Facebook

Saturday, 3 May 2014

Watoto saba wauawa kinyama Honduras


Polisi wa Honduras wa kupambana na mahadarati na magenge ya uhalifu
Serikali nchini Honduras inachunguza vifo vya watoto saba ambao huenda waliuawa baada ya kukataa kujiunga na magenge ya uhalifu katika mji wa viwanda wa San Pedro Sula.
Siku ya alhamisi ,Polisi walifanikiwa kupata mwili wa mtoto wa miaka saba ambaye mwili wake ulioneka kuwa alikuwa ameteswa kabla ya kuuawa.
Kaka ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 pia alikutwa amekufa siku kadhaa zilizopita.
Mwanasheria Mkuu nchini Honduras Oscar Chinchilla yupo katika mji huo ili kusimamia uchunguzi huo.
Taifa hilo la Honduras lina idadi kubwa ya matukio ya mauaji duniani ambapo inakadiriwa watu 15 wamekuwa wakiuawa kwa siku, takwimu hizo ni kwa mujibu ya mamlaka ya nchi hiyo.

Related Posts:

  • BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika magazeti yote ya leo Jumanne,Juni 2. MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu… Read More
  • Benki Kuu Nigeria yakumbwa na kashfa ya Ufisadi.Wakuu katika shrika la kupambana na rushwa nchini Nigeria wanasema maafisa kadhaa kutoka benki kuu ya nchi hiyo wamepelekwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi wa kiasi kikubwa cha fedha za thamani ya mamilioni ya dola. Pia baad… Read More
  • Watu zaidi ya 400 wazama na Meli China Meli ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali katika Mto Yangtze kusini mwaChina. Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa mpaka sasa na kazi inaendelea y… Read More
  • Lori la mafuta laua watu 70 Nigeria.Karibu watu 70 wamefariki huko mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto. Police wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali. Walioshuhudia wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti nd… Read More
  • Waandamana wakiwa Uchi Uganda.Wanawake katika kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka 10. Wakati wa maandamano hayo ,maw… Read More

0 comments:

Post a Comment