SERGIO Busquets amekiri kuwa matumaini ya Barcelona kutetea ubingwa wao wa La Liga msimu huu yamekwisha baada ya sare ya jana ya mabao 2-2 dhidi ya Getafe.
Barcelana walianza kufunga mara mbili kupitia kwa Lionel Messi
na Alexis Sanchez, lakini Getafe walichomoa yote kupitia kwa Angel
Lafita.
Bao la dakika za lala salama la Lafita limewafanya Barcelona kuwa pointi tatu nyuma ya vinara Atletico Madrid ambao wanaweza kufikisha pengo la pointi sita kama watawafunga Levante leo jumapili.
“La Liga kwetu tumeikosa. Kimahesabu hatuwezi”. Busquets amewaambia waandishi wa habari.
“Kwa wiki za karibuni hatujawa katika kiwango kizuri, lakini tulijitahidi kushinda mechi zetu, matokea kama ya leo (jana) yanawezekana kutokea”.
“Tulimiliki mpira na kupata nafasi za kufunga, tunatakiwa kujipanga zaidi na kucheza kitimu ili kushinda mechi zijazo”.
Kocha Tata Martino amekubali kubeba lawama zote kutokana na msimu mbaya kwa Barcelona, lakini Busquets amesema wachezaji nao wanatakiwa kushirikiana na kocha kubeba msalaba huu mzito kwao msimu huu ambapo wanaweza kumaliza bila kombe.
“Tulifungwa mabao ambayo hatukustahili kufungwa. Makosa ni kwa timu nzima”. Alilaumu kiungo huyo.
“Tumebakiwa na mechi mbili na tutajitahidi kushinda kwasababu tunaichezea klabu bora zaidi duniani”.
“Labda msimu ujao tutakuwa wazuri zaidi”.
Barcelona watasafiri kuwafuata Elche kabla ya kuwakaribisha Atletico Madrid katika mchezo wa mwisho.
Kama Atletico watashinda mechi zao mbili za mwisho, watakuwa wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa La Liga.

RATIBA YA LA LIGA LEO HII HAPA
SPAIN: Primera Division | |||||||
13:00 | Almeria | - | Betis | ||||
18:00 | Levante | - | Atl. Madrid | ||||
20:00 | Sevilla | - | Villarreal | ||||
22:00 | Real Madrid | - | Valencia |
0 comments:
Post a Comment