Facebook

Wednesday 7 May 2014

Azam tv wafanya kufuru...


Photo: Haya sasa...

Wapenzi wa Ku Dunk na Ku Dribble hapa nazungumzia Basketball ama mpira wa kikapu, Nyumba ya Burudani ya Michezo Tanzania Azam TV inakuletea: 

InterCity Basketball Championship 

Mashindano ya majiji makubwa na makuu katika nchi mbalimbali za Kanda ya Afrika Mashariki na kati, Manguli wa Vikapu watapambana ubavu,pumzi na kasi kupatikana mshindi mmoja atakayetambulika kwa majiji yote ya timu shiriki.

Hapa nazungumzia manguli kutoka Jiji la Kampala, Nairobi, Mombasa, Addis Ababa, Bujumbura, Arusha, Cairo, Mbeya, Mwanza na wengineo wengi bila kusahau wenyeji wa Mashindano haya kutokea Dar es salaam.

Kwa mara ya 16 tokea kuanzishwa kwake,mwaka huu jiji la Dar es  salaam limechaguliwa kuwa ni jiji pekee mwenyeji wa mashindano haya Yatakayofanyika Pale Indoor Uwanja wa Taifa wa Zamani tarehe 6-11 mwezi huu..

Watanzania,wapenzi wa michezo na wapenzi wa mpira wa kikapu tujitokeze kesho Indoor kuanzia saa 2 asubuhi kushuhudia mashindano haya ya manguli hawa wa Basketball.

Mashindano haya yatakujia Live ndani ya chanel ya Azam Two kupitia mdhamini pekee Azam Energy Drink.

Azam TV Burudani kwa Wote.
 
AZAM Tv imefanya kufuru kwa kutoa udhamini wa Sh 361.6 milioni kwa ajili ya kurusha ‘live’ mashindano ya mpira wa kikapu ya Miji Mikuu ya Afrika Mashariki na Kati, ambayo yanaanza leo Jumanne Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yatafanyika kwa siku sita kuanzia leo Jumanne mpaka Jumapili, Azam itakuwa inarusha mechi zote kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku mechi hizo zinapomalizika kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo.


Kurusha mechi moja kwa saa moja ni Dola 3,000 (Sh 4.8 milioni) ambapo kwa saa 12 itakuwa ni Sh57.6 milioni na hivyo kwa siku sita ni sawa na Sh345.6 milioni. Imeelezwa kuwa Azam wameahidi kusaidia bajeti ya Sh16 milioni ambayo waandaji walipeleka hivyo kufika kiwango cha Sh 361.6 milioni.


Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Mwenze Kabinda, alisema; “Bajeti yetu ilikuwa ni Sh16 milioni ndiyo tuliyopeleka kuomba kusaidiwa, lakini Azam wamechukua jukumu la kutudhamini kurusha mechi zetu zote na kusaidia fedha tulizoomba. Sisi tusingeweza kufanya hivyo kwani kiasi tulichoomba kilikuwa ni kwa ajili ya maandalizi mpaka tutakapomaliza.”


Katika ufunguzi wa mashindano hayo timu ya jiji la Dar es Salaam ambao ni wenyeji itaanza kampeni yake ya kusaka ubingwa huo kwa kucheza na Mombasa katika mechi ya ufunguzi, Mbeya na Kigali, Tanga na Adiss Ababa wakati upande wa wanawake, Dar es Salaam watacheza na Kampala mechi hizo zitachezwa kabla ya ufunguzi rasmi wa michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment