Mtangazaji wa kipindi cha XXL na Bongo Fleva ya Clouds Fm, Adam Mchomvu a.k.a Baba Jonni,siku ya juma pili anatarajia kudondosha mzigo wa video za nyimbo zake mbili ndani ya Maisha Club.
Licha ya wimbo wake wa Jonny kunfanya aonekane zaidi kwa upande wa Muziki, Mchomvu atazindua video mbili, ikiwa ni ya Au Sio na Una Akili wewe. vido ambazo zimefanya na kampuni mbili tofauti moja ikiwa imesimamaiwa na HK, na nyingine imesimamiwa na Benjamin wa Mambo Jambo.
"Baada ya watu wengi kujua game ninayofanya, na wengi wao kuona kama
siko serious, ndio maana kwa sasa nimeamua kuingia katika Mziki kwa
miguu yote miwili..." amesema Adam
Mchomvu atazindua video hizo akiwa na wasanii kibao kama T.I.D, County
Boy, Chege, Juma Nature, KCK, Mirror, Dogo Asley, Godzilla, Weusi na
wengineo, huku Kwenye Mc wa show hiyo akiwa ni Fid Q
0 comments:
Post a Comment