
Shirikisho la soka duniani FIFA
limesema kuwa vilabu havitashurutishwa kuwaachilia wachezaji wao ili
washiriki mechi za kufuzu kwa michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika
mwaka 2015.
Hii ni kwa sababu tarehe ya kufanyika kwa michuano hiyo iko nje ya tariba ya shirikisho hilo ya michuano ya kimataifa.Mechi za taifa bingwa Afrika, shirikisho na kombe la klabu bingwa Ulaya itafanyika kati ya tarehe 16-17.
Mechi hizo hazipo kwenye ratiba ya FIFA na kwa hivyo haitakuwa lazima wachezaji wa vilabu kuruhusiwa kuondoka.
Hata hivyo, michuano ya makundi itakayoshirikisha Ghana, Nigeria na Cameroon, zitakuwa katika tarehe iliyoidhinishwa na FIFA , ikimaanisha kuwa vilabu vya soka kote duniani lazima viwaruhusu wachezaji wao kushiriki mechi hizo.
Wachezaji kama Edward Sadomba, wataathiriwa na mgongano wa tarehe zilizo kati ya mechi za kufuzu zitakazofanyika 2015 na michuano ya vilabu.
Sadomba atahitajika kwa wakati mmoja na klabu yake ya Al Ahli Benghazi pamoja na timu yake ya taifa Zimbabwe.
Ni hali sawa kwa mchezaji wa Zamalek kutoka Mauritania Dominque da Silva pamoja na mtanzania Mbwana Samatta, anayechezea TP Mazembe ya DR Congo.
Maafisa wa kombe la mashirikisho wamesema kuwa wataviandikia barua vilabu vyenye wasiwasi wakitaka wachezaji kuruhusiwa kuwakilisha nchi zao kwa sababu ya changamoto zinazotokana na ratiba.
Lakini FIFAimesema kuwa wachezaji wanaweza tu kuondoka ikiwa maafisa wa vilabu na mashirikisho ya nchi husika wanaweza kukubaliana.
0 comments:
Post a Comment