Facebook

Wednesday, 18 November 2015

NINACHOAMINI MAESTRO:->NIDHAMU NA MIPANGO YA MCHEZO VIMETUFIKISHA HAPA.

Na: Ayoub Hinjo(Ayo's Mata Maestro)

1. GAME APPROACH(MBINU ZA MCHEZO)

Nidhamu ya mchezo ni kitu ambacho kinaweza kuamua mchezo. Tanzania hatukuwa na nidhamu ya mchezo kwenye michezo yote miwili dhidi ya Algeria. Mbinu za mchezo zinaanzia kwa kocha,benchi lake la ufundi na mwisho kwa wachezaji. Sisi Tanzania hatuwezi kucheza kwa kutumia viungo halisi wawili kati kati sababu uwezo huo haupo kwa sasa sababu tunahitaji kucheza kitimu zaidi ya hivi tunavyocheza. Mbinu za kimchezo walizokuwa nazo Maximo na Kim Paulsen zilikuwa zinatupeleka sehemu sahihi sababu hauhitaji elimu ya juu kulifahamu hilo,tunahitaji kubalance timu kuanzia kati kati sababu mpira wa sasa matokeo yanaamuliwa kupitia hapo.

Mkwasa ni kocha mwenye profile kubwa hapa nchini lakini mbinu zake za kiuchezaji kuanzia kwenye mchezo dhidi ya Malawi hazikuwa nzuri kulingana na wachezaji ambao tunao. Kwa uhalisia maumbo ya wachezaji wetu wengi ni madogo na jinsi ambavyo sisi tunatakiwa kucheza ni kujaza viungo kati kati hili kuleta uwiano kwenye timu. Mfano wa hilo ni timu ya taifa ya Hispania,wachezaji maumbo yao hayaruhusu kucheza mpira wa juu na kugusana ndio maana kocha anaweka uwiano wa viungo wengi hili kuwa na mlinganyo sawa.

2: GAME AND INDIVIDUAL DISCIPLINE(NIDHAMU BINAFSI NA MCHEZO)

Hatuna nidhamu ya mchezo na hata mchezaji mmoja mmoja nidhamu zao hazirizishi na hili linatokana na makuzi ya mchezaji husika. Nidhamu ni silaha tosha ya kuwa na mchezo bora dhidi ya mpinzani tutaishia kusema tunahujumiwa na marefa. Mchezaji kama Mudathir Yaya alitakiwa kucheza kwa tahadhari zaidi hili kujilinda yeye na timu lakini hakuwa na nidhamu ya mchezo aliamua kucheza tu kama yupo uwanja wa Chamanzi sababu alishazoea. Baada ya Himid na Mudathir kupewa kadi za njano kocha hakuwa na chaguo zaidi ya kufanya mabadiliko ya kuingia kiungo wa kwenda kutoa msaada kwa wengine sababu viungo vyote vilikuwa vimelegezwa.

Wakati mwingine ni wachezaji wetu kutokuwa professionals inaweza kuchangia kupoteza mchezo na kushindwa kuwa na mbinu bora za wachezaji binafsi.

Tanzania tuna wachezaji wengi sana lakini tuna wa-organize vipi kwenye mipango na mbinu za kujenga timu yetu ya taifa!!? Hilo ni tatizo pia.

0 comments:

Post a Comment