Facebook

Thursday 8 May 2014

Unaijua kauli ya Sauti Soul baada ya kupata taarifa ya kufungiwa kwa video yao........

TZA SAUTI SOL 
Ikiwa inakaribia wiki ya pili sasa tangu kundi la Sauti Soul kuachia video ambayo imeleta utata na baadae kutoka taarifa za kufungiwa,hatimae leo kuna kauli kutoka kwao kama Sauti Soul kuhusu hii video.
Miongoni mwa maoni ya watu kuhusu video hiyo ambayo bado imezua utata na hisia tofauti ni ile hali ya kuonyesha misuli iliyotajwa na mafans wa kike kama jambo la kufurahisha huku upande wa kiume wakisema kama inawadharirisha.
TZA SAUTI SOL2 
Kwa mujibu wa bendi nzima la Sauti Soul video ya Nishike ilitungwa tu kwa ajili ya kutuma ujumbe’Tuna pitisha ujumbe kwamba wanaume sharti wafanye mazoezi sio tu kupata sixpacks lakini kwa ajali ya afya yao’
‘Wengi wetu wamekua wanene kupita kiwango na njia ya pekee ya kupunguza unene huo nikupitia kufanya mazoezi kwenye gyme’.asema Delvin Mudig ambaye ni miongoni mwa waimbaji wanaounda Sauti Soul
Katika kauli nyingine Austin Chimano ambaye pia ni member wa Sauti Soul amesema’Hatukukiandaa video ya Nishike kukera mtu yeyote tunacheza na kuimba Kisauti Soul.tumekua sisi tu.hatukupanga kua na wimbo ulitakaozua hisia kama hizi Ilikua tu ni dhihirisho la penzi.hakukua na fumbo hapo’.
Naye Bien Aime Baraza ameongezea’kama bendi Sauti Soul sasa inawekwa kwenye kiwango sawa na bendi za hadhi ya juu kama P-Square, Mafikizolo,Mikasa na wengine tumekuwa kutoka wakati wa Lazizi na tungependa mafans wetu waendelee kutusapot kutuwezesha kuwa na kujulikana nje ya Bara la afrika’
Mwingine ni Polycarp Otieno ambaye yeye amesema’Sanaa inahusu kujieleza na kwetu haikua tu tutoe wimbo ambao watu wangeu skiza na kuridhika,lakini kitu ambacho kiingeonyesha hilo kwenye video,ndio tumepata maoni mabaya kutoka kwa wanaume,lakini tunawajibu kua ‘usimchukie mchezaji’, kwa kweli video inayotokea niya kuwahamazisha watu wafanye zoezi’.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari zilizo sahihi,makini, zenye mantiki na ukweli ndani yake

0 comments:

Post a Comment