Polisi nchini Nigeria wamewataka wazazi wa wanafunzi wasichana zaidi ya 200 waliotekwa kuwasilisha picha za mabinti hao.
Wasichana hao walichukuliwa na watu wanaoshukiwa
kuwa wanamgambo wa Kiislam kutoka shuleni kwao katika jimbo la Borno
zaidi ya wiki mbili zilizopita.Maandamano yalifanyika siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi, ambayo ni mapumziko, waandamanaji wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kuwaokoa wanafunzi hao wa kike.
Kundi la Kiislam la Boko Haram halijatamka lolote kuhusiana na tuhuma zinazolikabili kuwa wapiganaji wake wamehusika na utekaji wa wanafunzi hao kutoka shuleni kwao katika mji wa Chibok usiku wa manane wa tarehe 14 Aprili 2014.
Kundi hilo, ambalo jina lake lina maana ya "Elimu ya mgaharibi ni haramu" katika lugha ya Kihausa, limekuwa likiendesha mashambulio mbalimbali kaskazini mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, huku watu 1,500 wakikadiriwa kuuawa katika ghasia hizo na msako wa vyombo vya usalama mwaka huu pekee.
0 comments:
Post a Comment