Facebook

Sunday, 8 June 2014

Viongozi wa Muslim Brotherhood kunyongwa Misri.


Wanachama wa kundi la Muslim Brotherhood wakiwa kizuizini.
Mahakama moja nchini Misri imewahukumu vifo viongozi kumi wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood kwa kuchochea ghasia zilizosababisha vifo vya watu wawili mwezi July.
Washtakiwa wengine 38 akiwemo kiongozi wa kundi hilo Mohammed Badie watapewa hukumu yao ifikiapo mwezi ujao.
Raia hao walipatikana na hatia ya kuchochea uma na kuzuia msafara wa magari katika mji wa Qalyub kazkazini mwa mji wa Cairo.
Wamekuwa wakishiriki katika maandamano dhidi ya jeshi ambalo lilimpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Bwana Badie tayari amehukumiwa kunyongwa katika kesi nyengine.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....


Related Posts:

0 comments:

Post a Comment