Facebook

Thursday 8 May 2014

Rio Ferdinand nae anakuja na kitabu chake, Moyes katajwa...........



article-2621486-1BDADBAE000005DC-542_634x470 

Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson akizua mijadala mingi kwenye vyombo vya habari kutokana na vitu alivyoandika kwenye kitabu chake – hivi sasa beki Rio Ferdinand ambaye anakaribia kuondoka ndani ya klabu ya Man United nae anajiandaa kutoa kitabu chake ambacho kinatajwa kitafunua yote ya nyuma ya pazia kuhusu utawala wa David Moyes.
Ferdinand, 35, anatarajiwa kuandika yote yanayohusiana na maisha yake ya soka kwenye kitabu ambacho kitapewa jina la ‘#2sides: Rio Ferdinand – My Autobiography.’
Kitabu chake kinatarajiwa kueleza kiundani msimu mbovu kuliko yote ndani ya klabu hiyo kufuatia kuondoka kwa kocha Alex Ferguson na timu kukabidhiwa kwa David Moyes ambaye alitimuliwa wiki kadhaa zilizopita – huku wachezaji wakubwa kama Ferdinand wakitajwa kuwa na mkono kwenye kutia mchanga kibarua cha Moyes.
Kitabu hicho kinatarajiwa kutoka October 2 na kinachapishwa na kampuni ya Blink Publishing.

0 comments:

Post a Comment