Facebook

Sunday 22 June 2014

Mwandishi wa habari auwawa Mogadishu


Mogadishu, Somalia
Mwandishi wa habari kijana wa Somalia ameuwawa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa chini ya gari lake mjini Mogadishu.
Yusuf Keynan alikufa wakati bomu hilo liliporipuka alipotia moto gari, akitaka kuelekea kazini.
Mwandishi  mmoja mjini Mogadishu anasema Yusuf Keynan (aliyefanya kazi katika redio Mustaqbal), alikuwa mwandishi wa habari kijana aliyekuwa akipendwa na hodari katika kazi yake.
Huyo ni mwandishi wa habari wa kwanza kuuwawa nchini Somalia mwaka huu, baada ya waandishi habari kadha kuuwawa kwa mfululizo katika miaka miwili iliyopita.
Shirika la Kuwalinda Waandishi wa Habari linasema kuwa Somalia ni moja kati ya nchi hatari kabisa kwa waandishi.
Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji ya kijana huyo.

0 comments:

Post a Comment