vyake na itampatia majibu Kibona baada ya kutafakari
na kujadili suala hilo.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment