Facebook

Friday, 23 May 2014

Mambo muhimu usiyoyajua kuhusu Atletico Madrid



Athletico Madrid imeonekana kuwa maarufu kwa baadhi ya wapenda soka hasa Tanzania katika siku za karibuni kutokana na kufanya vizuri kwenye la liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini hii timu ni bora tokea muda mrefu sana na pengine leo Utapata nafasi ya kufahamu vitu ambavyo huvifahamu kuhusu Athletico Madrid.
Timu Hii ilianzishwa mwaka 1903 Katika Jiji la madrid nchini Spain na ndo vinara wa Ligi kuu nchini humo kwa sasa ( La Liga) wakiwa na pointi 88 pointi 3 mbele ya Mabingwa Watetezi Barcelona wanaokamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 85.

JINA LA UTANI: (LOS INDIANS)


Los Indios (the indians) Hili ni jina ambalo wengi hupenda kulitumia na kimsingi kuna vitu vingi vilivyochangia kuitwa "Los Indios" ila kikubwa ni kutokana na kusajili wachezaj wengi kutoka bara la America ya kusini(red indians) ambapo miaka hiyo ya 70 chini ya rais kipenzi Vicente Calderon.


JEZI:


Kuhusu jezi zina historia ndefu sana hizi ambazo tunaziona zikivaliwa hivi sasa na Atletico Madrid, Kwa mara ya kwanza Atletico walikua wanavaa rangi ya bluu na nyeupe tangu ilipoanzishwa 1903 mpaka mwaka 1911 (miaka minane) baadae zilibadilishwa kutoka nyeupe na bluu kwenda nyeupe na nyekundu.

Haikua mipango ya Atletico kubadilisha jezi hizo ila kuna kosa lilifanyika wakati wa kuzinunua huko England ambapo zilikosekana zile zilizozoeleka za nyeupe na bluu na hivyo kuamua kununua nyekundu na nyeupe kutoka kwa Southmpton badala ya Blackburn baada ya kuzinunua huko southmpton na kubadilika kuwa nyekundu na nyeupe, wakaendelea nazo kwa kuwa kule spain malighafi ya hivyo vitambaa vya kutengenezea jezi hizo ilikuwa ni rahis sana yaani bei nafuu kwa kuwa baada ya kutengenezeaa macover ya mattress basi vinavyobaki vinatengenezewa jezi....!!hapo ndo ikawa mwanzo wa kutumia jezi hizi mnazoziona leo.



KIWANJA:

 Athletico Madrid ina uwanja wa kisasa kabisa pale Ulaya unaitwa ESTADIO VICENTE CALDERON, ni uwanja wa 6 kwa ukubwa nchini Spain  kwa England upande wa klabu basi ungeshika nafasi ya 3 kwa ukubwa nyuma ya Old Trafford (Manchester United) na Emirates ( Arsenal), Uwanja wa Atletico Madrid una uwezo wa kuingiza watazamaji waliokaa 54,960.

 Historia ya uwanja huu ni ya kipekee kutokana na jina lake VICENTE CALDERON , hili ni jina la rais wa zaman wa Athletico Madrid na ni mtu ayeheshimika kuliko wote pale Atletico Madrid kutokana na kukaa miaka mingi kwenye kiti cha urais wa klabu hiyo Huyu alidumu kama Raisi wa Klabu kwa miaka 16.
Atletico Madrid iko katika mipango ya kupata uwanja mpya huku ukitanuliwa uwanja wa ESTADIO LA PEINETA au kwa jina lingine ambalo ndio litatumiwa ESTADIO OLYMPICO DE MADRID, huu ndio utakuwa uwanja mpya wa Atletico Madrid kufikia mwaka 2016, kwa sasa ujenzi bado unaendelea na uta-replace uwanja wa VICENTE CALDERON.

Kwa sasa huu uwaja wa Estadio la Peineta unaingiza watazamaji 20,000 lakini kwa ukarabati na utanuzi unaoendelea ukikamilika utaingiza watazamaji wapatao 70,000, shukrani zimuendee msanifu wa uwanja huu yaani ARCHITECT anayeitwa ANTONIO ORTIZ GARCIA ambaye anamiliki kampuni ya usanifu iitwayo CRUZ Y ORTIZ ARCHITECTS, huyu jamaa amefanya kazi nyingi nzuri za usanifu majengo na viwanja, ana ofisi Sevilla Spain na kule Uholanzi, ni mmoja wa wasanifu wanaoaminika nchini Spain!!!

 
WACHEZAJI:


Linapokuja suala la wachezaji hapo ndipo ninapofurahishwa na club hii, ina mfumo mzuri sana wa kukuza wachezaji wenye vipaji tokea chini. Atletico Madrid haina kawaida ya kununua sana wachezaji wenye majina makubwa.

Falcao na Diego Costa
 

Ni timu ambayo unaweza kusema imebarikiwa sana kupata Washambuliaji bora na kwa miaka ya karibuni ndio imezidi kudhihirisha hilo;
Kutoka kwa Fernando Torres, Diego Forlan, Sergio Aguero,Radamel Falcao hadi sasa kwa huyu Diego Costa bado hatushikiki. Wachezaji wana vipaji, wana uwezo kama huamini nenda kaangalie mechi moja tuu alafu njoo uniambie ulichoona jinsi Koke,Gabi,Turan, Raul Garcia wanavyopishana pale kati. Swali: kuna kipa bora kwa sasa duniani zaid ya Thibaut Curtouis?????

MAKOCHA

Timu ilitoka kwa Ricardo Zamora miaka hiyo hadi leo kwa master Diego Simeone, wengi mnafikiri Diego Simeone kaizaa upya Atletico Madrid ila kuna huyu anaitwa QUIQUE FLORES, kama humjui tafuta historia yake na nini amekifanya kuanzia 2009 - 2011.
Diego Simeone
swali la pili: kuna kocha mwingine bora duniani zaid ya DIEGO SIMEONE?????

UONGOZI:

Asikudanganye mtu bana timu ni uongozi aisee na ndio kitu ambacho Atletico Madrid kimeifanya ifanikiwe kwani ukiangalia viongozi wote wana uadilifu wa hali ya juu na kwa budget ndogo ya klabu lakini inaleta tija kwa kupata wachezaj bora.
Hivi unajua Sergio Kun Aguero alinunuliwa bei gani??  Diego Costa je? au  Arda Turan??
Hapa ndipo rais wa klabu ENRIQUE CEREZO anapozidi kuwa juu na kupewa Sifa.


Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kusoma makala mbalimbali zinazohusiana na soka.

0 comments:

Post a Comment