Facebook

Monday 12 May 2014

NIFIKIRIAVYO:Yaya Toure na makombe yake, Hazard-Suarez na tuzo zao

Photo: CHAMPIONS 2014 #TOGETHER
Karne ya 6 kabla ya kuzaliwa Kristo Generali
wa China na mtaalamu wa mbinu za jeshini anayejulikana kama Sun
Tzu aliandika kitabu “the art of war” sehemu
ya maneno kwenye kitabu hicho muhimu
sana kwenye jeshi la Uchina wakati huo
yalisema “lose the battle win the war”
akimaanisha “shindwa mapigano ila shinda
vita”.
Nafikiri maneno ya Generali Sun Tzu
yanamfaa zaidi Jenérari Yaya Touré, kijana
toka Bouake pale Ivory Coast, akiwa na uzito
wa 90kg na urefu wa futi 6 ni mkubwa zaidi
ya anavyoonekana kwenye luninga, pale
Uingereza wanapenda kumwita “bulldozer”
yani yale magari tunayoyaona wachina
wakitumia kwenye kutengeneza barabara,
jamaa hasukumiki kirahisi, miguu yake
mirefu inamfanya awe na hatua kubwa
kwenye kukimbia lakini zaidi inamwezesha
kupiga mashuti atakavyo kwenye ligi ya
Uingereza.
Katika orodha ya wachezaji bora wa mwaka
kwenye ligi ya Uingereza Yaya Toure
aliangukia nafasi ya tatu nyuma ya Suarez na
Hazard, Luis Suarez akiibuka mshindi na Eden
Hazard kushinda tuzo ya mchezaji bora
mdogo pale Uingereza, kama ni mapigano
basi kwa Yaya Toure ktk tuzo hizi alishindwa
mapigano (lose the battle), hakuna tuzo
binafsi ambayo anaweza tena kushinda kwa
msimu huu zaidi ya zile zitakazotolewa na
timu yake ya Manchester City.
Yaya Toure huyu wa Manchester city si yule
wa Olympiacos, wala Monaco na wala
Barcelona, wachambuzi wa soka wanapenda
kumfananisha na aliyekuwa nahodha wa
Arsenal kijana toka Ufaransa Patrick Viera
huyu alikuwa kila kitu kwenye sehemu ya kati
kati ya uwanja kwa The Gunners, hasa kwenye
msimu wa 2003/2004 waliomaliza ligi bila
kufungwa. Lakini kwa Viera huyu mpya
Mungu amemwongezea kitu kimoja miguu ya
kufunga magoli, iwe kwa mipira ya adhabu
ama mashuti, huyu ndiye mchezaji ambaye ni
injini kwenye gari la Manuel Pellegrini pale
Manchester city kuelekea ubingwa.
Takwimu zinatuambia ana magoli 20 na
“assist” 8 mpaka sasa wakati ligi ya Uingereza
ikielekea kumalizika huku Manchester City
wakihitaji pointi moja tu kuweza kutangazwa
mabingwa, tayari Yaya kibindoni ana kombe
la Capital one akifunga goli bora kabisa
kwenye fainali dhidi ya Sunderland, huyu
ndiye mchezaji aliyekimbia kwa yadi 66
kwenye mechi dhidi ya Aston villa akiwaacha
mabeki wakigalagala chini kufunga goli na
kuisaidia Manchester city kuwa kileleni kwa
tofauti ya pointi mbili dhidi ya Liverpool na
kukaribia kunyanyua ubingwa wa EPL.
Vita ya Yaya Toure kwasasa ni kunyanyua
ndoo ya ubingwa wa ligi (win
The war), baada ya kushindwa kwenye
mapigano ya tuzo binafsi za wachezaji nafikiri
wakati ni wake sasa kushinda vita ya
kunyanyua ubingwa kwa mara ya pili pale
Manchester City hasa ktk kipindi hiki
ambacho yuko kwenye fomu ya kipekee sana
kama kiungo wa kati duniani, shukrani ziende
kwa Fernandinho mchezaji mwenzake pale
City anayeifanya kazi ya Toure iwe rahisi.
Nawaza tu hakuna ubishi kwamba Yaya Toure
amekuwa na ubora wa pekee kama kiungo wa
kati kwenye ligi ya Uingereza ila kama
anataka dunia imfahamu vizuri basi afanye
alichokifanya Drogba akiwa Chelsea, kufika
mbali kwenye mashindano ya UEFA
CHAMPIONS LEAGUE na hata kunyanyua
ndoo.
Photo: Proud to be the first player to reach 20 goals, I hope to score many more. I'd like to share it you all, my colleagues and all the Liverpool fans! Great match at Anfield Tomorrow! Thank you everyone.

Es un orgullo poder ser el primer jugador en llegar a los 20 goles, y espero que lleguen muchos más. Lo quería compartir con todos ustedes, mis compañeros y toda la gente del Liverpool!! Mañana gran partido en Anfield! Muchas gracias a todos.Photo: Hello everyone. First of all I wanted to thank all the fans for supporting me this year, especially the RED FANS. We did everything we could until the last game but the important thing this year was that Liverpool came back in the Champions League!!! Me and my family want to thank you for living unique moments this year. The work done by my teammates and the entire staff of Liverpool has been incredible and I hope everyone enjoyed this year... Thanks again. YNWA!!!!!!!!

Hola a todos. Primero que nada les quería agradecer a todos los hinchas por apoyarme en este año, especialmente a los RED FANS. Hicimos todo lo que pudimos hasta el último partido pero lo importante de todo este año fue que el Liverpool volviera a estar en la Champions!!!! Yo y mi familia les queremos agradecer por haber vivido momentos únicos este año. El trabajo que hicieron mis compañeros y todo el staff del Liverpool ha sido increible y espero que todos hayan disfrutado de este año... Muchas gracias otra vez. YNWA!!!!!!!!
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kusoma makala mbali mbali za michezo zilizo andaliwa na wachambuzi makini na wenye ujuzi na masuala ya michezo mbalimbali hususan Mpira wa miguu
Imeandaliwa na........
                                 Katemi Methsela (Blogger)
                                      (0785 442 107)

0 comments:

Post a Comment