Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga (Chadema), amewaumbua
wabunge wenzake kuwa wanapeana na kuchukua rushwa ndani ya Bunge.
Suzan aliyasema hayo juzi jioni wakati akichangia katika mkutano wa
Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC). Suzan
alisema vitendo hivyo vya rushwa vilionekana wakati wabunge hao
walipokuwa wakiwachagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
“Rushwa ilikuwa ni wazi wazi ukienda chooni unapewa laki mbili (Sh200,000) unaondoka,”alisema Suzan.
Alisema wao kama viongozi ambao wanatunga sheria na wanatakiwa
kuisimamia serikali wanapaswa kuwa waadilifu. Hata hivyo, Mbunge wa
Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), alisema hakuna ukweli kuhusu jambo
hilo la baadhi ya wabunge kuchukua rushwa hadi chooni.
Hata hivyo, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura (CCM), alimuunga mkono
Suzan na kusema suala hilo ni la kweli na kwamba kama Sanga hakuliona
walikuwa wanamkimbia.
“Alichokizungumza Suzan ni cha kweli. Kaka yangu (Sanga) walikuwa wanakukimbia. Ni kweli hilo lilifanyika,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa APNAC, Vita Kawawa, alisema si vyema wabunge
wenye taarifa kuhusiana na masuala ya rushwa wakatoa taarifa katika
ofisi za Spika na kamati ya maadili ili liweze kufanyiwa kazi mara moja.
“Ni vyema mkatupa taarifa kitu ambacho kinaashiria rushwa sisi tupo, ofisi ya spika ipo na kamati yetu ya maadili,”alisema.
Alisema rushwa ni mdudu ambao unatakiwa kukataliwa na kila mtu. Alisema
rushwa imesababisha maisha ya wananchi kutobadilika ingawa uchumi wa
nchi unakuwa.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment