Facebook

Friday, 23 May 2014

Kauli ya Wayne Rooney ikiwa Van Persie akiwa nahodha wa Man United

Tangu Nemanja Vidic alipotangaza rasmi kwamba msimu ujao hatokuwepo Old Trafford kulianza tetesi juu ya mchezaji gani atapewa nafasi ya kurithi mikoba ya unahodha ambapo Wayne Rooney mmoja wa wachezaji wakubwa ndani ya klabu ya Manchester United alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha mpya wa United wakati timu hiyo ikiwa chini ya David Moyes.
Baada ya kutimuliwa kwa kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Louis Van Gaal, mshambuliaji wa Uholanzi na nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi Robin van Persie amekuwa akipewa nafasi ya kumrithi Vidic, huku Van Gaal akisema kwamba yeye na RVP wana filosofia moja hivyo wanakuwa na urahisi wa kufanya kazi pamoja kama kocha na nahodha wake.
Hali hiyo imepelekea Wayne Rooney ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya unahodha msimu ujao kuzungumza akisema “navutiwa na suala la kuwa nahodha, nimeshawahi kuwa anahodha wa muda United kwa mara kadhaa na kupata jukumu hilo moja kwa moja litakuwa jambo zuri sana.”

Akizungumzia suala la Van Persie kupewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha ajaye wa United, Rooney anakwambia ikiwa kocha wetu atamchagua mtu mwingine basi kiukweli kabisa sitokuwa na tatizo na hilo, nitaheshimu maamuzi yake… Robin ni nahodha wa nchi yake, ameshawahi kuwa nahodha wa Arsenal na ikiwa atapata nafasi hiyo United basi naamini atafanya kazi nzuri.”

0 comments:

Post a Comment