. Habari
zilieleza kuwa kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram, Wolper
amekuwa akitukanwa kila kukicha huku tetesi zikizagaa mtaani kwamba
mwanadada huyo ni msagaji. Matusi hayo yalikwenda mbele zaidi na kudai
kuwa kutokana na tabia yake ya usagaji ndiyo maana hataki kumweka
hadharani mwanaume wake.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi
iliyopita, Wolper alisema kuwa ni kweli amechoka lakini anawaachia
nafasi watu wanaomchafua kwenye mitandao na hatishiki kwa lolote kwani
maneno yao siyo ya kweli na kamwe hatamtangaza mpenzi wake kama
ilivyokuwa zamani.“Watukane sana, waseme mimi ni mwanaume lakini mimi
ninatambua ninachokifanya, wakichoka wataacha. Kamwe sipo tayari kumweka
mwanaume wangu kwenye vyombo vya habari, unajua kwenye mitandao kuna
uchonganishi mwingi sana na mtu usipokuwa makini utajikuta ukimchukia
mtu bila sababu kutokana na watu kuwa na mitazamo mbalimbali,” alisema
Wolper. |
0 comments:
Post a Comment