Facebook

Wednesday, 4 June 2014

Umeisikia hii kuhusiana na Wanariadha wanaokunywa maziwa ya Matiti !!


Akina mama wakiwanyonyesha Matiti watoto wao
Wanariadha wanaume wamekiri kuanza kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kusisimua misuli yao badala ya kutumia madawa yaliyoharamishwa ambayo yanaongeza nguvu mwili.
Kwa mujibu wa jarida la Mail kwenye mtandao , wanyanyua uzani wengi wameanza kutumia maziwa ya matiti kama njia ya kujipatia nguvu.
Mwanariadha mmoja kutoka mjini New York kwa jina Antony, aliambia jarida la NYMag.com kwamba hukutana na wanariadha kadhaa ambao hunywa maziwa hayo ambayo wanasema ni mazuri na yanawapa nguvu.
Maziwa haya hununuliwa kwenye maduka ya mitandaoni ikiwemo mtandao ujulikanao kama 'Only the Breast and Human Milk 4 Human Babies' kwa dola mbini na nusu.
Baadhi ya wanaume wanasema maziwa ya Matiti inawapa nguvu za ajabu
Mwanariadha huyo anasema kuwa maziwa hayo humpa nguvu za ajabu.
Sababu ya wao kufanya hivyo , ni kujizuia kutumia madawa ambayo yamepigwa marufuku kwani wanaamini kuwa maziwa ya Matiti ni njia ya kiasili ya kuwapa nguvu.
Mwanariadha mmoja ambaye ni baba wa watoto wanne Jason Nash, anasema alianza kunywa maziwa ya mkewe baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa na akahisi kuwa ikiwa maziwa hayo ni mazuri kwa mtoto basi pia ni mazuri kwa watu wazima.
Ananukuliwa akisema kuwa maziwa hayo yamemlinda kutokana na magonjwa miaka hii yote.
Wanaume kadhaa wamezungumzia kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kuwapa nguvu badala ya kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Wanaume ambao sio wanariadha wanasema maziwa ya Matiti yanawapa afya nzuri
Akijibu wakosoaji wake, wanaosema kuwa ni kitu cha ajabu na kushangaza, Antony alisema,'' mimi siamini madawa ya kusisimua misuli na ninataka vitu vya asili, ambavyo havina athari zozote mbaya kwa mwili.''
Wanaume wengine ambao sio wanaridaha ingawa wanakunywa maziwa ya Matit, wanasema kuwa maziwa hayo huwafanya kujisikia kama walio na nguvu mno na wenye afya tele.
David,mwenye umri wa miaka 42, kutoka Brooklyn, aliambia jarida hilo kuwa alianza kunywa maziwa ya matiti miaka mitatu iliyopita. Alisema ilisabidia sana wakati alipokuwa anapokea matibabu ya Saratani kwa kuwa alikuwa anahisi kutapika wakati wote alipokuwa anapokea matibabu.
Pindi alipokunywa maziwa hayo hisia za kutapika wakati wote zilimtoka
Alisema maziwa hayo ambayo ni matamu , yalimsaidia sana.

 Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

Related Posts:

  • Watu 10 wauawa katika mlipuko Nigeria   Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa na mlipuko wa bomu karibu na mashine ya kutoa pesa ya ATM. Walioshuhdia walisema kuwa ,mwanamume mmoja alikaribia watu waliokuwa wamepanga fol… Read More
  • Je,wajua kuna waombolezaji wa kulipwa ?   Kila Alhamisi na Ijumaa, shughuli katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, huvurugika kwa sababu mamia ya waendesha pikipiki huzuia barabara kutokana na kukodiwa kuomboleza msiba kwa malipo. Kelele za saut… Read More
  • wanafunzi 23 wauawa shuleni Nigeria.   Kumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Hata hivyo hakuna taarifa kamili kuhusu idadi ya majeruhi kufikia sa… Read More
  • Raisi Uhuru Kenyata apanda daladala kutoka Ikulu mpaka KICC Raisi wa nne wa Kenya Uhuru Kenyata amewaacha watu na surprise nyingine siku ya jana (jumatano) asubuhi baada ya kuamua kupanda matatu kuelekea KICC kwenye uzinduzi rasmi wa My 1964. CEO wa… Read More
  • Rais masikini zaidi duniani apewa dola milioni 1Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen. Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake ,alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kion… Read More

0 comments:

Post a Comment