Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Friday, 27 November 2015

Haya ndio maamuzi Magumu aliyoyafanya Waziri Mkuu baada ya kutembelea Mamlaka ya Bandari (TPA)

Waziri mkuu Kasim Majaliwa awasimamisha kazi kamishna wa kodi Tiagi Masamaki na Habibu Mpozya kitengo cha huduma kwa wateja kutokana ubadhilifu wa fedha kwa makontena zaidi ya 300 yaliyopotea.

Wengine ni Haruni Mpande -ICT, Hamisi Ali Omari na Eliachi Mrema incharge wa ICD na amemuru wrote wakamatwe  uchunguzi uendelee.

Walohamishwa kituo na kupelekwa mikoani ni Nsajigwa Mwandege, Robert Nyoni na  Anangisye  Mtafya

Vilevile Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa  wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.

Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.

Wednesday, 18 November 2015

Bomoa bomoa yaikumba Wilaya ya Kinondoni leo.

Hizi ni baadhi ya picha za bomoa bomoa katika eneo la tukio hapa Mwenge, baada ya hapo wameenda katika maeneo menginie ikiwemo Tegeta.

Inaelezwa kwamba wakazi waliokuwa wanaishi katika eneo la hilo walitakiwa kuondoka mapema kwa amri ya Serikali kutokana na kwamba maeneo hayo sio sehemu rasmi kwa makazi hivyo nyumba zote zilizokuwa zimewekewa alama ya mkasi zimebomolewa.

Zoezi hili ni muendelezo wa bomoa bomoa katika maeneo yatakayohusika na ubomoaji huo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni eneo la Biafra.


Baadhi ya majengo yaliyokuwa na maduka yamebomolewa.
Zoezi hilo likiendelea katika eneo la Mwenge.

Baadhi ya Askari wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi wakati wa bomoa bomoa

Kinondoni kuanza bomoabomoa leo

MANISPAA ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo inaanza ubomoaji wa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Kamishna wa Ardhi wizarani hapo, Moses Kusiluka aliwaambia waandishi wa habari kwamba maeneo yatakayohusika na ubomoaji huo ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni eneo la Biafra. “Ubomoaji huu unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Jumatano (leo) Novemba 18 hadi Ijumaa Novemba 20 mwaka huu,” alisema.
Alisema ubomoaji huo utahusisha nyumba zote zilizojengwa bila kibali cha ujenzi, bila kufuata michoro ya mipango miji na bila kufuata matumizi ya ardhi ambayo ni maeneo ya wazi.
Kamishna huyo alisema ubomoaji huo unafanywa baada ya kubaini kuwa maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma yamekuwa yakitumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.

NINACHOAMINI MAESTRO:->NIDHAMU NA MIPANGO YA MCHEZO VIMETUFIKISHA HAPA.

Na: Ayoub Hinjo(Ayo's Mata Maestro)

1. GAME APPROACH(MBINU ZA MCHEZO)

Nidhamu ya mchezo ni kitu ambacho kinaweza kuamua mchezo. Tanzania hatukuwa na nidhamu ya mchezo kwenye michezo yote miwili dhidi ya Algeria. Mbinu za mchezo zinaanzia kwa kocha,benchi lake la ufundi na mwisho kwa wachezaji. Sisi Tanzania hatuwezi kucheza kwa kutumia viungo halisi wawili kati kati sababu uwezo huo haupo kwa sasa sababu tunahitaji kucheza kitimu zaidi ya hivi tunavyocheza. Mbinu za kimchezo walizokuwa nazo Maximo na Kim Paulsen zilikuwa zinatupeleka sehemu sahihi sababu hauhitaji elimu ya juu kulifahamu hilo,tunahitaji kubalance timu kuanzia kati kati sababu mpira wa sasa matokeo yanaamuliwa kupitia hapo.

Mkwasa ni kocha mwenye profile kubwa hapa nchini lakini mbinu zake za kiuchezaji kuanzia kwenye mchezo dhidi ya Malawi hazikuwa nzuri kulingana na wachezaji ambao tunao. Kwa uhalisia maumbo ya wachezaji wetu wengi ni madogo na jinsi ambavyo sisi tunatakiwa kucheza ni kujaza viungo kati kati hili kuleta uwiano kwenye timu. Mfano wa hilo ni timu ya taifa ya Hispania,wachezaji maumbo yao hayaruhusu kucheza mpira wa juu na kugusana ndio maana kocha anaweka uwiano wa viungo wengi hili kuwa na mlinganyo sawa.

2: GAME AND INDIVIDUAL DISCIPLINE(NIDHAMU BINAFSI NA MCHEZO)

Hatuna nidhamu ya mchezo na hata mchezaji mmoja mmoja nidhamu zao hazirizishi na hili linatokana na makuzi ya mchezaji husika. Nidhamu ni silaha tosha ya kuwa na mchezo bora dhidi ya mpinzani tutaishia kusema tunahujumiwa na marefa. Mchezaji kama Mudathir Yaya alitakiwa kucheza kwa tahadhari zaidi hili kujilinda yeye na timu lakini hakuwa na nidhamu ya mchezo aliamua kucheza tu kama yupo uwanja wa Chamanzi sababu alishazoea. Baada ya Himid na Mudathir kupewa kadi za njano kocha hakuwa na chaguo zaidi ya kufanya mabadiliko ya kuingia kiungo wa kwenda kutoa msaada kwa wengine sababu viungo vyote vilikuwa vimelegezwa.

Wakati mwingine ni wachezaji wetu kutokuwa professionals inaweza kuchangia kupoteza mchezo na kushindwa kuwa na mbinu bora za wachezaji binafsi.

Tanzania tuna wachezaji wengi sana lakini tuna wa-organize vipi kwenye mipango na mbinu za kujenga timu yetu ya taifa!!? Hilo ni tatizo pia.

Askari 78 watimuliwa Mwanza

ASKARI 78 wa usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, wameondolewa katika nafasi zao na kupangiwa kazi nyingine katika vitengo mbalimbali kutokana na utovuwa nidhamu. .Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema mabadiliko hayo yamefanywa baada ya askari hao kujulikana hawafuati maadili na sheria za jeshi hilo.Mkumbo alisema kuwa askari waliondolewa nafasi hizona kupangiwa vitendo vingine ni 78, huku akisema kwamba wilaya ambayo haijafanyiwa mabadiliko ni Ukerewe kati ya saba za mkoa huo.“Tumefanya mabadiliko haya ni ya kawaida tu, tumefanya hivyo ili kuleta utendaji wenye tija, baadaya kubaini kuna mapungufu kwa askari hao na tusingeendelea kuwa nao kwa kuwa ni watovu wa nidhamu.“Wilaya ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Nyamagana askari 19, Ilemela 23, Sengerema 15, Magu 15, Misungwi na Kwimba mmoja (1), wilaya ambayo haijaguswa ni Ukerewe,”alisema Mkumbo.Hata hivyo Mkumbo alisema kuwa kabla ya kufanyika kwa mabadiliko hayo, walianza kutoa mafunzo kwa askari waliochukua nafasi hizo, kabla hawajaingia barabarani.Mkumbo alisema kuwa kabla ya mabadiliko hayo mkoa wa Mwanza ulikuwa na trafiki 249, na kwamba walioondolewa katika nafasi hizo ni askari wa kawaidana vyeo mbalimbali.

Tuesday, 17 November 2015

Utaangalia mechi ya Marudiano Kufuzu fainali za kombe la dunia :Algeria vs Tanzania kupitia BantuTv LIVESTREAMING.


BantuTv LIVE STREAMING:ALGERIA vs TANZANIA 21:15 USIKU.
 
Baada ya Timu ya taifa ya Tanzania katika michuano ya kufuzu kucheza fainali za la dunia kutoka sare ya Goli 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya 
Algeria katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Timu hizo zitacheza mchezo wa marudiano huko Algeria majira ya saa 3:15 Usiku kwa majira ya saa za Afrika Mashariki.

Mechi hiyo Kwa taarifa tulizozipata Bantuz.com itarushwa kupitia ZBC 2 kwa wenye KING'AMUZI CHA AZAM NI CHANNEL NAMBA 116, na vilevile kama patatokea matatizo yoyote katika kituo hicho unaweza kuungana na BantuTv kupitia BantuTv 
LIVESTREAMING.kwa kubofya link Hapo juu na kushuhudia  mtanange huu moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi, tablet au
Computer yako.

Monday, 16 November 2015

Diamond Platnumz na Vanessa Mdee washinda tuzo 4 za AFRIMA 2015 Nigeria

Tuzo za All Afrika Music Awards 2015 (AFRIMA) zimetolewa usiku wa Jumapili November 15 jijini Lagos, Nigeria ambapo Tanzania imetoa washindi wawili.

Diamond Platnumz aliyekuwa akiwania tuzo hizo ameibuka mshindi wa vipengele 3 kikiwemo kipengele muhimu cha Msanii Bora Wa Mwaka (Artist Of The Year) ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Alikiba, Davido, Jose Chameleone, Wizkid, Yemi Alade, Sarkodie na Flavour.Vipengele vingine alivyoshinda Diamond ni Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (Best Male Artist in Eastern Africa) pamoja na Wimbo Bora Afrika (Nasema Nawe)


Vanessa Mdee ameshinda kipengele cha ‘Best African Pop’ kupitia wimbo wake ‘Hawajui’.
msanii mwingine kutoka Tanzania 
aliewania tuzo hiyo 
Ni Linah ambae alikua kwenye kipengere cha msanii bora wa kike wa Afrika Mashariki

Sunday, 15 November 2015

Kundi la kigaidi la IS lakiri kuhusika na shambulizi la Paris-Ufaransa.

Kundi la kigaidi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi la Paris.Katika taarifa yake iliochapishwa mtandaoni,kundi hilo la kijihadi ,limesema kuwa shambulizi hilo lililenga kuielezea Ufaransa kwamba pia nayo ni miongoni mwa mataifa yanayolengwa na kundi hilo.

Kundi hilo limesema kuwa lilichunguza maeneo yalioshambuliwa na kutekeleza mashambulizi hayo kwa kuwatumia ndugu wanane waliovalia mikanda ya vilipuzi mbali na kujihami na bunduki.

ParisTangazo hilo lilitolewa katika maandishi ya kifaransa na kiarabu na kwa sauti zote kupitia idhaa za wapiganaji wa IS kulingana na mtaalamu wa habari za wanajihad Peter King.

Taarifa hiyo inadai kwamba ndugu wanne waliovalia vilipuzi na kujihami na bunduki waliyalenga maeneo yaliotengwa katikati mwa mji wa Ufaransa.Taarifa hiyo pia imeendelea na kutaja mji wa Paris kama mji mkuu wa 'uchafu na upotoshaji'.

Ujumbe wa IS''Katika shambulizi takatifu ,kundi la waumini la Ukhalifa -mwenyezi mungu alipe nguvu na ushindi-lililenga mji mkuu wa uchafu na upotoshaji,mji unaobeba bendera ya msalaba barani Ulaya,Paris'

Na Happiness Katabazi:- DK.TULIA ACKSON HUFAI KUENDELEA KUWA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Dk.Tulia Ackson  Novemba 11 Mwaka huu, amechukua fomu ya Kugombea nafasi ya Spika kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Ieleweke kwamba Cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ni Cheo Che kiutendaji na hivyo anayeshikilia Cheo hicho ni mtumishi wa Umma kwa maana Kuwa ni Wakili wa Serikali ambaye Sheria ya Utumishi wa Umma ha imruhusu Kuwa mwanasiasa wala kujiunga na vyama vya Vya siasa.

Lakini Dk.Tulia amejidhihirisha wazi Kuwa licha ni mtumishi wa umma mwenye Cheo cha juu serikali ni mwanasiasa wa CCM. Na Watendaji wa idara za Utoaji wa Haki kama Wanasheria wa serikali, Mahakimu na Majaji hawapaswi Kuwa wanasiasa wala kujiunga na vyama Vya siasa kwa Sababu ya kukwepa kukosa  kuaminiwa na umma Kuwa hawawezi Kutenda haki .

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.Tulia alipoenda kuchukua fomu ya Uspika mapema wiki hii ametudhihirishia yeye ni mwanasiasa na wakati huo huo ni mtumishi wa umma .

Ni wazi hafai kuendelea kushika Cheo hicho endapo akikosa Uspika kwasababu Tayari Utendaji wake umeanza kutiliwa Mashaka Kuwa hawezi Kutenda Haki kwa wananchi ambao  siyo wana CCM na ukweli ni kwamba amepoteza ' Public Confidence'.

Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inatoa haki kwa wananchi wake ya kuchagua, kuchaguliwa,au kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala".

Hivyo  Dk. Ackson  ambaye ni miongoni mwa wagombea Nafasi ya Uspika kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) , Ana Haki hiyo ya Kikatiba ya Kugombea nafasi hiyo ya Uspika licha ni Mtumishi wa serikali tena Mwandamizi.

Itakumbukwa Kuwa Septemba 9 Mwaka huu, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimteua Dk, Ackson Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao anaushikiria hadi sasa alikuwa ni Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.

Dk.Ackson  kwa sasa siyo Mbunge ila anagombea nafasi ya Spika kwasababu Ibara ya   84(1) ya Katiba ya nchi inatoa haki kwa mwananchi kugombea nafasi hiyo ya uspika hata kama siyo Mbunge na inasomeka hivi ;

"  Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge."..

Nimelazimika kuandika makala hii Leo kwasababu uamuzi wa Dk.Ackson Kugombea nafasi ya Uspika wakati akiwa na wadhifa wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye Moja ya jukumu la Mwanasheria Mkuu wa serikali kuishauri serikali Katika masuala yote ya Sheria.

Kwanza napenda kumpongeza Dk.Ackson kwa kuteuliwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali mwanamke mwanamke wa kwanza Tanzania tena mwenye  umri Mdogo .Hongera sana .

Pili nampongeza kwa ujasiri wake wa kuamua kujianika hadharani bila kujali madaraka makubwa aliyonayo wala miiko ya Kazi yake ya Mwanasheria wa Serikali  Kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM  na mwanasiasa.

Tatu nampongeza Dk.Acksonkwa uwazi  wake wa kuamua Kugombea nafasi ya Uspika ikiwa ni siku Chache tu tangu alipoteuliwa Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9 Mwaka huu. Hatari sana.

Nne, Nampongeza sana Dk.Ackson  kwa kuchukua fomu ya Uspika kwasababu ni wazi sasa umedhiirishia umma Kuwa hiyo Nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,haitaki  na Cheo hicho ni kidogo sana kwake hivyo unataka Cheo kingine kikubwa Uspika.Yangu  macho.

Tuelezane ukweli ,licha Dk.Ackson  Ana Haki ya Kugombea nafasi hiyo nanina mgombea     ashinde licha kwa asilimia 99 hawezi kushinda nafasi ya Spika .Na ikitokea Akakosa hiyo nafasi umma hasa vyama Vya upinzani  utamwamini tena Katika Utendaji wake?

Maana siyo Siri Dk.Ackson  alipoenda kuchukua fomu Tayari Yale maneno yaliyokuwa yakisemwa na wapinzani Kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ina baadhi ya Wanasheria wa serikali wanatumiwa na CCM kwa   maslahi ya CCM licha wapinzani Hao hawakuwahi kutoa vielelezo vinavyoonyesha ni Mwanasheria yupi wa serikali ni Mwana CCM.

Lakini kupitia Mgombea Uspika ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  sasa wapinzani wamepata ushahidi Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye ni mtumishi Mwandamizi wa serikali  Mwana CCM na uthibitisho ni kwamba ametumia Kadi yake ya uaachama wa CCM kwenda Kugombea nafasi ya Uspika.

Hivyo ni wazi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi sasa imebaki Ukitazamwa ndivyo sivyo kwasababu ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda Kugombea nafasi ya Uspika kwa tiketi ya CCM .

Kama hivyo ndivyo, huyu Dk.Ackson  uchaguzi wa Spika ukimalizika na ikatokea akashindwa hivi akirudi ofisini kwake wananchi tutakuwa tunamtazamaje zaidi ya kubaki na hisia na maswali dhidi yake Kuwa hawezi Kutenda Haki sawa kwa wote kwasababu Tayari ameishaonyesha yeye ni Mwanachama wa CCM wakati hapaswi Kuwa mwanasiasa ?

Uchaguzi Mkuu umekwisha ,Kesi za kupinga Matokeo ya Ubunge lazima zitafunguliwa Katika baadhi ya Mahakama zetu na Kesi hizo mdaiwa wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbunge aliyeshinda na Msimamizi Wa uchaguzi.

Enzi zake Mwanasheria Mkuu wa sasa George Masaju akiwa na wadhifa wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa akienda Mahakamani Mwenyewe kuiwakilisha serikali pindi iliposhitakiwa au serikali ilipofungua Kesi dhidi ya mtu,au Taasisi Fulani.

Hata sasa hivi Mwanasheria Mkuu wa serikali hazuiwi kwenda mahakamani kuendesha baadhi ya Kesi ila kutokana na jukumu zito anaamua  kukasimu majukumu Mawakili wa serikali na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Na Mfano hai ni Oktoba Mwaka huu, Kada wa Chadema alifungua  Kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam itoe Tafsiri ya mita 200 Katika Kesi maarufu ya mita 200 .

Masaju alimtwisha jukumu hiyo Naibu wake Dk.Tulia na Wanasheria wengine wa serikali kwenda kutetea Kesi hiyo hiyo na hatimaye walishinda.

Swali langu Je , itokee siku aliyekuwa mgombea Ubunge wa vyama Vya upinzani Kufungua Kesi ya kupinga Ubunge wa Mbunge wa CCM halafu Dk.Ackson  aende kuitetea hiyo Kesi mahakamani.

Je Yule mlalamikaji ambaye alikuwa mgombea toka vyama Vya upinzani akiiambia  Mahakama Kuwa Hana Imani na Dk.Ackson  Katika Kesi hiyo kwasababu ni Kada wa CCM na hivyo hatoweza kusaidia Mahakama Kutenda Haki Atakuwa amekosea?

Sina Chuki na Dk.Ackson  na sina Sababu ya Kujenga Chuki naye ,ila tu napenda kumweleza kijana mwenzangu Kuwa Kabla ya kuchukua uamuzi aliouchukua wa Kugombea Uspika akijitafakari kwanza yeye kwasasa ni nani?Ana wadhifa gani?Anafahamu Jamii itamtafsiri vipi?

Je anapoenda Kugombea Uspika awe na uhakika Kuwa atashinda na asiposhinda basi atakuwa amejipunguzia  asilimia za kutoaminiwa Katika suala zima za Utoaji Haki hasa Katika vyombo vyetu Vya Sheria hata kama Atakuwa anatenda Haki kweli kwasababu Tayari ameishauthibitishia umma yeye ni Mwanachama wa Chama Fulani.

Hivi Leo hii itokee Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mgonjwa au amesafiri nje ya nchi au amefariki ghafla na hivyo kusababisha Naibu Mwanasheria wa Serikali Dk.Tulia kukaimu Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ,awe Bungeni anatoa ushauri wa kisheria ndani ya Bunge kuhusu muswaada Fulani au jambo Fulani ambalo wabunge wa upinzani hawalitaki hata kama ni kweli Dk.Tulia yupo sahihi kisheria, wale Wabunge wa upinzani wakiamua kumpinga kwa Kigezo yeye anatetea huo muswaada kwasababu pia ni Mwanachama wa CCM, at akasirika au sisi wananchi na viongozi wa serikali hiyo Hali watachukuliaje?

Kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya nchi inasema Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifa .

Ibara hiyo haijasema Mwanasheria Mkuu wa serikali atakuwa mbunge  
wa Chama Fulani cha siasa.

Ieleweke kwamba uteuzi wa Dk.Ackson  ulizua  minong'ono na maswali mengi chini kwa chini kutoka Katika Kada ya Wanasheria hasa wa serikali licha ana elimu nzuri licha tu hajawahi Kuwa Wakili wa serikali na Hana udhoefu wa uendeshaji wa Mashitaka.

Baadhi ya watu wa Kada ya Sheria Walisema licha Rais anayo mamlaka ya Kumteua mtu yoyote kushika wadhifa wowote ,Walisema aikuwa busara kwa  Rais Kikwete   kuacha kuteua Mawakili wa serikali kushika Nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwenda kumteua Dk.Ackson  ambaye hata miiko ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali hajaijua .

Kumbe sasa wale waliokuwa wakipata Mashaka kuhusu Utendaji wa Dk.Ackson kwa upande Fulani sasa tunaweza Kusema walikuwa sahihi kwasababu kitendo cha Dk.Ackson Kugombea nafasi ya Uspika wakati yeye ni mtumishi wa umma na hapaswi Kuwa mwanasiasa tena katika kipindi kifupi tu ni dhahiri sasa miiko ya Kazi yake haifahamu na hakutaka kuifahamu  akaamua kukurupuka na kufanya hicho alichokifanya ambacho kimesababisha watu kutulia mashaka utendaji wake.Aibu sana.

Kuna taarifa zisizo rasmi Kuwa Dk.Ackson ametumwa kwa makusudi na kiongozi mmoja Mwanamke ambaye ni Waziri na ana nafasi kubwa ndani ya CCM agombee nafasi hiyo   ili aende kuwaganya kura za baadhi ya wagombea Uspika ambao ni tisho kwa hao waliomtuma Dk.Ackson.

Kwa Kuwa sina ushahidi na taarifa hizo Mimi nitabaki kuamini Dk.Ackson amegombea Uspika bila kutumwa na mtu.

Ila taarifa hizo   ziwe za kweli  au siyo za uzushi, zinazidi kujengea Mashaka Utendaji wa  Dk.Ackson kutokana na Cheo Chake na yote hayo yanampata na yatazidi  kumpata kwasababu ameamua kuingia Kwenye siasa ,asingeingia huko yasingemfika.

Hakuna ubishi Kuwa Dk.Ackson  kwa kitendo chake cha kugombea uspika licha ana haki ya Kikatiba kugombea, amedhihirisha kuwa yeye ana papara ya kupata madaraka makubwa tena kwa vipindi vifupivifupi ili Hali bado Ana umri Mdogo.

Ushahidi ni huu Septemba 9 kateuliwa na Rais Mstaafu Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Novemba 11 Mwaka huu, kachukua fomu ya Kugombea Uspika.

Hivi tukisema Dk.Ackson  ameudharau,aupendi na autaki uteuzi  Rais Kikwete wa alipomteua yeye Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali tutakuwa Tunakosea?

Maana Aiingii akilini kwa Kipindi kifupi hicho alichoteuliwa kushika nafasi hiyo nzito serikali halafu aamue kwenda kuwania nafasi ya Uspika halafu tuache kuamini kuwa Dk.Ackson  ile nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaipenda?

Aipendi na ninatabiri anaweza asidumu Katika wadhifa huo kwa muda mrefu kwasababu Tayari ameishaonyesha wazi Ana tamaa ya kupata madaraka makubwa kwa harakahara na hataki kujifunza Kazi kutoka Kwa waiomtangulia na akae akijua baadhi ya watendaji wake wa chini wamekerwa na yeye kiongozi wao kujiingiza Kwenye siasa wakati haruhusiwi Kuwa Mwanachama wa Chama cha siasa.

Hivi wewe Dk.Ackson  kama umegombea Uspika sasa ,nikuulize Je umepata muda saa ngapi ya kukaa na Mawakili wa serikali wakawa wana kufundisha jinsi ya kuendesha hiyo Ofisi na wewe ukapata uzoefu ?

Ni wazi bado unaitaji kupikwa na Wanasheria wa serikali ili uive  lakini ni wazi sasa umeonyesha hata huo muda wa kukaa kitako upikwe na watangulizi wako katika hiyo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali huna unawaza Kugombea madaraka ya kisiasa.Huzuni.

Minakushauri, kuliko kuendelea kushikilia nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati matamanio yako ni Kugombea Uspika na siasa, ni vyema ungeandika barua ya kujihudhuru wadhifa huo mapema ili Rais mpya Dk.John Magufuli ateue mtu mwingine ambaye kwanza ana uzoefu na kazi ya wakili wa serikali ambaye akili zake zimetulia,maana wewe bado hujatulia ili afanyekazi.

Wewe Dk,Ackson tayari  umeishaonekana mguu mmoja upo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mguu mwingine upo CCM Kugombea madaraka makubwa ya kisiasa.

Sasa mtu wa aina ya Dk. Tulia ni wazi Utendaji wake katika madaraka aliyonayo hautakuwa mzuri maana muda mwingi atakuwa fikra za kupanga mikakati ya jinsi ya kupata nafasi nyingine kubwa zaidi ya hiyo tena kwa chap chap.

Dk.Tulia unapaswa utambue jambo Moja Kuwa wanasiasa siyo watu wa kuaminika sana.Wakikupa ushauri wa kufanya jambo lolote hata hili la Kugombea Uspika ulitakiwa ulitafakari sana kwamba endapo ukikosa nafasi hiyo wewe hadhi yako Mbele ya Jamii inakuwaje.

Umeanza kutiliwa Mashaka na baadhi ya Jamii,lakini waliokushauri  ugombee Uspika hawatakusaidia kuminya fikra za watu na baadhi ya watendaji wako wasikuone wewe ufahai tena kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa kitendo Chako cha Kugombea Uspika kupitia CCM licha siyo kosa la jinai.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa Dk.Ackson endapo ukikosa nafasi ya Spika ,hufai kuendelea Kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwasababu Tayari umeonyesha wewe ni mwanasiasa hivyo Utendaji wako unatiliwa Mashaka.

Pia nakushauri acha pupa ya kuwania  madaraka ili Hali wewe ni msomi na bado ni binti Mdogo sana licha una elimu kubwa lakini bado unaitaji kuelewa,kupikwa na waliokutangulia na wenye uzoefu Katika eneo la Mawakili wa Serikali ,siasa utafanikiwa.

Au kama fikra na moyo wako hautaki uendelee Kuwa na  Cheo cha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,zinakutuma kwenda kufanya siasa ni vyema basi ukaomba Kibali cha kumuona Rais Magufuli ili umeombe akutoe Katika Cheo hicho au wewe Mwenyewe andika barua ujiudhuru kuliko kufanya hili uliofanya  ambalo linakatazwa kabisa Kuwa Mwanasheria wa serikali Kuwa mwanasiasa lakini wewe mwenzetu bila woga tena hadharani umeonyesha wewe ni mwanasiasa wakati huo huo ni mtumishi wa umma.

Dk.Ackson nakupenda ebu punguza kasi kidogo ya matamanio ya kupata madaraka inakusaidia Kwani Mtaka yote ukosa yote Waswahili Walisema.Nakutakia kila la kheri Katika mbiyo zako za Uspika.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
14/11/2015

Saturday, 14 November 2015

Mamba wakali kutumika kulinda wafungwa Indonesea.

Mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Indonesia amependekeza mamba watumiwe kulinda wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.

Budi Waseso anataka taifa hilo lijenge gereza kwenye kisiwa na kizingirwe na mamba akisema wanyama hao ni walinzi bora kushinda wanadamu, kwani hawawezi kuhongwa.Amesema atazuru maeneo mbalimbali katika taifa hilo kutafuta mamba wakali zaidi.

Indonesia ina moja ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya duniani na ilianza tena kunyonga watu baada ya kusitisha hukumu hiyo kwa miaka minene 2013.

"Tutaweka mamba wengi sana huko,” Bw Waseso alinukuliwa na tovuti moja nchini humo kwa jina Tempo."Huwezi kuwahonga mamba. Huwezi kuwashawishi waruhusu washukiwa watoroke.”Mpango huu bado umo katika hatua za mwanzo mwanzo na bado haijaamuliwa gereza hilo litakuwa wapi na ni lini litafunguliwa.

Hizi ndizo Channel zitakazorusha moja kwa moja mechi Tanzania vs Algeria.

Hii ni mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili kufuzu kuelekea Kombe la Dunia 2018.Ni mechi muhimu kwa timu ya taifa ya Tanzania maana itakuwa nyumbani uwanja mkuu wa Taifa.Katika michezo mitano ya mwisho timu ya Tanzania imeshinda mchezo mmoja pekee, huku ikitoka sare michezo miwili na kufungwa miwili.

Algeria wao katika michezo mitano ya mwisho wamepoteza mchezo mmoja tu na kushinda mingine minne iliyobakia.Hadi sasa Tanzania na Algeria zimeshakutana mara 7, huku mara 3 Algeria ikishinda, mara 1 Tanzania ikishinda na mara 3 ikiwa ni sare.

Kupitia uzi huu tuungane pamoja kushuhudia kile kitakachojiri siku ya mchezo.TANZANIA - ALGERIA16:30Waamuzi: Keita Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory

TV Listing :ZBC 2, TBC1, Bein Sports 1HD(Bein US)

Kikosi TZ: 
Ally Mustapha, Shomari Kapombe, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondani, Nadir Haroub, Himidi Mao, Mudathir Yahya, Mrisho Ngassa, Farid, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu

Maalim Seif atangaza kutoshiriki Uchaguzi utakaorudiwa Zanzibar.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF Zanzibar Maalim Seif amesisitiza tena kuwa yeye na chama chake hawatoshiriki kwenye zoezi la kurudia Uchaguzi Visiwani Zanzibar kama ilivyotangazwa na ZEC

Ameyasema hayo Jijini Dar baada ya kikao na vyama vinavyounda UKAWA kukutana Jijini Dar es Salaam jana, pamoja na aliyekuwa mgombea Urais Edward Lowassa.

Taarifa kamili kuhusiana na Shambulio la kigaidi lililotokea Paris-Ufaransa.

Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.

Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.

Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa

Mashabiki waliingia uwanjani baada ya milipuko kutokea Stade de France.

Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.

Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.

Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa "bila huruma".

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ali hutubia taifa.

Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako mwandishi mmoja anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine kufarikiMoja kwa moja:

Habari za karibuni zaidi kuhusu shambulio Paris Mtu aliyeshuhudia amesema ya kwamba naye alisikia risasi zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika mtaa nambari 11.

Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles.Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa "jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia" na kuahidi kusaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika."Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja," amesema.

Polisi wa Ufaransa walosogea karibu na eneo la ukumbi wa Bataclan  "Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.

”Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya "lolote tunaloweza kufanya kusaidia.

Friday, 13 November 2015

Pato la Manchester United laongezeka Maradufu katika robo ya Kwanza ya Mwaka wa Kifedha.

Klabu ya soka ya Manchester United imetangaza mapato yao ya robo ya Kwanza ya Mwaka wa Kifedha.Klabu hiyo pia iko mbioni kuvunja rekodi ya kuvuka Mapato ya pauni milioni 500 na kuweka Rekodi ambayo hajafikiwa na Klabu yeyote.

Mapato ya Man United kwa Miezi Mitatu, iliyoiishia Septemba, ni Pauni Milioni 123.6 ikiwa ni ongezeko la Asilimia 39 kwa kipindi kama hiki kwa Mwaka 2014.

Pia mapato yameongezeka baada ya kusaini Mkataba mpya na kampuni ya vifaa vya michezo vya Adidas ambayo yatawaingizia Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10 ukiwa ni Mkataba mkubwa kabisa Duniani kwa Klabu na Watengeneza Vifaa vya Michezo.

Vilevile, kushiriki kwa timu hiyo katika michuano ya Uefa Championz ligi kumechangia ongezeko la pato lao kwenye Matangazo ya Mechi kwa Asilimia 64.3.

Asilimia 64.2 hutokana na vingilio vya mashabiki pamoja na kuuzwa kwa bidhaa nyingine zikiwemo jezi.

Pambano kati ya Brazil dhidi ya Argentina lasogezwa mbele kutokana na hali mbaya ya hewa.

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Brazil na Argentina umeahirishwa sababu ya mvua nyingi kunyesha.

Mchezo huo iliokua uchezwe usiku wa siku ya alhamisi katika uwanja wa Estadio Antonio Vespucio Libert, mjini Buenos Aires sasa utachezwa usiku wa siku ya ijumaa.

Sehemu ya kuchezea ya uwanja huo ulijaa maji na washabiki wa soka pamoja na maafisa wa timu ya Brazil walikwama njiani kwenye foleni sababu ya mvua kubwa iliyonyesha.

Kocha msaidizi wa Brazil Gilmar Rinaldi, alisema "tulikutana na maafisa wa soka wa Argentina tukazungumza na hakukua na namna ya mchezo kuchezwa.

Katika mchezo huu Argentina itamkosa Nahodha wake Lionel Messi anayesumbuliwa na maumivu wakati Brazil itakuwa nae tena Nahodha wao Neymar Jr ambae hakucheza Mechi 2 za mwanzo akutokana na kuwa adhabu ya kutocheza michezo minne.

Kikwete afurahia kasi ya Rais Magufuli.

Rais aliyeondoka mamlakani majuzi nchi Tanzania amesifu jinsi Rais mpya John Magufuli ameanza kufanya kazi na kumtaka aendelee vivyo hivyo.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema hayo wakati wa kukabidhi rasmi ofisi yake kwa Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5 baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25.

“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi,” alisema Bw Kikwete.

Dkt Magufuli amekuwa akifanya ziara za kushtukiza, ya kwanza ikiwa katika makao makuu ya Wizara ya Fedha siku yake ya kwanza kazini ambako aliwakuta wafanyakazi wengi wakiwa wametoka ofisini.

Siku chache baadaye, alifanya ziara ya kushtukiza hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alisikitishwa na utoaji huduma.Hafla ya kukabidhi rasmi afisi kwa Rais Magufuli ilishuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.

Magufuli alisikitishwa na utoaji huduma Muhimbili na akabadilisha usimamizi wa hospitali hiyoKwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, Rais mstaafu Kikwete alimkabidhi Rais Magufuli taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji.Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Klabu ya Lille yawasilisha rasmi ofa ya kumsajili Samatta.

Klabu ya Lille inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa imewasilisha rasmi ofa ya kumsajili mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC) na Taifa Stars, imefahamika.

Katika mahojiano na moja ya vituo vya televisheni vya Afrika Kusini usiku wa kuamkia jana, Mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alisema klabu hiyo imewasilisha maombi hayo na sasa wanasubiri kuitwa kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

Katumbi alisema Lille ndiyo klabu ambayo imekuwa ikikumbushia maombi yake mara kwa mara tofauti na klabu nyingine zilizowasilisha maombi ya kumnasa straika huyo ambazo hata hivyo, hakuwa tayari kuzitaja.

Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo, pia alikiri kufahamishwa juu ya ofa ya Lille na kueleza kuwa waliamua kusimamisha mazungumzo kuzipa kipaumbele mechi mbili za fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya USM Algiers ambazo TP Mazembe walishinda zote na kutwaa ubingwa.

"Hiyo ofa ninaijua, ilikuwa mapema na tulikubaliana mjadala wake uanze baada ya mechi za fainali kumalizika, wakati wowote tunaweza kukutana nao kwa ajili ya kuijadili," alisema meneja huyo.

Kisongo aliongeza kuwa hawatakuwa na papara katika kufanya uamuzi kwa sababu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yuko katika kiwango cha hali ya juu kwa sasa.

Alipotafutwa na mtandao huu wa
Bantuz jana kuzungumzia masuala ya usajili, Samatta alisema atakuwa tayari kuanza kuzungumzia mahali anapokwenda baada ya kuitumikia nchi (Taifa Stars) katika mechi mbili zinazoikabili dhidi ya Algeria.

Serikali yasimamisha wafanyakazi 4 kwa tuhuma za wizi wa kuaminika Kilimanjaro.

Wafanyakazi wanne wa halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamesimamishwa kazi na mweka hazina wa hospitali ya machame amefukuzwa kazi kwa tuhuma mbili tofauti za wizi wa kuaminika wa kujipatia zaidi ya shs.74mil/=.

Mkuu wa wilaya hiyo Bw Antony Mtaka amesema, wafanyakazi wawili wa idara ya fedha Valentine Elisha na Edwin Kalokora wamehusika kugawana shs. 38mil/=kwa ushirikiano na mweka hazina huyo Philipo Masasi ambazo zilikuwa posho ya kujikimu madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo. 

Bw Mtaka amewaambia wafanyakazi wa hospitali hiyo ya KKKT kuwa, wafanyakazi wawili wa idara ya utumishi Faraja Ndatu na Isaya Bahege  walighushi nyaraka za serikali zikiwemo nembo za halmashauri na saini za madaktari waliofariki na kustaafu na kuchukua mkopo wa shs. 36mil/= kutoka benki ya CRDB. 
Mkurugenzi wa hospitali ya Machame Dr Laiser Saitore amesema, fedha hizo ziliidhinishwa kisheria na wahusika wote kati ya Nov 2014 hadi Feb mwaka huu lakini hazijafika katika hospitali hiyo hadi sasa. 

Mganga mkuu wa wilaya ya Hai Dr Paul Chaote amesema, ufisadi wa fedha hizo waliugundua baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Saitore kutokana na kutowasili kwa fedha hizo kwa miezi nane. 

Ronaldo anunua 'Private Jet' kwa zaidi ya Bilioni 44.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo anaripotiwa kutumia mkwanja mrefu kununua ndege binafsi, Staa huyo anayeongoza katika list ya rekodi ya watu maarufu wanaongoza kupata likes nyingi katika mtandao wa facebook amenunua ndege binafsi aina ya Gulfstream G200 Business Jet.
CTmoKwwUkAALhqc
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 anatajwa kununua ndege hiyo kwa thamani ya pound milioni 13.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 44 za kibongo kwa ajili ya kuzunguuka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na mipango yake ya kujitanua kibiashara, ndege ya staa huyo inatajwa kuwa na uwezo wa kubeba watu 8 hadi 10, jiko la umeme, bafu, friji, makabati, simu na internet.
CTmoLGsUwAAD05O
Nyota huyo ambaye anaonekana kujiimarisha zaidi kibiashara tayari amezindua movie ya maisha yake halisi aliyoizindua hivi karibuni Uingereza ila mwaka 2015 alitajwa kuzindua perfume, brand ya viatu vyake.
CTmoLjrU8AA1tuN
Sports-people-and-Private-jets
Cristiano Ronaldo akiwasili uwanja wa ndege wa Centrair International airport uliyopo Nagoya Japan kwa ndege yake binafsi.
GettyImages-79579622-742x505
CR7-742x474

Bantuz MAGAZETINI-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 13.

DSC02252BantuTz MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusoma na kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu baada ya maombi ya wadau mbalimbali. DSC02248 DSC02249 DSC02250 DSC02251  DSC02253 DSC02254 DSC02255 DSC02256 DSC02257 DSC02258 DSC02259 DSC02261 DSC02262 DSC02263 DSC02264 DSC02265 DSC02266 DSC02267 DSC02268 DSC02269 DSC02270 DSC02271 DSC02272 DSC02273 DSC02274 DSC02275 DSC02276 DSC02277 DSC02278 DSC02279 DSC02280 DSC02281 DSC02282 DSC02283 DSC02284Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz hapo mwakani.