Facebook

Monday, 24 November 2014

UKWELI KUHUSIANA NA MAJINA YANAYOTUMIKA KATIKA MASAKATA MBALIMBALI YA UFISADI.

Leo rafiki yangu Charles Wanga kanifurahisha alipohoji kwanini tunaibiwa kwa majina ya kizungu tu? Mara RICHMOND, EPA, DOWANS, na sasa ESCROW. Hii ESCROW ni neno la kiingereza lenye maana ya DHAMANA. 

Na akaunti hii ilifunguliwa BOT kama akaunti ya dhamana ya TANESCO dhidi ya madai ya IPTL. Sasa kwanini akaunti hii haikuitwa DHAMANA?? Labda walihisi tungeshtuka mapema.. maana inadaiwa eti ili kumuibia mtanzania weka kitu kwa kiingereza.. hahahaah.!

Anyway, tukiacha hilo la lugha sasa twende kwenye hesabu; wataalamu wanaiita hisabati. Kiasi kinachodaiwa kuibiwa kwny akaunti hiyo ya DHAMANA ambayo "wasomi" wanaiita ESCROW ni takribani shilingi bilioni 400.

Pesa hizi ikiwa zitawekwa katika noti ya shilingi elfu kumi kumi tutapata noti milioni 40.

Kila noti moja ya elfu kumi ina urefu wa sentimita 14 hivyo tukizidisha noti zetu 40,000,000 mara 14 tutapata urefu wa sentimita 560,000,000.

Kilomita moja ni sawa na sentimita 100,000. Hivyo tukigawanya 560,000,000 kwa 100,000 utapata kilomita 5,600.

Hivyo basi pesa hizi za ESCROW zikitandazwa njiani kwa noti za elfu kumi kumi zitaenea umbali wa kilomita 5,600.

Umbali wa kutoka Songea hadi Chalinze kwa kupitia Mtwara ni kilomita 1,160. Na kutoka Chalinze hadi Arusha ni kilomita 536.. Na kutoka Arusha hadi Mwanza ni kilomita 619. Jumla ya Umbali wa kutoka Songea hadi Mwanza kwa kupitia mikoa niliyotaja ni kilomita 2,315.

Hivyo basi pesa za ESCROW zinawez kutandazwa kwa noti za elfu kumi kumi kutoka Songea hadi Mwanza kwa kupitia Mtwara, Lindi, Pwani, Dar, Tanga, Moshi, Arusha, Singida, Tabora, Shinyanga hadi Mwanza mara mbili na zikabaki milioni 970.

Naposema mara mbili namaanisha utandaze noti za elfu kumi kutoka Songea hadi Mwanza, halafu tena kutoka Mwanza hadi Songea kisha ubakiwe na Milioni 970.

Nadhani kwa mfano huu Mtanzania wa kawaida anaweza kuelewa ni pesa nyingi kiasi gani; japo nasikia kuna wanasiasa wanaziponda na kudai ni pesa za vikao vya harusi. Mimi nasema ziwe za vikao vya harusi au za send off tunataka pesa zetu. Please#BRING_BACK_OUR_MONEY .

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!

0 comments:

Post a Comment