Beki wa Porto Eliaquim Mangala anayesakwa sana na Manchester City
angependa zaidi kujiunga na Manchester United, ingawa Louis van Gaal ana
mashaka naye kutokana na hasira zake (Guardian),
Chelsea wanatazamia
kukamilisha usajili wa wachezaji watatu,
Luis Filipe, Tiago na Diego Costa kwa jumla ya pauni milioni 50 (Daily
Mirror),
Jose Mourinho amethibitisha kumtaka Cesc Fabregas (Times),
Real
Madrid watalazimika kutoa karibu pauni milioni 80 kama walivyotoa
kumnunua Gareth Bale, ikiwa wanataka kumsajili Luis Suarez kutoka
Liverpool (Marca),
Liverpool wamekubaliana na Sevilla kumsajili beki
Alberto Moreno kwa pauni milioni 17 (Daily Mirror),
Inter Milan
wanafanya mazungumzo na Manchester United kuhusiana na usajili wa Javier
Hernandez Chicharito (Daily Express),
Paris St-Germain wapo tayari
kumuuza beki wa kati Marquinhos, ambaye Man City wanamtaka (Talksport),
Arsenal wapo tayari kutoa pauni milioni 17 kumsajili mshambuliaji wa
Napoli na Italy, Lorenzo Insigne, ikiwa atawika katika Kombe la Dunia
(Metro),
Chelsea wanamfuatilia winga kutoka Mexico Jurgen Damm (Daily
Star),
Tottenham wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 5 kumsajili
winga wa Bayern Munich Julian Green (Metro),
Mshambuliaji wa Barcelona,
Pedro inadaiwa anasakwa na Man United, na amekiri kuwa hana uhakika na
hatma yake Barca (Mundodeportivo),
Chelsea wamempa mkataba mpya na mnono
wa pauni LAKI MBILI kwa wiki, Edin Hazard ili kumzuia asisajiliwe na
Paris ST-Germain (Daily Express),
Chelsea wametoa dau la pauni milioni
27 kumsajili Cesc Fabregas (Daily Express),
Arsene Wenger anatumanini
kukamilisha mkataba na Real Madrid kumsajili kipa wa Real Madrid Iker
Casillas baada ya Kombe la Dunia (AS).
SHARE TETESI HIZI NA WAPENZI WOTE
WA SOKA.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment