Facebook

Sunday 22 June 2014

Usalama waimarishwa Maracana.



Brazil wameahidi shirikisho la soka duniani FIFA kuwawataimarisha usalama katika viwanja vya kombe la dunia baada ya tukio ambalo mashabiki wa Chile walikamatwa wakijaribu kupenyeza ndani ya uwanja bila ya kulipia tiketi ilikushuhudia mechi baina ya Chile na Uhispania.
Hata hivyo ilikuwa dhiki wa dhiki kwao kwani walipenyeza na kuingia kwa sehemu iliyofungwa kwa ajili ya wanahabari.
Mechi baina ya Ubeljiji na Urusi ambayo imeratibiwa kuchezewa katika uwanja wa kihistoria wa Maracana ndiyo inayolengwa na wasimamizi wa FIFA.
Idadi ya maafisa wa Usalama watakaokuwa wakishika doria imeongezeka maradufu kutoka kwa maafisa 600 hadi 3,100.

Aidha kutakuwepo na wasaidizi 1,100 zaidi watakosaidia kudumisha utengamano katika mechi hiyo ya kundi H.
Mashabiki kadha pia wanaripotiwa kuruka uwa wa uwanja wa Beforelast ilikushuhudia mechi baina ya Argentina na Bosnia-Hercegovina.
Katibu wa FIFA anayeshughulikia maswala ya usalama , Ralf Mutschke, alikiri kuwa FIFA ilihuzunishwa na tukio hilo na kuwa itafanya kila iwezalo kuzuia aibu kama hiyo kurejelewa tena katika mechi zote zilizosalia.

0 comments:

Post a Comment