Poliso Mkoa wa Temeke, imewakamata vijana wawili wanaodaiwa kujifanya
waganga wanaotoa tiba kwa wanawake, ambayo masharti yake ni kushiriki
nao ngono bila kinga na kuacha nguo za ndani, ili zifanyiwe dawa zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alidai vijana hao Juma Hemedi
(32) na Abrahman Mulsin, wote wakazi wa Tandika, baada ya kushiriki
ngono na wagonjwa wao huwaambia waache nguo za ndani.
Kamanda Kiondo alidai baada ya kupata malalamiko, Jeshi la Polisi
lianzisha msako na kuwapekua waganga hao, ambapo walikutwa na nguo za
ndani za kike 22, ambazo alisema zitakuwa ushahidi wa kuingiliwa kimwili
kwa wanawake hao. Vitu vingine wanavyodaiwa kukutwa navyo ni pembe,
tunguli, makopo ya dawa na vibuyu.
“Sheria iko wazi, inasema mganga anapofanya ngono kama uganga anakuwa
amebaka, na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu 130 sura ya
16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” alisema Kamanda Kiondo.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kiondo, vijana hao wamekuwa wakijifanya
waganga wa tiba asili, husambaza vipeperushi sehemu mbalimbali za jiji
kutafuta wateja.
Mbali na tiba hiyo ya kupata watoto, inayotolewa kwa kushiriki ngono na
mganga, Kamanda Kiondo alidai watuhumiwa hao wamekuwa wakidai kutibu
magonjwa mengine kama kisukari, vidonda vya tumbo, nguvu za kiume,
kukuza maumbile, kupata kazi, kufaulu mtihani, mvuto wa biashara,
kumilikishwa jini na kupewa pete ya bahati.
Katika tukio lingine, Polisi inamshikilia kijana mwingine mkazi wa
Tandika Devis Corner, Maalim Kimti Rita au kwa jina lingine, Joseph Rita
anayedaiwa kutapeli Sh milioni 11 akijidai kumfanyia dua mfanyabiashara
aweze kukuza biashara yake.
Alidai kuna mfanyabiashara mwanamke ambaye alitoa Sh milioni 11 kwa
Maalim Rita, akidanganywa kuwa atafanyiwa uganga ili afanikiwe katika
biashara yake, lakini alipoona hakuna alichopata, akaamua kutoa taarifa
Polisi.
Kamanda Kiondo alisema jamii inapaswa kuelimishwa kuachana na mambo
hayo, kwa sababu tiba yake haipo kwa waganga wa jadi na kwamba hakuna
uhusiano kati ya kufaulu na kwenda kwa waganga isipokuwa bidii ya kazi.
“Watu wengi wamelalamikia matukio ya namna hiyo, sasa tumeamua kuweka
wazi kwa umma kwa kuwa watu wanateketea kwa kukosa elimu… watu wanauza
nyumba magari na mali zao, kwa ajili ya kupata fedha za kupeleka kwa
waganga wakiamini kuna tiba, huu ni utapeli vijana kama hawa hawawezi
kukupa utajiri wala mtoto,” alisema Kamanda Kiondo.
Alisema waganga hao wamepata vyeti vya kufanyia kazi hiyo ya uganga wa
jadi, lakini wanachofanya ni kinyume na kazi hiyo ambapo aliahidi vyeti
vyao kuchunguzwa, kuona wamevipataje na kuwasiliana na Wizara ya
Maliasili na Utalii, ili watambue pembe wanazotumia ni za mnyama gani.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
Thursday, 12 June 2014
Waganga wa kutibu kwa kutumia ngono na nguo za ndani wakamatwa Temeke
Related Posts:
BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO FEBRUARI 20 BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa ka… Read More
Watu Watatu wafariki wakiiba mafuta kwenye lori Watu watatu wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa wakati wakijaribu kuiba mafuta kutoka kwenye lori la kusafirisha mafuta aina ya petroli ambalo limepinduka na baadaye kulipuka na kuwaka moto katika kijiji cha Id… Read More
Kijana uawa na Simba alipokuwa anatoka kusaga Ifakara-Morogoro. Mwananchi mmoja amefariki dunia huko Ifakara Mkoani Morogoro ambaye hakuweza kutambulika hadi tunaweka taarifa hii.Tukio hilo lilitokea alipokuwa anatoka kusaga akielekea nyumbani kwake, akiwa njian… Read More
Watuhumiwa wanne wa uhalifu Amboni watiwa mbaroni Watuhumiwa wanne wa makundi ya uhalifu waliokuwa wamejificha katika mapango ya maji moto eneo la Amboni jijini Tanga, wametiwa mbaroni na jeshi la polisi kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na wananchi. Watuhumiwa wanne wa… Read More
Wanafunzi IFM wamuunga mkono Mh.Edward Lowassa kugombea Urais Wanafunzi wa Chuo cha IFM jijini Dar es Salaam wametangaza azma yao ya kumuunga mkono Edward Lowassa iwapo ataamua kugombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu 2015. Je wewe unadhani ni wakati sahihi kuonyesha ut… Read More
0 comments:
Post a Comment