
Familia ya Oscar iko mahakamani kumuunga mkono
Mwanariadha anayekabiliwa na kesi ya mauaji nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius alikuwa na majuto baada ya kumuua mpenzi wake.
Hii ni kwa mujibu wa ushahidi wa jirani yake
huku kesi dhidi ya mwariadha huyo ikianza kusikilizwa tena baada ya
kuahirishwa kwa wiki mbili.Pistorius amekana madai kuwa alimuua mpenzi wake kwa maksudi.
Anasema kuwa alifyatua risasi kupitia mlango wa chooni wakati akiwa katika hali ya kuogopa akidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Bwana Stander alitaka kuonyesha kuwa Bwana Pistorius' alikuwa na majuto na uchungu mwingi kwa kumuua mpenzi wake na kwa hivyo huenda alimuua kwa bahati mbaya.
"Niliona ukweli asubuhi ile na ninahisi hivyo ndivyo ilivyokuwa,’’ Sanders aliambia mahakama."Alitaka sana kumuokoa na alichofanya tu ni kumuomba Mungu,’’ aliongeza kusema shahidi huyo.

Oscar Pistorius akiwa mahakamani
Alisema kuwa mwanariadha huyo alimwambia kwamba: ''Nimemuua Reeva nikidhani alikuwa jambazi kavamia nyumba yangu, tafadhali njoo haraka.’’
Bwana Stander alisema kuwa alipowasili nyumbani kwake Oscar alimuona mwanaridha huyo akishuka ngazi akiwa amembeba Reeva.
"Alikuwa analia, akipiga mayowe, akiomba Mungu,’’ alisema Stander naye akiwa analia.
‘‘Sidhani ni kitu ningependa kuona tena maishani mwangu,’’ alisema jirani huyo
Stander aliambia mahakama kuwa eneo hilo lilikuwa limewahi kuvamiwa , ingawa kwa ujumla wake ni mahali salama.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com tutakuwa tunakujuza kila kitakachokuwa kinaendelea kuhusiana na kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius
0 comments:
Post a Comment