Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, 12 March 2016

UVUMILIVU UMEMSHINDA MANARA, AJA NA TAKWIMU NANI ANASTAHILI KUITWA WA KIMATAIFA.

Haji Manara-Afisa habari Simba SC
Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi, kuna neno wa ‘kimataifa’ hulisikia likiimbwa.
Waimbaji wakuu wa neno hilo ni mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.
Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa ‘mchangani’ au wa ‘matopeni’. Wengi wananilaumu kuwa kwa nini huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa Yanga. Jibu langu ni jepesi tu, lazima tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.
Mimi hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni. Haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki ‘maandazi’.
Kwa hiyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni. Mara zote nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo.
Wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halafu zifananisheni na timu nyingine nchini.
Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya. Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii katak kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.
Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.
Simba ndiyo timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyewe na hili lilizinduliwa 1971.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.
Simba klabu ya kwanza nchini kwenda Ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika Mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.
Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na Kati, ndiyo timu iliyochukua ubingwa mara nyingi kuliko klabu yeyote Afrika Mashariki na Kati (Champs off all time.)
Simba ndiyo timu pekee nchini iliyowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na hii ilikuwa1974.
Simba ndiyo timu pekee nchini na Afrika Mashariki kufika fainali ya kombe la Caf na hii ilikuwa1993.
Simba ndio timu inayoshikilia rekodi Afrika kama si duniani kwa kufungwa na Mufurila Wonderers ya Zambia magoli 4-0 na kwenda kuibamiza 5-0 kwao, mbele ya rais wao Kenneth Kaunda. Hii haijafanywa na klabu yeyote Afrika na nina mashaka duniani, hii ilikuwa 1979.
Simba ilicheza katik hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.
Simba ndiyo timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwa Afrika nadi Zamalek hii ilikuwa pia 2003.
Simba ndiyo klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu kuanzia
Waliowatoa mwaka jana Etoile du Sahel (Tunisia)
Widad Casablanca (Morocco)
El Setif (Algeria)
El Harach (Algeria)
halaf tumezifunga timu zote kubwa za Misri Zamelek,Al Ahly, Arab Contractors, Ismailia, Mehala, Al kubra na timu nyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.
Pia imeshaitoa El Merekh ya Sudan 1994 katak klabu bingwa ya Afrika. Simba pia imeshazifunga miamba ya Afrika Magharibi kuanzia Asec, Asante Kotoko, Hafia ya Guinea hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia Nkana Red Devils.
Tukirudi juu Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.
Simba ndiyo klabu pekee nchini kujenga jengo lake yenyewe kwa nguvu za wanachama na mashabiki, wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee Karume100%, Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.
Angalia idadi ya wachezaji wa Simba walioenda Ulaya kucheza soka la kulipwa.
Nico Njohole
Deo Njohole
Kassim Matitu
George Kulagwa
Huku ikiwa na makumi ya nyota wake kadhaa waliowahI kutapakaa sehemu mbalimbali duniani.
Nikutajie wachache.
Khalid Abeid
Haidar Abeid
Martin Kikwa
Athman Mambosasa
Zamoyoni Mogella
Hamis Gaga
Lilla Shomari
Iddi Pazi
Kiwelu Mussa
George Masatu
Hussein masha na wengine wengi.bila kumsahau nguli wa sasa mbwana samata.mutoto ya msimbazi.
Na hapa kumbukumbu zikae vizuri wazee wangu mimi, Sunday na Kassim Manara wakati wanaenda kucheza Ulaya hawakuwa wachezaji wa Yanga, walikuwa wakicheza Pan African.
Nimalizie kwa kuwaambia FIFA ilizitaja timu bora za karne kwa kila nchi kwa Tanzania Simba ilitajwa ndio timu bora ya karne na wenye mpira wao FIFA. Nenda kwenye rekodi za Caf ndio utajua nani wa kimataifa baina ya cc na wao.
Porojo za mjini ntakuwa nimezimaliza sasa na anayebisha abishe kwa data. Wakoloni wetu walitufundisha hivi…No reaserch no data no right to speak.Tafsiri isiyo rasmi, hujafanya utafiti na huna takwimu funga bakuli lako.
Asanteni na nendeni mkawaambie.
Haji S Manara
Msemaji wa klabu bora ya muda wote Tanzania (best club of all time)
Ukiona errors zipotezee jadili issues na nnaruhusu challenges kama zipo
Porojo peleka kuleeeeeee..
Nini maoni yako

Friday, 11 March 2016

Hawa ndio Mawaziri wa Rais Dkt Magufuli waliopewa kibali cha kusafiri Nje ya Nchi.

Rais John Magufuli ametoa kibali kwa Mawaziri wawili kusafiri nje ya nchi, wameruhusiwa kwenda nchini Vietnam kujifunza mbinu za kuinua kilimo na kujenga viwanda

-Mawaziri wawili waliopata kibali hicho ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba.

Saturday, 6 February 2016

Ratiba ya Soka katika ligi mbalimbali barani Ulaya Leo Jumamosi.

RATIBA YA SOKA LEO JUMAMOSI 06/02/2016
★Barclays Premier League
3:45 PM - Manchester City vs Leicester City
6:00 PM - Aston Villa vs Norwich City
6:00 PM - Liverpool vs Sunderland
6:00 PM - Newcastle United vs West Bromwich Albion
6:00 PM - Stoke City vs Everton
6:00 PM - Swansea City vs Crystal Palace
6:00 PM - Tottenham Hotspur vs Watford
8:30 PM - Southampton vs West Ham United

★Spanish Primera División
6:00 PM - Atletico Madrid vs Eibar
8:15 PM - Rayo Vallecano vs Las Palmas
10:30 PM - Athletic Bilbao vs Villarreal
07/02/2016
12:05 AM - Sporting Gijon vs Deportivo La Coruña

★German Bundesliga
5:30 PM - Eintracht Frankfurt vs VfB Stuttgart
5:30 PM - FC Ingolstadt 04 vs FC Augsburg
5:30 PM - Hannover 96 vs Mainz
5:30 PM - Hertha Berlin vs Borussia Dortmund
5:30 PM - Schalke 04 vs VfL Wolfsburg
8:30 PM - Bayer Leverkusen vs Bayern Munich

★Italian Serie A
8:00 PM - Bologna vs Fiorentina
10:45 PM - Genoa vs Lazio

★French Ligue 1
4:00 PM - AS Monaco vs Nice
7:00 PM - Angers vs Lyon
10:00 PM - Bastia vs Troyes
10:00 PM - Caen vs Stade de Reims
10:00 PM - GFC Ajaccio vs Guingamp
10:00 PM - Lorient vs Montpellier
10:00 PM - Toulouse vs Nantes

~Abel Alvaro

Rosicky Nje miezi mitatu.

Kiungo wa kati wa kilabu ya Arsenal Tomas Rosicky hatochezea timu yake kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na jeraha.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye kandarasi yake inakamilika katika msimu wa joto,alipata jeraha jingine la paja wakati wa mechi dhidi ya Burnley siku ya jumamosi baada ya kipindi cha miezi saba akiuguza jereha.Mchezaji huyo wa taifa la Czech alijiunga na Arsenal mnamo mwezi Mei mwaka 2006.

Alipoulizwa iwapo Rosicky ameichezea Arsenal mechi yake ya mwisho,Wenger alijibu:Natumai hapana ,lakini jeraha hilo ni baya sana.Rosicky ambaye aliichezea Arsenal mara 246 alisaini mkataba wa mwaka mmoja msimu uliopita.

Wakati huohuo,Wenger amethibitisha kwamba mshambuliaji Danny Welbeck atarudi kuwachezea wachezaji wa Arsenal wasiozidi umri wa miaka 21 siku ya ijumaa.Mchezaji huyo wa Uingereza,mwenye umri wa miaka 25,ameuguza jereha tangu mwezi Aprili 2015 baada ya kupata jeraha hilo katika mechi iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Chelsea.

Friday, 5 February 2016

Hili ndilo Baraza la Mawaziri Vivuli lilikotajwa leo bungeni.

BARAZA KIVULI LA MAWAZIRI

1.Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na
Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano
na Mazingira
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana,
Ajira na Walemavu
Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla

4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Magdalena Sakaaya
Naibu Waziri – Emmaculate Swari

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha

6.Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde

7.Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche

8.Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri – Tundu Lissu
Naibu Waziri Abdalla Mtolela

9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal

10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara

11.Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla

12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.
Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso

13.Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso

14.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe

15.Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph

16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto
Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul

17.Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja

18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Hamidu Hassan
Naibu Waziri– Peter Lijualikali.

Tuesday, 2 February 2016

Kiungo wa Manchester United ajiunga na Hull City.

Kiungo wa Klabu ya Manchester United,Nick Powell amejiunga na klabu ya Hull City baada ya kukosa nafasi katika klabu hiyo na atakuwa Hull City kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu kumalizika.

Manchester United,Arsenal zatuma ofa kwa Mshambuliaji wa PSG.

Vilabu vya Arsenal na Manchester United vyote vinashiriki ligi kuu nchini Uingereza vimeripotiwa kuangalia uwezekano wa kumsajili Mshambuliaji hatari Edison Cavan ambaye hana furaha katika klabu ya PSG ya nchini Ufaransa.

Mshambuliaji huyo ambaye anapendelea zaidi kucheza nafasi ya ushambuliaji hana furaha katika klabu ya PSG kutokana na kuchezeshwa sehemu ambayo haifurahi,Cavani anapatikana kwa £55m endelea kutembelea www.bantuz.com na kwa taarifa za usajili kwa wakati na muda muafaka like na tembelea page yetu facebook :--> http://www.facebook.com/bantuzfanspage

Monday, 1 February 2016

Beki wa Arsenal asajiliwa rasmi Bordeaux.

Klabu ya Arsenal imethibitisha mlinzi wake wa pembeni Mathieu Debuchy amejiunga na klabu ya Bordeaux kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Huku taarifa za awali zinasema;Klabu ya Manchester United ilikuwa imetuma maombi kwa klabu ya Arsenal kuhitaji kuhitaji huduma ya mlinzi huyo lakini kocha wa Arsenal ameamua kukubali ofa ya klabu ya Bordeaux.

-www.bantuz.com

VALENCIA YANASA KIFAA KUTOKA REAL MADRID

Klabu ya Valencia inayonolewa na Muingereza,lijendari wa Manchester United Garry Neville imethibitisha kumnasa winga mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid; Denis Cheryshev kwa mkopo wa miezi sita.

-Bantu Sources.

Radamel Falcao kurejea Atlético Madrid.

Mshambuliaji wa Chelsea mwenye asili ya Colombia Radamel Falcao muda huu anasafiri kuelekea Spain kufanya makubaliano na Klabu yake ya zamani Atlético Madrid ili kuhamia katika Klabu hiyo.

Dili hilo likitarajiwa kukamilika kabla dirisha la usajili halijafungwa.Endelea kutembelea www.bantuz.com kwa taarifa zote za usajili.

NEWCASTLE UNITED YAPELEKA DAU KWA BERAHINO.

Klabu ya Newcastle United ambayo inaonekana kufanya usajili wa kutisha katika dirisha hili muda huu imetuma maombi na dau la £24ml katika klabu ya West Brom kumsajili mshambuliaji hatari Saido Berahino.

-Bantu Sources.

MAN UNITED YARUSHA 'NDOANO' KWA IGHALO.

Klabu ya Manchester United imewasilisha maombi kwa klabu ya Watford kumsajili mshambuliaji wao hatari Odion Ighalo kabla dirisha la Usajili halijafungwa.

-Bantu Sources.

Bayern Munich yamsajili Serdar Tasci kutoka Spartak Moscow

Klabu ya Bayern Munich imemsajili Serdar Tasci kutoka klabu ya Spartak Moscow inayoshiriki ligi Kuu nchini Urusi kwa mkopo uliogharimu €2.5m kukiwa na kipengele cha kumnunua jumla kwa €10m.

-Bantu Sources

Klabu ya Hannover 96 yanasa kifaa kutoka Besiktas.

Klabu ya Hannover 96 inayoshriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) imethibitisha kumsajili Alexander Milošević kwa mkopo kutoka Besiktas huku katika mkataba kuna kipengele cha kumnunua mkataba utakapomalizika.

-Bantu Sources.

Sunday, 31 January 2016

ARSENE WENGER AWANASA MAKINDA WAWILI KUTOKA NIGERIA.

Klabu ya Arsenal iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa wachezaji wawili kutokea nchini Nigeria, Kelechi Nwakali na Samuel Chukwueze ambao walipelekwa katika Jiji la London na mchezaji lijendari wa Klabu ya Arsenal,Nwanko Kanu na kukutana na bosi wa Klabu hiyo Mzee Arsene Wenger

- www.bantuz.com

Saturday, 30 January 2016

Chelsea yakamilisha usajili wa beki 'kisiki' kutoka Marekani.

Klabu ya Chelsea imethibitisha kunasa saini ya beki wa kati Matt Miazga kutoka klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Marekani. Matt Miazga amesaini mkataba wa miaka minne na nusu huku ada ya uhamisho ikiwa haijawekwa wazi.

Huu ni usajili wa pili katika Klabu ya Chelsea mara baada ya hapo jana kufanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Alexandre Pato.

Endelea kutembelea www.bantuz.com kwa taarifa mbalimbali za usajili barani Ulaya.

Friday, 29 January 2016

Mbwana Samatta asajiliwa rasmi na klabu ya KRC GENK ya nchini Ubelgiji.

Mshambuliaji hatari Mbwana Ally Samatta 'Popa' ambaye aliibuka mfungaji bora katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kisha kujinyakulia Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Afrika.Amekamilisha usajili wake akitokea klabu ya TP Mazembe ya nchinI DR Congo.

Dili la Sammata kujiunga na miamba ya soka ya Nchini Ubelgiji,KRC Genk limekamilika mara baada ya mmiliki wa klabu ya TP Mazembe hapo juzi kumruhusu Sammata kijiunga na klabu hiyo.

Sammata amesaini mkataba wa miaka 4 itakayomfanya kukipiga katika klabu hiyo mpaka 2020 huku akikabidhiwa jezi namba 77.

Klabu ya KRC Genk kupitia website yake na ukurasa wake wa twitter wamedhibitisha dili hili kukamilika na kuanzia hivi sasa Sammata atakuwa mchezaji halali wa Klabu ya KRC Genk na kufungua njia kwa wachezaji wengine kwenda kukipiga huko barani Ulaya.

Tuesday, 26 January 2016

Tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya Leo Jumanne,26.

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, alikuwa tayari kujiuzulu siku ya Jumamosi baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Southampton, lakini akabembelezwa asifanye hivyo na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward (Sun),

Van Gaal ambaye amekwenda Uholanzi kwenye sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwa binti yake, ataendelea na mazungumzo na Ed Woodward siku ya Jumanne atakaporejea (Guardian),

Ed Woodward amezungumza na wachezaji kadhaa, pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu Old Trafford kuhusu Van Gaal (Sky Sports),

Hata hivyo Ed Woodward yuko tayari kwenda kinyume na mtazamo wa mashabiki wengi na kuamua kumuacha Van Gaal aendelee kusalia Old Trafford (Mirror),

Mwandishi wa habari Miguel Delaney amesema Manchester United wanafahamu kuwa Jose Mourinho anataka kumrithi Van Gaal na kuwa mazungumzo kati ya wawakilishi wake na United yamekuwa yakiendelea kwa muda (BBC Radio 5 live),

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 26, ameogopa kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 100 kutokana na hali ya mashaka iliyopo sasa kuhusiana na Van Gaal (Independent),

Winga wa Tottenham Andros Townsend, 24, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Newcastle, baada ya timu hizo mbili kukubaliana ada ya uhamisho (Guardian),

Totteham wana wasiwasi kuwa huenda beki Jan Vertonghen, 28, aliumia zaidi goti lake na huenda asicheze msimu wote uliosalia (Sun),

Newcastle watapanda dau jingine kutaka kumsajili Alexandre Lacazette, 24, kutoka Lyon, baada ya mchezaji huyo kusema hataki kwenda Newcastle (Telegraph),

Liverpool wamegonga mwamba katika dau lao la pauni milioni 28 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Alex Teixeira, ambaye amepachika mabao 22 katika mechi 15 msimu huu (Mail),

West Brom wanataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, anayechezea AC Milan kwa mkopo (Express & Star),

Matumaini ya Newcastle kumsajili Loic Remy, 28, kutoka Chelsea yatategemea na kukamilika kwa usajili wa Alexandre Pato kutoka Corinthians kwenda darajani (Chronicle),

Sunderland kwa mara nyingine tena wamehusishwa na mshamuliaji kutoka Ivory Coast, Seydou Doumbia, 28, anayecheza Roma na ambaye inadaiwa amekataa mkataba wa fedha nyingi kwenda China (Sunderland Echo),

West Ham wamekubaliana na mshambuliaji kutoka Nigeria Emmanuel Emenike, 28, lakini bado hawajaafikiana na klabu yake Fernabahce, na Al Ain ya Imarati anapocheza kwa mkopo (Evening Standard),

Watford wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fiorentina Mario Suarez, 28 (Watford Observer).

Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye baadhi ya magazeti ya Ulaya. Zimealia siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Endelea kutembelea www.bantuz.com kwa taarifa mbalimbali.

TAKUKURU: Kesi ya Ukwepaji Kodi ya LAKE OIL mtuhumiwa amepewa miezi miwili kurejesha Kwa umma Bilioni 8.5!

TAKUKURU: Kesi ya Ukwepaji Kodi ya LAKE OIL mtuhumiwa amepewa miezi miwili kurejesha Kwa umma Bilioni 8.5!

KLABU YA MARSEILLE YAPELEKA OFA KWA MBWANA SAMATTA.

Klabu ya Olympique Marseille inayoshiriki Ligi kuu Nchini Ufarasansa (Ligue 1) imeripotiwa kupeleka ofa kwa klabu ya TP Mazembe kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji hatari Mbwana Samatta ambaye alinyakua tuzo mchezaji bora wa ndani wa Afrika mwezi uliopita.

Katika hali ya sintofahamu iliripotiwa Samatta kusaini mkataba wa awali na klabu ya Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji na utata uliojitojeza ni Klabu ya TP Mazembe kuweka vipengele vigumu kwa klabu ya Genk katika makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo hali iliyopelekea dili la Samatta aliyebakiza muda wa miezi miwili katika mkataba wake kushindikana.

Hapo awali klabu nyingine ya Ufaransa ya Nantes ilituma maombi ya kumsajili Samatta dili likashindikana lakini hivi sasa Kama dili ka Genk halitokamilika Samatta anapendelea kwenda Kusini mwa Ufaransa kujiunga na miamba ya soka nchini humo Klabu ya Marseille.

Endelea kutembelea www.bantuz.com kupata habari za kina na uhakika.

Wema,Idris watarajia kupata mtoto.Waamua kuweka uhusiano wao wazi.

Kulingana na ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother Idris Sultan,Wema sio tu eti keshapata mchumba ila pia ashapata uja uzito!

Muigizaji huyo maarafu wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu aligonga vichwa vya habari kote kanda ya Afrika Mashariki na Kati walipokosana na mwimbaji huyo nguli Diamond raia wa Tanzania.

Wema alijieleza kuwa amepigwa teke na mwimbaji huyo wa ''Mdogo mdogo'' na ''Number One'' kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kupata mimba.

Idris, ambaye alikuwa amehusishwa na mlimbwende huyo kwa muda mrefu alikuwa akibubujikwa na penzi katika taarifa hiyo yake kwenye Instagram.

''Mimi nawe sio wa kawaida. Nala, natembea, nalala, nazungumza nikikuwazia wewe tu.''

''Na kama utadhani kuwa umebahatika kuwa nami, pia mimi naona nimebahatika kuwa nawe.''

''At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama.''

“Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike”.

''Au ukiingia jikoni kwangu na unapika na kuniandalia chakula kizuri,” aliandika Idris.

“Nitafanya kila niwezalo ilimradi ufurahi.''Nitakulinda, nikupende, nikutendekeze, tupike nawe, tujiburudishe kwa pamoja na kujivinjari; kwa hakika wewe ndiye uliyekonga moyo wangu''.''Wewe ndiye mke wangu''

Mchumba wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum amepata mtoto na bi. Zari kutoka Uganda ambaye ni mpinzani mkubwa wa Wema.

Idris na Wema watakumbukwa kwa kuanda matangazo ya kibiashara kama ''mume na mkewe'' Wema kwa upande wake alimsifu Idris kwa ucheshi wake hata mara nyengine akiachilia picha zake kwenye mtandao wake wa Instagram na kumtambua kama ''mpenzi''

Wema alitofautiana na Diamond Platinumz na akakurubiana na mwakilishi mwengine wa Big Brother Luis Munana raia wa Namibia.

Ramires kutimkia China.

Kiungo wa kimataifa wa Brazil na klabu ya soka Chelsea Ramires Santos do Nascimento anakaribia kujiunga na timu ya Jiangsu Suning ya China.Kiungo huyu mwenye miaka 28 alisajiliwa na Chelsea toka Benfica, mwaka 2010 kwa pauni la pauni milion 17 na inatarajiwa timu hiyo inayocheza ligi kuu ya china iko tayari kutoa dau la pauni million 25 kumnasa nyota huyo.

Ramires, alisaini mkataba mpya wa miaka minne mwezi Octoba,mwaka jana, ila ameanza kikosi cha kwanza kwenye michezo saba tu msimu huu wa ligi ya England.Timu ya Jiangsu ilimaliza katika nafasi ya nane kwenye msimu wa mwaka 2015, na kikosi hicho kinanolewa na nyota wa zamani wa Chelsea Dan Petrescu.

Kiungo huyu wa kibrazil akiwa na The Blues, ametwaa ubingwa wa ligi, kombe la Fa,kombe la ligi , ubingwa wa klabu bingwa ulaya na ile michuano ya Europa ligi.

Rais wa Russia,Vladmir Putin atuhumiwa na Marekani 'kula Rushwa'

Wizara ya Fedha ya Marekani imesema kuwa rais wa Urusi Vladmir Putini anakula rushwa.Tayari serikali ya Marekani imeshawawekea vikwazo wasaidizi wa rais Putin na inaonekana ni mara ya kwanza kwa kumhusisha moja kwa moja rais huyo na rushwa.

Msemaji wa wa rais huyo Urusi amesema kuwa hakuna maswali jambo lolote linapaswa kujibiwa kwa sababu ni wa kutunga.Tuhuma hizi zinakuja siku chache ambapo hivi majuzi tume ya uchunguzi ya Uingereza iliyokuwa ikichunguza mauaji ya jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinesko lilimtuhumu pia Putin kuwa huenda alitoa amri ya kuuawa kwa jasusi huyo.

Litvinenko aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya usalama ya urusi aliuawa kwa sumu ya polonium mjini London mwaka 2006.Adam Szubin anayesimamia vikwazo vya Wizara ya fedha vya Marekani amekiambia kipindi cha Panorama cha BBC kuwa rais wa Urusi ni mla rushwa na hilo lilifahamamika na serikali ya Marekani miaka mingi iliyopita.

"Tumemwona akiwaneemesha marafiki zake na watu wake wa karibu na kuwakandamiza wale ambao sio marafiki wake kwa kutumia rasilimali za taifa kama utajiri wa nishati au mikataba baina yao na serikali amekuwa akitoa maagizo iwanufaishe wale ambao anaamini watamnufaisha na kuwatenga wale wasiomnufaisha. Kwangu mimi hiyo hiyo ni sura ya rushwa."

Maafisa wengine wa Marekani waliogoma kuhojiwa kuhusu utajiri anaodaiwa kuwa nao Putin ambaye na Szubin pekee aliyekubali kushiriki kwenye uchuguzi huo uliofanywa na kipindi cha Panorama hata hivyo alikataa kutoa maoni yake kuhusu ripoti ya siri ya Shirika la kijasusi la CIA iliyotolewa mwaka 207 kuhusu utajiri wa Putin unaofikia dola bilion 40.

Mwaka 2008 Putin Mwenyewe alizielezea tuhuma kwamba ni ana utajiri mkubwa kuwa ni propaganda na hazina maana.Kuhusu tuhuma hizi za Rushwa Putin alikataa kuhojiwa na kipindi hicho cha Panorama.

Monday, 25 January 2016

Rais Dkt. J.P Magufuli 'atumbua majipu' Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa.

Rais Magufuli ameamuru kurudi nyumbani mabalozi sita haraka akiwemo Dr Batilda Buriani, Dr James Nsekela wa Italia na Peter Kalaghe wa Uingereza

Pia Mkurugenzi mkuu wa NIDA Bw Mwaimu amesimamishwa kazi kuanzia sasa.

Akitangaza hatua hiyo, Katibu mkuu kiongozi Ombeni sefue amesema Batilda na mabalozi wengine watano wamekuwa hawafanyi kazi kikamilifu ya kuiwakilisha nchi kama jinsi majukumu yao yanaavyoeleza.

Sefue amewataka mabalozi hao watatu kuondoka leo hii katika nchi waliko na kurudi Tanzania

Kuhusu Mwaimu, Sefue amesema yeye na vigogo wengine watatu wa NIDA wameaimamishwa kazi mara moja.

Aidha Rais Magufuli amemfukuza kazi Katibu Tawala mkoa wa Katavi Madeni Kipande kwa kushindwa kazi na Rais kutokuridhishwa na utendaji kazi wake.

Kipande aliteuliwa na JK kuwa katibu tawala Mkoa wa Katavi wiki moja kabla ya Magufuli Kuapishwa

==================

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

1.1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa Bwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia leo, tarehe 25 Januari, 2016.

1.2 Aidha, baada ya utenguzi huo, Bwana Dickson E. MAIMU amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao:

1.2.1 Bwana Joseph MAKANI, Mkurugenzi wa TEHAMA

1.2.2. Bi Rahel MAPANDE, Afisa Ugavi Mkuu

1.2.3 Bi Sabrina NYONI, Mkurugenzi wa Sheria

1.2.4 Bwana George NTALIMA, Afisa usafirishaji

1.3 Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni. Kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

1.4 Hivyo, Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.

1.5 Rais pia ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.

1.6 Rais vile vile ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

2.2Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa takapopangiwa kazi nyingine.

2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE

2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA

kuchaguliwa kuwa Mbunge.

2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray

MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

3.0 Tawala za Mikoa

3.1 Rais ametengua uteuzi wa Eng. Madeni Juma KIPANDE kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

4.0 Utumishi wa Umma

3.2 Nachukua nafasi hii kuwahimiza viongozi wote katika Utumishi wa Umma, na watumishi wote wa umma, kubadilika kwa dhati kwenye utendaji wao na uadilifu wao.

3.3 Napenda kusisitiza kuwa Rais na sisi tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine. Tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua. Mambo yafuatayo ni muhimu:

4.2.1 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu isipate kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi.

4.2.2 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu asipate kigugumizi kuchukua

hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.

4.2.3 Lazima uongozi na watumishi wa umma wawahudumie wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Kwa sababu hiyo:

a)Kila ofisi ya Serikali iwe na dawati la kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

b)Kwenye kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wajenge uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati. Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu anayeweza kumaliza matatizo yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu. Ikibidi wananchi wafike Ikulu ina maana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao.

c) Kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae majina yao ili iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati, na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo ya hovyo.

d) Kila ofisi ya Serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni ya wananchi

kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo, na kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Hizi ni tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo J'Tatu.

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal,
64, anakaribia kujiuzulu baada ya kukiri kuwa
amewaangusha mashabiki (Sun), Van Gaal
atakuwa na mazungumzo na makamu mwenyekiti wa United Ed Woodard kujadili jinsi ya kukatisha
mkataba wake unaokwenda hadi mwaka 2017
(Star), Woodward amezungumza na wachezaji
wakuu wa United kuhusiana na mikakati ya Van Gaal na anafikiria kumteua Ryan Giggs kuwa meneja hadi mwisho wa msimu (Mail), meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, 52, anazidi kupata matumaini ya kuwa meneja wa Manchester United (Times),

Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini
Manchester United wangekuwa tayari wamempa
kazi Jose Morinho, kama wangekuwa wanamtaka,
na anadhani wanasubiri hadi mwisho wa msimu
kujaribu kumchukua meneja wa Bayern Munich,
Pep Guardiola, 45, au Diego Simione, 45 kutoka
Atletico Madrid (Telegraph),

Liverpool wamekubaliana maslahi binafsi na Shaktar
Donetsk, kumsajili mshambuliaji Alex teixeira, 26
(Futbol Ukraine), hata hivyo bado hakuna
muafaka juu ya ada wanayotaka kutoa Liverpool
na bei iliyowekwa kwa mchezaji huyo kutoka
Brazil (Liverpool Echo),

Kiungo wa Fiorentina
Mario Suarez anafikiria kuhamia Watford (Mirror),

Roma wamethibitisha kuwa wanazungumza na
Jiangtsu Suning ya China kuhusiana na kumuuza
mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho,
28 (Guardian),

Mshambuliaji wa Atletico Madrid
Antoine Greizman, 24, amesema hana mpango
wa kuondoka Spain na kujiunga na Chelsea kwa
pauni milioni 75 (Telefoot),

Chelsea wamekuwa
wakimalizia kukamilisha usajili wa Alexandre
Pato, 26, kutoka Corinthians kwa mkopo, huku
wakitazamia kumsajili moja kwa moja baadaye
(Mail),

Newcastle wamepunguza kasi ya
kumnyatia winga wa Tottenham Andros
Townsend, 24 kutokana na Spurs kutaka pauni
milioni 14 (Sky Sports),

Newcastle wanaonekana
kufanikiwa kubaki na kiungo kutoka Ufaransa,
Moussa Sissoko, 26, lakini mchezaji huyo
amesema huenda akaondoka mwisho wa msimu (Sun),

Mshambuliaji wa Liverpool Christian
Benteke, 25, huenda akaondoka Anfield baada ya michuano ya Euro 2016 (Bleacher Report),

Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany, 29, anakabiliwa na jeraha jingine la msuli wa mguu na huenda asicheze kwa mwezi mmoja zaidi (Star).

Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa
kwenye magazeti ya leo Ulaya. Tetesi nyingine
kesho tukijaaliwa. Zimesalia siku saba kabla ya
dirisha hili la usajili kufungwa.

www.bantuz.com

Matokeo ya Mechi zote za Soka Jana J'Pili 25 katika Ligi Mbalimbali barani Ulaya.

MATOKEO YA SOKA JANA JUMAPILI 24/01/2016
★Barclays Premier League
Everton 1-2 Swansea City
Arsenal 0-1 Chelsea

★Spanish Primera División
Athletic Bilbao 5-2 Eibar
Atletico Madrid 0-0 Sevilla FC
Deportivo La Coruña 1-1 Valencia
Real Betis 1-1 Real Madrid

★German Bundesliga
Eintracht Frankfurt 3-2 VfL Wolfsburg
Schalke 04 1-3 Werder Bremen

★Italian Serie A
Fiorentina 2-0 Torino
Hellas Verona 1-1 Genoa
Internazionale 1-1 Carpi
Lazio 4-1 Chievo Verona
Palermo 4-1 Udinese
Sampdoria 2-4 Napoli
Sassuolo 0-2 Bologna
Juventus 1-0 AS Roma

★French Ligue 1
AS Monaco 4-0 Toulouse
Stade de Reims 1-1 St Etienne
Lyon 1-1 Marseille

~Abel Alvaro

Sunday, 24 January 2016

Ratiba ya Mechi zote za Soka leo Jumapili 24,Katika Ligi Mbalimbali barani Ulaya.

RATIBA YA SOKA LEO JUMAPILI 24/01/2016
★Barclays Premier League
4:30 PM - Everton vs Swansea City
7:00 PM - Arsenal vs Chelsea

★Spanish Primera División
2:00 PM - Athletic Bilbao vs Eibar
6:00 PM - Atletico Madrid vs Sevilla FC
8:15 PM - Deportivo La Coruña vs Valencia
10:30 PM - Real Betis vs Real Madrid

★German Bundesliga
5:30 PM - Eintracht Frankfurt vs VfL Wolfsburg
7:30 PM - Schalke 04 vs Werder Bremen

★Italian Serie A
2:30 PM - Fiorentina vs Torino
5:00 PM - Hellas Verona vs Genoa
5:00 PM - Internazionale vs Carpi
5:00 PM - Lazio vs Chievo Verona
5:00 PM - Palermo vs Udinese
5:00 PM - Sampdoria vs Napoli
5:00 PM - Sassuolo vs Bologna
10:45 PM - Juventus vs AS Roma

★French Ligue 1
4:00 PM - AS Monaco vs Toulouse
7:00 PM - Stade de Reims vs St Etienne
11:00 PM - Lyon vs Marseille

~Abel Alvaro

Matokeo ya Mechi zote za Jana Jumamosi,23 katika Ligi Mbalimbali barani Ulaya.


★Barclays Premier League
Norwich City 4-5 Liverpool
Crystal Palace 1-3 Tottenham Hotspur
Leicester City 3-0 Stoke City
Manchester United 0-1 Southampton
Sunderland 1-1 AFC Bournemouth
Watford 2-1 Newcastle United
West Bromwich Albion 0-0 Aston Villa
West Ham United 2-2 Manchester City

★Spanish Primera División
Malaga 1-2 Barcelona
Espanyol 2-2 Villarreal
Granada 3-2 Getafe
Rayo Vallecano 3-0 Celta Vigo

★German Bundesliga
FC Cologne 1-3 VfB Stuttgart
FC Ingolstadt 04 1-0 Mainz
Hannover 96 1-2 SV Darmstadt 98
Hertha Berlin 0-0 FC Augsburg
TSG Hoffenheim 1-1 Bayer Leverkusen
Borussia Monchengladbach 1-3 Borussia Dortmund

★Italian Serie A
Frosinone 0-0 Atalanta
Empoli 2-2 AC Milan

★French Ligue 1
Paris Saint-Germain 5-1 Angers
Guingamp 1-0 Bastia
Lille 1-3 Troyes
Montpellier 1-2 Caen
Nantes 2-2 Bordeaux
Nice 2-1 Lorient

~Abel Alvaro

Saturday, 23 January 2016

Chicharito Mchezaji Bora Amerika ya Kaskazini.

Hernandez ‘Chicharito’ ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Kanda ya Kisoka ya CONCACAF inayojumuisha Nchi za Marekani ya Kati na Kaskazini pamoja na Visiwa vya Carribean.

Tuzo hiyo imetokana na Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa pamoja na Wanahabari maalum na Mashabiki.

Baada ya kuihama Manchester United na kuhamia Klabu ya Bundesliga ya huko Germany, Bayer Leverkusen, Chicharito amewika mno na pia kuisaidia Nchi yake Mexico kuifunga USA 3-2, huku yeye akifunga 1, wakati wanafuzu kuiwakilisha CONACAF kwenye Fainali za Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara za 2017 zitakazochezwa huko Urusi.

Akitwaa Tuzo hii, Chicharito aliwabwaga Bryan Ruiz wa Costa Rica na Andres Guardado wa Mexico.

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA: NEYMAR, TEIXEIRA, MESSI, WENGER, ADEBAYOR, BERAHINO, KLOPP, THIAGO SILVA, PETR CECH

Manchester United na Manchester City watashindana kuipigania saini ya mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 23 (Chanzo Gazzetta)

United wanakaribia pia kumpata kiungo wa Benifica Renato Sanches, 18, na wanategemewa kulipa paundi millioni 30. (Chanzo Daily Mail)

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero ameongea na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 28, kuhusu kumshawishi kuhamia Manchester City. (Chanzo Sky Sports)

Wakati huo huo, Meneja wa City Manuel Pellegrini hatagemei kununua au kuuza mchezaji yoyote mwezi huu Januari (Chanzo Manchester Evening News)

Bosi wa Arsenal mzee Arsene Wenger, 66, anajiandaa kuongeza mkataba mpya na klabu ya Arsenal. (Chanzo Sun)

Washika Bunduki wanafikiria pia kuongeza dau la pili kwa beki wa kushoto wa Leicester City Ben Chilwell, 19, baada ya ofa ya paundi millioni 3.5 waliyoitoa awali kukataliwa. (Telegraph)

Bosi wa Manchester United Louis van Gaal anapanga kumchukua beki wa kushoto wa Southampton Ryan Bertrand, 26, lakini itamlazimu kulipa zaidi ya paundi millioni 20. (Chanzo Daily Star)

United wanaweza wakamchukua beki wa zamani wa Chelsea na Arsenal Ashley Cole. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 yuko huru kwa sasa baada ya kuondoka klabu ya Roma ya nchini Italia.(Chanzo Independent)

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema klabu yake haitoa pesa nyingi zaidi kwa mshambuliaji wa Shakhtar Donest Alex Teixeira, 26. (Chanzo Daily Telegraph)

Majagoo hao wa jiji bado wako kwenye mazungumzo na klabu ya nchini Ukrain Shakhtar juu ya makubaliano ya Teixeira, na wanafikiria kuongeza pesa kidogo kwenye ofa ya paundi millioni 24.6 waliyoitoa awali kwa mshambuliaji huyo wa Brazil. (Chanzo Guardian)

Chelsea wamewafata Paris St-German juu ya dili la kumsajili beki wa kati Thiago Silva, 31, mwishoni mwa msimu. (Chanzo Tuttomercatoweb – kwa Ligha ya Kiitalia)

Wakati huo huo, Chelsea wamemfanya kocha Massimiliano Allegri, 48, wa Juventus kuwa chagua la kwanza kama kocha atakayekuja kuingoza klabu hiyo msimu ujao. (Chanzo Sun)
Crystal Palace watalazimika kumlipa Adebayor paundi 77,000 kwa wiki endapo watataka kumsajili mshambuliaji huyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. (Chanzo Mirror)

Winga wa Tottenham Andros Townsend, 24, na mshambuliji wa West Brom Saido Berahino, 22, wanatamani kuhamia Newcastle – Lakini juhudi za Newcastle United kuwasajili wachezaji hao zinazidi kugonga mwamba. (Chanzo Newcastle Chronicle)

Swansea City wanaonekana kumtaka mshambuliaji wa Barcelana Sandros Ramirez, lakini wanaweza wakapata upinzani kutoka kwa Tottenham. (Chanzo Daily Mail)

Golikipa Petr Cech, 33, asingetakiwa kuondoka Chelsea, amesema bosi wa The Blues Hiddink.(Chanzo Times) Hizi ni baadhi ya habari tulizozipata leo,

Tetesi nyingine tukutane kesho panapo majaaliwa.

Man United yakaribia kunasa saini ya kiungo chipukizi Renato Sanchez.

Klabu ya Manchester United inakaribia kunasa saini ya kiungo Chipukizi mwenye miaka 18,Mreno Renato Sanchez anayekipiga katika klabu ya Benfica.

Kiungo huyo ameshafunga magoli mawili katika mechi 13 tangia alipopandishwa kutoka timu ya vijana ya Benfica.

Viongozi wa Manchester United walikutana na wawakilishi wa Renato hapo jana (Ijumaa) katika jiji la London huku kiungo huyo akiwa na kizuizi katika mkataba wake cha Paundi ml 60 lakini viongozi wa Manchester United wanajaribu kuwashawishi Benfica kushusha dau hilo.

Kiungo huyo ameweza kuteka macho ya Wadau mbalimbali wa soka hususan ufundi alionao na nguvu huku akifananishwa na kiungo wa zamani wa Uholanzi Edgar Devis.

www.bantuz.com

Ratiba ya Soka ligi mbalimbali barani Ulaya Leo Jumamosi.

RATIBA YA SOKA LEO JUMAMOSI 23/01/2016

★Barclays Premier League
3:45 PM - Norwich City vs Liverpool
6:00 PM - Crystal Palace vs Tottenham Hotspur
6:00 PM - Leicester City vs Stoke City
6:00 PM - Manchester United vs Southampton
6:00 PM - Sunderland vs AFC Bournemouth
6:00 PM - Watford vs Newcastle United
6:00 PM - West Bromwich Albion vs Aston Villa
8:30 PM - West Ham United vs Manchester City

★Spanish Primera División
6:00 PM - Malaga vs Barcelona
8:15 PM - Espanyol vs Villarreal
10:30 PM - Granada vs Getafe
24/01/2016
12:05 AM - Rayo Vallecano vs Celta Vigo

★German Bundesliga
5:30 PM - FC Cologne vs VfB Stuttgart
5:30 PM - FC Ingolstadt 04 vs Mainz
5:30 PM - Hannover 96 vs SV Darmstadt 98
5:30 PM - Hertha Berlin vs FC Augsburg
5:30 PM - TSG Hoffenheim vs Bayer Leverkusen
8:30 PM - Borussia Monchengladbach vs Borussia Dortmund

★Italian Serie A
8:00 PM - Frosinone vs Atalanta
10:45 PM - Empoli vs AC Milan

★French Ligue 1
7:00 PM - Paris Saint-
Germain vs Angers
10:00 PM - Guingamp vs Bastia
10:00 PM - Lille vs Troyes
10:00 PM - Montpellier vs Caen
10:00 PM - Nantes vs Bordeaux
10:00 PM - Nice vs Lorient

JANA

★Spanish Primera División
Sporting Gijon 5-1 Real Sociedad

★German Bundesliga
Hamburg SV 1-2 Bayern Munich

★French Ligue 1
Stade Rennes 1-0 GFC Ajaccio

~Abel Alvaro

Friday, 22 January 2016

Klabu ya Liverpool yakaribia kuinasa saini ya Mshambuliaji hatari Teixeira.

Liverpool inamuandama mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira huku Jurgen Klopp akijaribu kufanya usajili wa kwanza tangu alipokuwa mkufunzi wa Anfield.The Reds kama wanavyojiita wako tayari kulipa pauni milioni 24.5 kwa saini ya mchezaji huyo wa miaka 26.

Hatahivyo kilabu hiyo ya Ukraine inasema kuwa Texeira ambaye pia amehusishwa na uhamisho katika kilabu ya Chelsea atagharimu pauni milioni 39.Klopp anapanga kuimarisha safu yake ya mashambulizi huku Danny Ings,Divock Origi na Daniel Sturridge wakiwa wanauguza majeraha.

Huku Christian Benteke aliyeighrimu kilabu hiyo pauni milioni 32 akisalia,Liverpool imefunga mabao 25 pekee katika mechi 22 za ligi msimu huu.Shakhtar ambao wako katika mazoezi mjini Florida wanamthamini sana Texeira.
Amefunga mabao 22 katika mechi 15 na mabao manne katika mechi 10 za kilabu bingwa Ulaya simu huu.

Alianza kuchezea kilabu ya Vasco da Gama kabla ya kuelekea Shakhtar mwaka 2010.

Manchester United itakuja kuwa klabu namba 1 duniani kwa utajiri ifikapo 2017 na kuipiku Real Madrid.

Klabu ya Manchester United huenda ikawa klabu itakayokuwa ikipokea pesa nyingi zaidi duniani katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Kwa mujibu wa orodha ya mapato ya klabu iliyotayarishwa na kampuni ya Deloitte, miamba wa Uhispania Real Madrid kwa sasa wanaongoza kwa mwaka wa 11 mtawalia.

Klabu hiyo ilipata euro 577m (£439m) msimu wa 2014-15.
Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na euro 560.8m (£426.6m), huku United wakiwa nambari tatu kwa kujipatia euro 519.5m (£395.2m).

Lakini Deloitte wamesema kuna uwezekano mkubwa sana kwamba United huenda wakawa wamewapita Real Madrid wakati wa kutolewa kwa orodha ijayo.

Manchester United walishuka kutoka nambari mbili hadi nambari tatu baada ya kushuka kwa mapato yao lakini Deloitte wanasema “ukuaji thabiti wa kibiashara” wa Manchester United, pamoja na “uwezo wa kupata mikataba ya thamani kubwa ya uthamini” kama ule wa Adidas wa £75m kila mwaka, vimesaidia sana klabu hiyo.
Kutokana na mkataba mpya wa haki za utangazaji katika runinga wa thamani ya £5.1bn utakaoanza msimu wa 2016-17, Real Mdrid huenda ikatatizika kupata mapato ya juu.

Ligi ya Premia inaongoza kwa kuwa na klabu nyingi kwenye orodha ya klabu 30 tajiri, ikiwa na klabu 17.

Hii inatokana na mikataba mizuri ya utangazaji na upeperushaji wa mechi.
West Ham wamefika kwenye 20 bora kwa mara ya kwanza tangu 2005-06, baada ya kupata mapato ya euro 160.9m (£122.4m).

Manchester United waliongoza orodha hiyo, ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Deloitte Football Money League, ilipozinduliwa mwaka 1998, walipoandikisha mapato ya jumla ya £87.9m.

Wednesday, 20 January 2016

Matokeo ya Michezo Mbalimbali ya Soka iliyopigwa hapo Jana Barani Ulaya.

MATOKEO YA SOKA JANA JUMANNE 19/01/2016

★English FA Cup
Aston Villa 2-0 Wycombe Wanderers
Bradford City 0-0 Bury (Bury won in Shoot-out)
Bristol City 0-1 West Bromwich Albion
Milton Keynes Dons 3-0 Northampton Town
Portsmouth 2-1 Ipswich Town
Yeovil Town 1-1 Carlisle United (Carlisle won inbShoot-out)
Bolton Wanderers 3-2 Eastleigh
Reading 5-2 Huddersfield Town

★French Coupe de France
GFC Ajaccio 3-0 Guingamp
Stade Rennes 1-3 Bourg-Peronnas
Angers 1-2 Bordeaux
Bastia 1-2 Sochaux
US Sarre-Union 1-0 Niort
Paris Saint-Germain 2-1 Toulouse

★Italian Coppa Italia
Napoli 0-2 Internazionale

~Abel Alvaro

Ratiba ya Michezo Mbalimbali ya soka Barani Ulaya leo Jumatano

RATIBA YA SOKA LEO JUMATANO 20/01/2016
★English FA Cup 3rd Round Replay
10:45 PM - Leicester City vs Tottenham Hotspur
11:00 PM - Liverpool vs Exeter City

★Spanish Copa del Rey
10:30 PM - Celta Vigo vs Atletico Madrid
11:00 PM - Athletic Bilbao vs Barcelona

★Italian Serie A
10:45 PM - Sassuolo vs Torino

★French Coupe de France
8:30 PM - Chambly Thelle FC vs Lyon
8:30 PM - Concarneau vs Troyes
8:30 PM - Evian Thonon Gaillard vs AS Monaco
8:30 PM - Mantes 78 vs Nantes
8:30 PM - Trelissac FC vs Lille
9:30 PM - Boulogne vs Lorient
11:00 PM - Marseille vs Montpellier

★Italian Coppa Italia
10:45 PM - Lazio vs Juventus

~Abel Alvaro

Taarifa kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa kuhusiana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha Nchini.

Monday, 18 January 2016

Real Madrid,Barcelona zapeta ligi Kuu Hispania kwa ushindi mnono.

Klabu ya soka ya Real Madrid imefanikiwa kuizamisha Sporting Gijon katika mwendelezo wa ligi kuu ya Hispania kufuatia ushindi mnono wa mabao 5-1 ambayo yamefungwa na wachezaji Gareth Bale bao 1 , Chirstiano Ronaldo mabao 2 pamoja na Karem Benzema akifunga mabao 2.

Na klabu ya Barcelona imekwea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kufuatia ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Althltic Bilbao,mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Lionel Messi , Neymar da Silva Santos , Luis Alberto Suárez , na Ivan Rakitic .

Man United yapata ushindi mwembamba nyumbani kwa Liverpool.

Wayne Rooney alifunga bao lake la kwanza katika uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005 na kuiwezesha timu yake kupanda katika msimamo wa ligi ya Uingereza.

Liverpool ilitawala mchezo huo huku mkwaju wa Emre Can ukipanguliwa na kipa David De Gea.Lakini Liverpool walilazimika kulipa makosa yao wakati Wayne Rooney alipofunga mkwaju mzuri akiwa karibu na eneo la hatari baada ya kichwa cha Marouane Fellaini kugonga mwamba wa goli.

Wageni hao ambao sasa wako katika nafasi ya tano walikuwa hawajashambulia hata mkwaju mmoja katika lango la Liverpool hadi mshambuliaji huyo wa Uingereza alipofunga bao hilo la ushindi.Liverpool itasalia katika nafasi ya tisa ikiwa alama sita nyuma ya Manchester United.

Matokeo ya Soka katika Ligi mbalimbali barani Ulaya kwa Michezo ya Jana.

MATOKEO YA SOKA JANA JUMAPILI 17/01/2016:
••Barclays Premier League
Liverpool 0-1 Manchester United
Stoke City 0-0 Arsenal

••Spanish Primera División
Valencia 2-2 Rayo Vallecano
Real Madrid 5-1 Sporting Gijon
Getafe 3-1 Espanyol
Las Palmas 0-3 Atletico Madrid
Barcelona 6-0 Athletic Bilbao

••Italian Serie A
Genoa 4-0 Palermo
AS Roma 1-1 Hellas Verona
Bologna 2-2 Lazio
Carpi 2-1 Sampdoria
Chievo Verona 1-1 Empoli
Udinese 0-4 Juventus
AC Milan 2-0 Fiorentina

••French Ligue 1
Lorient 0-2 AS Monaco
Caen 1-3 Marseille
St Etienne 1-0 Lyon

~Abel Alvaro

Serikali yatoa ratiba mkutano wa Wazalishaji Umeme Wazalendo.

WAZALISHAJI UMEME WAZALENDO 

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM, Jumatatu, 18-1-2016: WIZARA ya Nishati na Madini imeandaa mkutano wa wazalishaji umeme wazalendo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar.

"Wizara itatoa ratiba kwa makampuni ya wazalendo kuja kutoa mapendekezo ya miradi yao tarehe 15-17 February 2016", alisema Prof Muhongo.

Prof Muhongo alisema mkutano huo utahusu miradi yote ya uzalishaji umeme kutoka vyanzo mbalimbali nchini.

Taarifa ya Waziri ilisema vikao na wadau hao vitafanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini.

"Iwapo kuna WABIA  kutoka nje ya nchi tungalipenda na hao WABIA wawepo kwenye vikao", alisema Waziri.

Tanzania itazalisha umeme wake kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Gesi Asilia (natural gas), Maji - Maporomoko (Hydro), Makaa ya Mawe (coal) na  Nishati Jadidifu  (Renewable Energies).

Vyanzo vingine ni Jua (solar), Upepo (wind) , Jotoardhi (geothermal) na  Mawimbi (tides&waves).

Alikitaja chanzo kingine ambacho mi maarufu kwa wananchi wengi wa kawaida kuwa ni Bio-Energies ambayo ni biogas (gesi ya kinyesi) na biomass (kuni).

Bantuz.Com

Sunday, 17 January 2016

Serikali yalifungia gazeti la 'Mawio'.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016 Serikali imelifuta Gazeti hilo ikiwa ni uamuzi uliotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).

Alieleza kuwa, hatua ya kulifuta gazeti hilo inazuia pia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.‘’Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu’’, alisema Nnauye.

Aidha, alifafanua kuwa hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.

‘’Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na Mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya  mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti,Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo’’ alisisitiza Mhe.

Nnauye.Katika hatua nyingine, Waziri nape alitoa pongezi kwa Vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi. ‘’Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja  na wahariri wa magazeti ya; Mwananchi Tanzania, Mtanzania, The East African, Magazeti ya Daily News na Habari Leo, Uhuru na mengineyo’’, alisema Mhe. Nnauye

WAZANZIBARI MNALIJUA HILI KUHUSU MAALIM SEIF?

Na Bollen Ngetti
Kuna baadhi ya wasomaji wa maandiko yangu wameendelea kunilaani na kudai ninamshambulia Maalim Seif na huenda nina chuki binafsi na mwanasiasa huyo wa Z'bar. Wengine wameenda mbali na kudai ninatumika! Ninachojua ni kwamba unaweza kumzuia ndege asitue juu ya kichwa chako lakini kamwe huwezi kumchagulia pa kujenga kiota chake. Sina chuki na Seif, situmiki maana si hulka yangu. Tatizo ni kuwa mimi ni muumini wa dhana ya ukweli hata kama ni mchungu kama "kloriti" ya Masai nitausema tu. Kuna baadhi ya Watu Z'bar kwa sasa hawataki kabisa kuambiwa ukweli maana unawachoma hadi kwenye mfupa.

Wengine wamenitukana huku wengine wakinitisha nakadhalika. Niwaambie tu kuwa nitaacha kusema tu ninachojua ni uongo lakini ukweli ninausema hadi mwisho wa uhai wangu maana bila kuyasema mambo haya mtaendelea kuishi ndani ya boksi jeusi.

Maalim Seif hana mkosi wa kumfanya asiwe Rais wa Z'bar isipokuwa ukweli mchungu ni kwamba amekosea hesabu katika mbio za kusaka Urais toka 1995, 2000,2005,2010,2015 na sasa 2016 na sasa wakati umeshamtupa mkono. Hawezi tena. Niharakishe kusema kwamba Seif anatafunwa na mzimu wa dhambi ya kumsaliti mwalimu wake mkuu wa siasa Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi na labda hili ndilo limemfuja.

Z'bar kwa asili ya Mila, jadi na ilivyojengeka na kuaminiwa na wengi ni kuwa huwezi kumsaliti, kumdharau ama kumdhihaki mwalimu wako wa skuli, amali, madrasa, au sheikh wako wa ilmu au wa kitwanga maana kufanya hivyo ima utapungukiwa na ibra njema au hutofanikiwa katika mbio za kusaka tija au mafanikio ya maisha yako.

Wengi hatujui ama hatutaki kujua ni kwa namna gani Seif aliweza kupenya hadi leo kuwa MAALIM na kuwa mwanasiasa mashuhuri kama walivyokuwa Profesa Abdulrahman Babu au Ali Muhsin Al-Barwan.

Mzee Jumbe alifanya ujasiri wa aina yake kumteua Seif kijana kutoka Pemba kuwa Waziri wa Elimu katika wakati wa siasa za mbinde kufuatia Mapinduzi ya damu yaliyofanywa na wakulima na wakwezi ambao wengi hawakuwa na elimu lakini pia ni kufuatia kuuawa kwa Rais Amani Karume aliyepigwa risasi na Homoud Mahmoud kijana mwenye asili ya uchotara wa ki-Arabu kama Maalim Seif kutoka Pemba.

Ikumbukwe kuwa ndani ASP (sasa CC.) kulijengeka dhana iliyojenga kiongozi wa ZPPP Mohammed Shamte Hamad mwenye asili ya Pemba kulikataa pendekezo la ASP mwaka 1963 la kumtaka aunde Serikali ya mseto yenye sura ya ki-Afrika lakini hakuliafiki na kuamua kupeleka viti vyake kwa ZNP-HIZBU na kuunda ZPPP/ZNP zikiwa na asili ya Upemba kupambana ASP (weusi wa Unguja).

Ni kweli kuwa Jumbe alihitaji wasomi maana alikuwa ni msomi lakini kumchukua mwanasiasa kutoka Pemba kumfanya mtu wa karibu ulikuwa ni ujasiri maana iliaminika kuwa mtu kutoka Pemba asingeweza kuwa mtetezi wa kweli wa mapinduzi ya mwaka 1964 (rejea maadhimisho ya juzi).

Hata hivyo jumbe hakujali pamona na kwamba hata Unguja kulikuwepo na vijana wasomi lakini Jumbe alitaka kuwaunganisha Wazanzibari na kuondoa dhana ovu ya u-Pemba na u-Unguja ambao sasa Seif anashutumiwa kuufufua kwa Ari mpya. Hata sasa Seif anashutumiwa kuwa machotara wa ki-Arabu ndio wenye sauti ndani ya CUF na ndio maana chama hicho kimeota mizizi Pemba tofauti na CCM iliyopo pande zote hata hakina nguvu kubwa kwa Pemba.

Karatasi za SIRI za Rais Jumbe zilizokuwa na mikakati ya kudai Serikali 3 ziliibwa ofisini kwa Jumbe zikakutwa mezani kwa Nyerere Dodoma, NEC huku Seif akiwa msatari wa mbele kumwambia Nyerere, "Mwl ukitaka muungano uendelee kumwondoe Jumbe kwenye Urais" na hata sasa kina Seif Khatib wanasema wazi, "Seif aliwasaliti Wazanzibari kupata kiti Chao UN nk."

Miongoni mwa wasemaji wakubwa katika mkutano huo wa NEC kutaka Jumbe abanduliwe nyadhifa zake abaki kapuku alikuwa Maalim Seif kwa mategemeo ya kutwaa Urais. Hapo mwanafunI anaamua kumsulubu mwalimu wake hadharani!

Mwalimu wake aliyemfanya agile hapo juu hadi sasa anataka avuliwe nguo hadharani. Hii kwa Wazanzibari ni laana mbaya sana na ishangaze leo huyo huyo aliyekataa serikali 3 leo anasafiria nyota ya Jumbe ya Serikali 3. Tuiteje hali hii kama si unafiki na uzandiki? Seif akawa kama Petro (Biblia) alivyomkana Bwana Yesu aliyekuwa kipenzi na msaidizi wake wa karibu.

Zama za Jumbe imebebeshwa lawama nyingi kuwa Wapemba walinyimwa elimu huku Waziri wa Elimu akiwa ni Mpemba. Mdaini elimu yenu.

Leo wapambe wanaliangalia kundi la machotara kutoka Pemba wakimuunga mkono Seif lakini hawaliangalii abadan lile la Waafrika weusi titii lilipo Unguja likilinga na kujenga hofu iliyowagusa Enzi za Maalim Seif akiwa Waziri wa Elimu na usaliti alioufanya dhidi ya Mzee Jumbe.

CUF bado ina nafasi ya kumpata mgombea Urais anayeweza kuunganisha visiwa vya Pemba na Unguja na ijulikane kuwa Maalim anatafuta Urais kwa ajili ya machotara wa Pemba na si kuunganisha Wazanzibari maana historia ni mwalimu mzuri. Mkataeni Seif kwa usalama, amani na umoja wa visiwa vya Zanzibar. Nawasilisha.

BNgetti 15/01/2016