Facebook

Monday, 2 June 2014

Mmiliki mbaguzi Donald Sterling akataa timu yake kununuliwa kwa Bilioni 2



Mmiliki Mbaguzi Donald Sterling Apinga Timu Yake Kununuliwa Kwa Bilioni 2
Baada ya aliyekuwa mkurugenzi wa Microsoft Steve Ballmer  kusema amefikia makubaliano na timu ya mpira wa kikapu ya Las Angeles Clippers ya kuinunua timu hiyo kwa dola bilioni mbili, mmiliki wa sasa wa timu hiyo Donald Sterling amepinga kwa nguvu zote timu hiyo kununuliwa kwa bilioni 2.

 Fahamu Donald alitoka kama kiongozi wa timu hio baada ya kutoa matamshi ya kibaguzo kwa watu weusi ambao asilimia kubwa ndio wachezaji na mashabiki wa mpira wa kikapu Marekani.
Matamshi ya Donald yalihofiwa kuhatarisha biashara na pesa nyingi zinazotokana na mchezo huo.

Mpaka sasa Sterling ametozwa faini ya dola milioni 2 na kupigwa marufuku kujihusisha na mchezo wa kikapu.
Ballmer amewapiku matajiri wengine waliotaka kununua timu hio wakiwemo David Geffen na Oprah Winfrey. Ballmer alikuwa mkurugenzi wa Microsoft na baada ya kumaliza muda wake amebaki na pesa nyingi na hisa kwenye kampuni hio zenye thamani ya dola bilioni 13.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kutoka kila pande za dunia.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment