Habari wakuu,
Leo tunamaliza ngwe yetu ya mwisho bungeni, baada ya wasilisho la ripoti ya PAC, majibu ya serikali na mjadala wa wabunge wa jana, moja kwa moja kutoka Dodoma tuwe pamoja kuimaliza ngwe yetu. TANESCO wameshatoa tangazo rasmi la matatizo ya umeme hivyo chaji zetu ziwe vizuri nafasi ya kupata umeme inapopatikana.
=============
SAA 3:00 ASUBUHI.
Spika ana Makinda ndiye aliekalia kiti leo na Mwanri anajibu maswali yanayohusu wizara ya afya.
MangungoNyongeza: Eneo la Mlandizi ni eneo la barabara kuu, nini ahadi serikali kuharakisha upatikanaji wa kituo ili kuwapelekea wananchi huduma karibu? Lipo tatizo la wahudumu wa afya na madaktari japo majengo yapo, nini jitihada ya serikali?
Mwanri: Nakubaliana eneo la barabarani ajali nyingi, tutajitahidi kukamilisha haraka na kuona inafanyiwa kazi. Kuna vibali vimetoka kwa wahudumu wa afya pia wizara pia inapeleka watumishi moja kwa moja.
Tuliwapa nafasi cha watumishi 8,000 wizara ya afya pia tumewapa kibali cha watumishi 1,000 na bado hakijamaliza.
Suzan Lymo: Maslahi ya walimu lazima yaboreshe, serikali inafahamu tatizo
Mwanri: Nakubaliana lazima kuboresha maslahi ya walimu, tuna upungufu wa walimu na nyumba za walimu. Mkakati wa serikali na pamoja na kudahili walimu na maabara, nyumba za walimu na kuimarisha mfumo wa kuwahudumia walimu.
3:25 ASUBUHI
Suzan Lymo: Kuna tatizo la upangaji walimu kwa shule za pembezoni, pia watendaji wanakaimisha walimu majukumu badala ya kukaa kwenye vituo vyao vya shule
Mwanri: Kwanza kweli kuna tatizo, lakini tatizo kwa walimu wa sanaa limpembukua sana, tutafanya upangaji(re-allocation). Mwalimu kazi yake ni kufundisha hivyo kuwapa kazi za watendaji haikubaliki.
Leizer: Ni lini serikali itachukua mkakati kwa nyumba za walimu kama walivyofanya maabara!
Mwanri: Jitihada za maabara tunazipongeza halmashauri, kuna halmashauri tumewapelekea milioni 500 kila moja ambazo zipo katika mazingira magumu.
SAA 3:45 ASUBUHI.
Maswali sasa ni kwa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo maswali yanajibiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe Stephen Masele.
Mhe Mbilinyi: Tunazaungumzia sana mafanikio ya kusambaza umeme, kuna umuhimu gani wa kuendelea kusambaza umeme wakati huwa unakatwa kwenye nyakati maalum. Mfano; Jana kwenye mjadala wa umeme?
Jibu: Tutofautishe kati ya kuwapatia umeme wananchi na kupatikana umeme wakati wote. Jana kulikuwa na hitilafu ndogo tu, ila Leo mbona umeme upo.
Komba: Katika Maeneo ya Mbamba bay, kwanini umeme mpaka sasa haujafika kama ilivyoahidiwa?
Jibu: Kuna Matatizo ya nguzo, kutokana na demand kuwa kubwa sana wakandarasi wameagiza nguzo za kutosha ili kuhakikisha miradi yote inakamilika.
SAA 4:00 ASUBUHI.
Maswali kwa wizara hii bado yanaendelea....
============================== =========
Sasa ni zamu ya maswali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi.
Swali: Ni lini serikali itaboresha magereza kwa kuwa yapo kwenye hali mbaya kwa uchakavu, pamoja na miundombinu yake mibovu?
Jibu (Naibu waziri) : Serikali kupitia wizara yangu, ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hiyo.
SAA 4:05 ASUBUHI
Swali: Hivi karibuni, nchi jirani ya Kenya tukio la westgate lilitishia usalama wa nchi na raia wake, Je serikali imejipanga vipi kuzuia tukio kama lile lisiikumbe Tanzania?
Jibu: Tukio la Westgate la Kenya, lilikuwa ni tukio la kupangwa kwa masuala ya ugaidi. Serikali ya Tanzania kupitia jeshi la polisi, linajitahidi kwa makusudi kukusanya taarifa za kiintelijensia na kuimarisha ulinzi.
SAA 4:20
==================
Maswali kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia
Swali: Ni kiasi gani makampuni ya simu za mikononi zimelipa Kodi kwa Mwaka uliopita?
Jibu: Makampuni ya simu hulipa kodi kwa utaratibu uliowekwa. Aina za kodi ni pamoja na VAT, Service, Corporate TAX na nyinginezo.
Swali Nyongeza: Hivi karibuni serikali imeweka mtambo wa kudhibiti simu zinazoingia na kutoka nchini. Je, imeongeza vipi kodi (pato)?
Jibu: Ni kweli serikali imeweka mtambo wa mawasiliano pale TCRA, Mtambo huo una kazi zake mbali mbali. Lakini kwa sasa serikali imefikiria namna ya kupata solution ya kuangalia namna gani itakagua mobile money transfer ili kuweza kutoza kodi.
Swali nyongeza (Zungu): Mheshimiwa waziri hujatoa majibu ya kitaalamu, kwani mtambo huo bado kabisa haujaanza kufanya kazi kama inavyotakiwa kufanya. Sasa nauliza, ni lini software hii ya kutoza wafanya biashara hasa wa mitandao ya simu italetwa na kuanza kufanya kazi ili mwananchi ajue kodi yake inaenda serikalini moja kwa moja?
Jibu: Kwa sasa mtambo unafanya kazi ya kukagua simu zinazoingia na kutoka, za kihalifu pamoja na kukagua mawasiliano kwa ujumla. ILa Tunaamini mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu kazi hiyo itakuwa imekamilika.
0 comments:
Post a Comment