Kinondoni kuanza bomoabomoa leo
MANISPAA
ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi leo inaanza ubomoaji wa nyumba zilizojengwa bila kufuata
taratibu za ujenzi.
Kamishna
wa Ardhi wizarani hapo, Moses Kusiluka aliwaambia waandishi wa habari
kwamba maeneo yatakayohusika na ubomoaji huo ni Mbezi, Tegeta, Bunju,
Mwenge na Kinondoni eneo la Biafra. “Ubomoaji huu unatarajiwa kufanyika
kwa siku tatu kuanzia Jumatano (leo) Novemba 18 hadi Ijumaa Novemba 20
mwaka huu,” alisema.
Alisema
ubomoaji huo utahusisha nyumba zote zilizojengwa bila kibali cha
ujenzi, bila kufuata michoro ya mipango miji na bila kufuata matumizi ya
ardhi ambayo ni maeneo ya wazi.
Kamishna
huyo alisema ubomoaji huo unafanywa baada ya kubaini kuwa maeneo
yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya
wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma yamekuwa
yakitumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kukosesha
umma manufaa yaliyokusudiwa.
0 comments:
Post a Comment