
Uwanja ambao umepangiwa michuano ya kombe la dunia 2022 Qatar
Waandalizi wa kombe la dunia
mwaka 2022 nchini Qatar wanatarajiwa kukutana na mchunguzi wa shirikisho
la soka duniani FIFA, Michael Garcia hii leo huku kukiwepo wito kwa
taifa hilo kunyimwa haki ya kuandaa mashindano hayo.
Jumapili, gazeti la SUNDAY TIMES la Uingereza,
liliripoti kwamba mamilioni ya pauni zilitolewa kama malipo kwa maafisa
waliounga mkono ombi la Qatar kuandaa michuano hiyo mwaka 2022, tuhuma
ambazo Qatar imepinga vikali.
Bin Hammam afisa wa soka Qatar ndiye anadaiwa kuwalipa hongo maafisa wa FIFA
Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa FA Mark Palios, anadhani kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter anajitahidi kulinda kazi yake.
Garcia anatarajiwa kukutana na maafisa wa FIFA nchini Qatar. Wakili huyo anachunguza madai mengine ya tuhumza dhidi ya maafisa wa FIFA kuhusiana na kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
Jarida la Sunday Times, linadai kuwa maafisa wa soka walipokea hongo ya kima cha pauni milioni 3 ili waweze kuunga mkono azma ya Qatar kutaka kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi
0 comments:
Post a Comment