Facebook

Sunday, 17 May 2015

BantuTz SPORTS:UCHAMBUZI MECHI KALI ZA LEO LIGI KUU UINGEREZA (EPL) NA HISPANIA (LA LIGA).

MANCHESTER vs ARSENAL 18:00
 
       Hatua ya kwanza ngoja tuipige pale machinjioni nazungumzia Old Trafford ambapo vijana Van Gaal walio na historia nzuri mbele ya wageni wao Arsenal watakwenda kukipiga.

    Ugumu wa mchezo huu ni kutokana na historia nzuri ya United kwani kwenye michezo saba ya hivi karibuni ligi kuu wameibuka na ushindi michezo sita na kutoshana sare moja kwa namna hiyo kwa mujibu wa hiyo takwimu Asenal wana nafasi ndogo ya kuibuka na ushindi siku ya leo.

     Vijana wa Mzee Wenger mara ya mwisho kuibuka na ushindi hapo machinjioni ilikuwa ni mwezi wa tisa msimu wa 2006 na katika chagizo la michezo mitano hali ni mbaya kwa Arsenal kwani waliruhusu jumla ya magoli 14 na upande wao kufunga magoli 4 pekee.

   Hapa tunazungumzia ligi kuu pekee maana unaweza jiuliza kulikoni mbona hivi majuzi kombe la FA tuliwashinda 2-1 pale Old Trafford nadhani umenielewa ukiachilia mbali hilo kingine ni Manchester kutokuruhusu kufungwa goli zaidi moja na kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal mara ya mwisho ilikuwa enzi hizoo 1979.

   Hii ngoma nzito kweli ambayo kwa kuangazia haina umuhimu kuchezeka leo isipo kuwa kwa kuwa ni maarufu basi watu washajifunga vibwebwe kuicheza Chelsea msimu wa 2004/05, Spurs msimu wa 1988/90 na Aston Villa msimu wa 1919/20 hapa enzi hizo tulikuwa tunatawaliwa na wakoloni hiyo miaka na hizo timu ndo pekee kuzifunga Manchester mara mbili ndani ya msimu mmoja hivyo Mzee Wenger nafasi ni yake kuiandika historia kwa timu yake.

  Katika michezo sita ya ligi kuu matokeo yapo hivi

     MANCHESTER- WWLLLW
      ARSENAL- WWWDWL

   Kwa kuangazia takwimu hiyo inaonyesha kuimalika kwa Arsenal kuliko Manchester mchezo wa mwisho Arsenal kupoteza dhidi ya Swansea ilikuwa ni baada ya miezi 3 timu zote zina umiliki mzuri wa mpira na ni miongoni mwa burudani nzuri siku ya leo.

   Manchester wapo nafasi ya 4 wakiwa na pointi 68 wakati wana wa London wapo nafasi ya 3 kwa pointi 70 hivyo vita vilivyopo ni kuwania nafasi ya 3 na ya 2 ilikufudhu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi kombe la mabingwa Ulaya kuliko kuanzia mchangani pindi timu ikishika nafasi ya 4.

   Upande wa nidhamu ndani ya uwanja mashetani wana jumla ya kadi za manjano 63 na nyekundu 4 vijana wa Wenger wana kadi za njano 67 huku wakiwa na kadi nyekundu 2.

     Ukiachilia mbali majeraha ya baadhi wachezaji ya muda mrefu wachezaji watakao mchezo huu upande wa wenyeji ni mlinzi Shaw na nahodha Rooney ambae ukizungumzia timu tatu alizo zifunga mara nyingi ligi kuu Arsenal ni miongoni ( Aston Villa-13,Newcastle-12, Arsenal -11) upande wa Wenger huenda Welbeck aka kosekana na kama unakumbuka mchezo wa FA ndie alikuwa mwiba wa mwisho kuichoma Manchester.

KONA KALI::

    Ni mchezo mgumu hilo lipo wazi kulingana na historia mbinu nzuri ya United ni mashambulizi ya spidi kwa kupita pembeni niki maanisha mipira mirefu hasa kwa kuwatumia mawinga wake ila kwa undani wa vikosi vyote vitakavyo anza Arsenal ana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi na United nafasi yao kubwa ni sare.
      Haina maana kuingazia Manchester matokeo mabaya ila uwezo wa timu zote kwa hivi karibuni kuna utofauti mkubwa bado United ni tiamaji-tiamaji endesha liende na michezo mingi wamekuwa na uchezaji mzuri pasipo huitaji wa pointi tatu kwa maangazio ya jinsi mchezo wanavyo ucheza.

--------
ATLETICO MADRID vs BARCELONA 20:00

      Najua asilimia kubwa homa ipo Old trafford ila pale viunga vya Vincente Calderon wana wa Diego Simeone walio nafasi ya tatu pointi (77) watahitaji matokeo mazuri kulinda vyema nafasi hiyo kwa Valencia wanao nyemelea wakiwa na pointi (73).

    Mawindo yao watayafanya kwa vijana wa Luis Enrique Barcelona ambao wao shabaha yao ni kukwepa windo la Athlètic Madrid ili kuvuka pori na kwenda kwenye nyumba pekee upande wa pili wa pori ambapo ndipo kuna Ubingwa wa La-liga.

  
Blaugrana hitaji lao ni pointi tatu ambazo zitawapelekea kufikisha pointi 93 ambazo hazitoweza kufikiwa na wapinzani wao Real Madrid walio nafasi ya pili kwa pointi 86 na michezo iliyobaki ni miwili ya ligi ya siku ya leo na juma lijalo hivyo hata Real Madrid wakishinda michezo miwili hiyo watakuwa na pointi 92.

     Msimu wa 1995/96 Atlètico Madrid walichukua ubingwa wao wa 9 wa ligi ilichukua muda mpaka msimu wa 2013/14 kutwaa ubingwa wao wa 10 na ngoma ilinoga kwenye viunga vya Catalunya kwani walihitaji sare kuutwaa wakati huo wana wa Catalunya Barcelona walihitaji ushindi ili kutetea ubingwa wao kwani walikuwa wamechukua msimu wa 2012/13 Sanchez aka anza kuangazia mwangaza wa kutetea ubingwa ila mwana wa Roberto kutoka kule Rosario,Argentina Diego Godin akawaduwaza mashabiki wa Barcelona kwa kusawazisha goli na kuipa Athletic Madrid ubingwa.

   MSN kombinenga itakuwa haija kamilika kwani Suarez anamajeraha hivyo hatocheza mtanange huu Pedro anatarajiwa kuchukua nafasi na upande wa wenyeji Tiago atakosekana hivyo Mario Suarez huenda akachukua nafasi yake.

      Michezo tisa hivi karibuni Barcelona bado ni wababe kwa Simeone kwani wameshinda michezo 7 na kutoshana sare mara 2 kikubwa pia ni safu ya ulinzi ya Barca ambayo haija ruhusu goli kwenye michezo mitano huku safu ya ushambuliaji ikifunga magoli 20.

KONA KALI::

    Kuna kijana Griezmann ambae hazungumzwi sana ila jua mpaka sasa ndo kinara wa magoli pale Athlètic Madrid akiwa na magoli 22 ni mingoni mwa silaha tegemezi kwa Simeone hivyo kina Pique watakuwa na kazi ya ziada.
     Uwepo wa Torres kwenye mchezo kama huu ni muhimu kuliko kwa Mandzukiç kwa maana ni straika alie na vitu vya ziada Mara nyingi presha imekuwa ya kawaida kwa vijana wa Simeone mbele ya Barcelona kuliko na Real Madrid.

    KONA kali nafasi anayo Barcelona kuibuka na ushindi kwa takwimu nzuri kupata matokeo njia pekee kwa Simeone ni utulivu pasipo rafu za ovyo na kushambulia kwa spidi.

    Je! Windo la Simeone litafanikwa kuwazuia Barcelona kuchukua ubingwa wao wa 23 La-Liga.


For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment