Facebook

Sunday, 8 June 2014

Mganga Mghana adai amemroga Cristiano Ronaldo awe majeruhi asicheze kombe la Dunia

Mbwembwe na matukio ya kushangaza yanazidi kuonekana kati ya nchi zinazopeleka timu zao Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia.

Mganga wa kienyeji wa Ghana anaejulikana kwa jina la Nana Kwaku Bonsam amewatoa wasiwasi raia wan chi hiyo wanaomhofia Cristiano Ronaldo katika mchezo kati ya Ghana na Ureno utakaofanyika June 26. 


Mganga huyo aliyewahi kutabiri mwezi February kuwa Ronaldo angezikosa fainali za Kombe la Dunia ameweka wazi kuwa yeye ndiye anaemroga mchezaji huyo ambaye Jumatano hii alitangazwa kuwa majeruhi anaesumbuliwa na goti. 


Nana Kwaku ambaye maana ya jina lake ni ‘Shetani wa Jumatano’ amesisitiza kuwa hakuna dawa yoyote itakayoweza kumponya mchezaji huyo hadi kombe la dunia litakapokwisha.


“Ninafahamu sababu ya majeraha ya Cristiano Ronaldo, ninamfanyia kazi. Niko serious kuhusu hilo. Wiki iliyopita, nilizunguka nikitafuta mbwa wane na niliwapata, watatumika kutengeneza mzimu maalum unaitwa ‘Kahwir Kapam.” Alisema Mganga huyo kwenye maelezo yake. 


Balaa! Taarifa hii itapokelewaje na wananchi wa Ghana? Je, watampa sapoti wakimuombea adui yao njaa ili asiwe kikwazo kwao? Vipi Wareno watachukua hatua gani au watazipuuzia habari za mganga huyo wa kienyeji?




Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment