Mtoto mchanga, amekutwa ametupwa pembezoni mwa barabara ya Kawe-Beach,
huku puani na mdomoni akiwa amefungwa plasta, iliyosababisha kukosa
pumzi na kufariki.
Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina
lake wala kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali
juu kwa kumuua huyo mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara
hiyo.
Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo
iliwashtua na kuamua kusogea karibu, ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye
jinsi ya kike, akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na
puani.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment