Serikali ya Afghanistan
imetangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa kwa mamia ya watu
waliofukiwa katika kifusi cha udongo wakati maporomoko ya ardhi
yalipokifukia kijiji chao Ijumaa.
Gavana wa jimbo la Badakhshan, Shah Waliullah
Adib amesema kwamba kwa sasa hakuna matumaini ya kuwapata hai watu
zaidi ya 2,000 wanaoaminika kufukiwa katika nyumba zao.Maafisa wa serikali walihitimisha rasmi Jumamosi shughuli za utafutaji wa watu walionusurika.
Mashine za uchimbaji ziliondoka kijiji cha Ab Barik bila kutumika kutokana na eneo la tukio kutofikika kirahisi.
0 comments:
Post a Comment